Sifa Lyrics

Baba Natamani Kuwa Nawe by Eunice Njeri cover art

Eunice Njeri - Baba Natamani Kuwa Nawe Lyrics

Artist:
Eunice Njeri

Lyrics

Natamani, Baba natamani kuwa nawe

Kuishi nawe kukaa nawe, natamani
Yesu wewe wanitosha, Bwana wangu nakutamani


Baba natamani uwe wangu niwe wako
Chote kilicho changu kiwe ni chako pia
Upendo wako kwangu Yesu ni kama moto
Nimekukimbilia nisiabike milele lee Eh Baba


Baba natamani kuwa nawe

Kuishi nawe kukaa nawe, natamani
Yesu wewe wanitosha, Bwana wangu nakutamani


Baba nimeona upendo wako sio kwa mbali
Moyo wangu wafurahi ndani ya moyo wako
Nitakuinua umekuwa mwema kwangu
Pokea sifa Wewe umekuwa mwema kwangu, wewe mwema


Baba natamani kuwa nawe

Kuishi nawe kukaa nawe, natamani
Yesu wewe wanitosha, Bwana wangu nakutamani


Nitakuita hadi moyo wangu uzimie
Uniongoze kwenye mwamba ulio juu zaidi yangu
Nitakuita Bwana wangu unisikie
Ombi langu sifa zangu kilio changu
Ninapoomba (wanisikia eeh), Ninapoimba (wanisikia eeh)
Ninapolia mimi (wanisikia eeh), Ninapokuita, wanisikia eeh


Baba natamani kuwa nawe

Kuishi nawe kukaa nawe, natamani
Yesu wewe wanitosha, Bwana wangu nakutamani


Video