Hata tusipokuamini
Wewe utabakia wa kuaminiwa
Heri mimi kukuamini
Maana umedhibitika wa kuaminiwa
Hakuna mtihani ule uliitwa
Kwako ukakosa jibiwa
Na hakuna jibu ulotoa
Likakosa jitosheleza
Nakuamini Yesu ee
Kiongozi wangu bora ee
Kama kipofu kwa fimbo yake
Sitakuacha ehe
Nakuamini Yesu ee
Kiongozi wangu bora ee
Kama kichanga kwa mama yake
Kuna wakati ulinisubirisha
Nusura nikate tamaa
Nikakumbuka wako wema
Imani yangu ikainuka
Kumbe ulikuwa waniimarisha
Hatua zangu kuzisogeza
Sasa mwendo nimeuanza
Na imani yangu kwako imesimama
Nakuamini Yesu ee
Kiongozi wangu bora ee
Kama kipofu kwa fimbo yake
Sitakuacha ehe
Nakuamini Yesu ee
Kiongozi wangu bora ee
Kama kichanga kwa mama yake
Naamini nguvu zako
Naamini uwezo wako
Upendo ni sifa yako
Naamini kazi zako
Naamini neno lako
Na yote uyafanyayo
Nakuamini Yesu ee
Kiongozi wangu bora ee
Kama kipofu kwa fimbo yake
Sitakuacha ehe
Nakuamini Yesu ee
Kiongozi wangu bora ee
Kama kichanga kwa mama yake
Sitakuacha ehe
Nakuamini Yesu ee
Kiongozi wangu bora ee
Kama kipofu kwa fimbo yake
Sitakuacha ehe
Nakuamini Yesu ee
Kiongozi wangu bora ee
Kama kichanga kwa mama yake
Sitakuacha ehe