Lady Bee - Damu ya Yesu Lyrics

Lyrics

Damu ya Yesu inazungumza mema Damu ya Mwana kondoo inazungumza mema Inazungumza zungumza inazungumza mema Inazungumza zungumza inazungumza mema

Pale Calvary alisema yamekwisha Pale Calvary Yesu alisema yote yamekwisha Ni nani atakayeanza kazi yeye mwenyewe alimaliza Ni nani atakayemaliza kazi yeye mwenyewe aliyeanza

Damu ya mwokozi  Ilinitoa kwa minyororo ya dhambi Damu ya mwokozi  Ilinitoa kwa minyororo ya dhambi

Damu ya Yesu inazungumza mema Damu ya Mwana kondoo inazungumza mema Inazungumza zungumza inazungumza mema Inazungumza zungumza inazungumza mema

Wana wa Israeli  Walipaka damu kwa nyumba zao Wakati mwangamizi Alipita hakuruhusiwa

Kwa sababu ya damu Alipitapita juu Ila waliokosa alama ya damu Waliangamizwa

Leo kuna damu iondoae dhambi zote Leo kuna damu zaidi ya waliopaka Leo kuna damu iondoae dhambi zote

Damu ya Yesu inazungumza mema Damu ya Mwana kondoo inazungumza mema Inazungumza zungumza inazungumza mema Inazungumza zungumza inazungumza mema

Damu ya Yesu huponya magonjwa yote Inazungumza mema Saratani hata ukimwi inaponya magonjwa yote Inazungumza mema

Waliofungwa na adui damu ya Yesu inawakomboa Inazungumza mema Waliokosa amani damu ya Yesu inaleta amani Inazungumza mema

Video

Lady Bee-Damu Ya Yesu Official Video (SMS "Skiza 7913843 to 811)

Thumbnail for Damu ya Yesu video
Loading...
In Queue
View Lyrics