Ben Pol - Mama Lyrics

Contents: Song Information
  • Song Title: Mama Yeyoo (feat. Ben Pol)
  • Album: Mama Yeyoo (feat. Ben Pol) - Single
  • Artist: Ben Pol
  • Released On: 23 Apr 2013
  • Download/Stream: iTunes Music Amazon Music
Ben Pol Mama

Mama Lyrics

Ooooh mama
Mama ninakupenda mama
Mama ninakuheshimu mama
Mama ninakupenda mama
Mama ninakuheshimu mama

Miezi tisa eee ee
Mbumbumbu sijui lolote
Ila mama 
Wewe waniongelesha

Miezi tisa eee ee
Tumboni sijui lolote
Ila mama 
Kabisa uliningojea

Ukashona na sare
Kusubiri nianze shule
Wakasema chizi yule
Si angengoja akuwe

Eeh, mama siwezi kukulipa mimi
Uliyonipa hayanunuliki
Upendo wako mi sitosheki
Jembe jembe mama nakukubali wewe

Ooooh mama
Mama ninakupenda mama
Mama ninakuheshimu mama
Mama ninakupenda mama
Mama ninakuheshimu mama

Aah aah, ukitoa Mungu
Mbunge ni wewe ni wewe ni wewe
Waziri ni wewe ni wewe ni wewe
Rais ni wewe ni wewe ni wewe mama
Kila kitu ni wewe ni wewe ni wewe

Aah, nitanunua na kanga zenye maneno mazuri uone
Aaah tena nitazichanga na sarafu nikupe uchune
Aah, nitanunua na Kanga zenye maneno mazuri uone
Aaah tena nikizichanga nitakupa na noti uone eeh mama

Sijasahau sadaka zako kutoka moyoni
Uliponipa wakati mama yangu hauna
Sijasahau sadaka zako kutoka moyoni mama
Uliponipa mama wakati wewe hauna

Tena kama ukiina mama, jua ninakuthamini
Na moyoni mwangu nimekuweka mama
Tena nikiina mama, jua ninakuthamini
Na moyoni mwangu nimekuweka mama

Oh kipenzi ooh kipenzi oh kipenzi oh
Oh mpenzi ooh mpenzi oh mpenzi oh

Mama ninakupenda mama
Mama ninakuheshimu mama
Mama ninakupenda mama
Mama ninakuheshimu mama

Mama ninakupenda mama
Mama ninakuheshimu mama

Asante kwa malezi
Asante kwa vitumbua
Asante kwa chapati
Asante kwa kunikung’uta

Asante kwa malezi
Asante kwa vibajia
Asante kwa mandazi
Asante kwa kunipa bua
 
(Asante)


Ben Pol Songs

Related Songs