Zekaria 10 Swahili & English

Listen/Download Audio
Zekaria 10 (Swahili) Zechariah 10 (English)

Mwombeni Bwana mvua wakati wa masika, naam, Bwana afanyaye umeme, naye atawapa manyunyu ya mvua, kila mtu atapewa nyasi kondeni. Zekaria 10:1

Ask of Yahweh rain in the spring time, Yahweh who makes storm clouds, And he gives rain showers to everyone for the plants in the field.

Kwa maana vinyago vimenena maneno ya ubatili, nao waaguzi wameona uongo; nao wameleta habari za ndoto za uongo, wafariji bure; kwa sababu hiyo waenda zao kama kondoo, wateswa, kwa sababu hapana mchungaji. Zekaria 10:2

For the teraphim have spoken vanity, and the diviners have seen a lie; And they have told false dreams. They comfort in vain. Therefore they go their way like sheep. They are oppressed, because there is no shepherd.

Hasira yangu imewaka juu ya wachungaji, nami nitawaadhibu mbuzi waume; kwa maana Bwana wa majeshi ameliangalia kundi lake, yaani, nyumba ya Yuda, naye atawafanya kuwa kama farasi wake mzuri vitani. Zekaria 10:3

My anger is kindled against the shepherds, And I will punish the male goats; For Yahweh of Hosts has visited his flock, the house of Judah, And will make them as his horse in the battle that he is proud of.

Kwake yeye litatoka lile jiwe la pembeni, kwake yeye utatoka msumari, kwake yeye utatoka upinde wa vita, kwake yeye atatoka kila mtawala pamoja. Zekaria 10:4

From him will come forth the corner-stone, From him the nail, From him the battle bow, From him every ruler together.

Nao watakuwa kama mashujaa, wakanyagao adui zao katika matope ya njia vitani; nao watapiga vita, kwa sababu Bwana yu pamoja nao; na hao wapandao farasi watafadhaishwa. Zekaria 10:5

They shall be as mighty men, Treading down muddy streets in the battle; And they shall fight, because Yahweh is with them; And the riders on horses will be confounded.

Nami nitaitia nguvu nyumba ya Yuda, nami nitaiokoa nyumba ya Yusufu, nami nitawarudisha, kwa maana nawaonea rehema; nao watakuwa kana kwamba sikuwatupa; kwa maana mimi ni Bwana, Mungu wao, nami nitawasikia. Zekaria 10:6

"I will strengthen the house of Judah, And I will save the house of Joseph, And I will bring them back; For I have mercy on them; And they will be as though I had not cast them off: For I am Yahweh their God, and I will hear them.

Na watu wa Efraimu watakuwa kama shujaa, na moyo wao utafurahi kana kwamba ni kwa divai; naam, watoto wao wataona mambo haya, na kufurahi; mioyo yao itamfurahia Bwana. Zekaria 10:7

Ephraim will be like a mighty man, And their heart will rejoice as through wine; Yes, their children will see it, and rejoice. Their heart will be glad in Yahweh.

Nitawapigia kelele, na kuwakusanya pamoja; kwa maana nimewakomboa; nao wataongezeka kama walivyoongezeka. Zekaria 10:8

I will signal for them, and gather them; For I have redeemed them; And they will increase as they have increased.

Nami nitawapanda kama mbegu kati ya mataifa; nao watanikumbuka katika nchi zilizo mbali; nao watakaa pamoja na watoto wao; tena watarudi. Zekaria 10:9

I will sow them among the peoples; And they will remember me in far countries; And they will live with their children, and will return.

Tena nitawarudisha toka nchi ya Misri, nitawakusanya na kuwatoa katika Ashuru; nami nitawaingiza katika nchi ya Gileadi na Lebanoni; ila nafasi ya kuwatosha haitaonekana. Zekaria 10:10

I will bring them again also out of the land of Egypt, And gather them out of Assyria; And I will bring them into the land of Gilead and Lebanon; And there won't be room enough for them.

Naye atapita kati ya bahari ya mateso, na kuyapiga mawimbi ya bahari, na vilindi vyote vya mto wa Nile vitakauka; na kiburi cha Ashuru kitashushwa; na fimbo ya enzi ya Misri itatoweka. Zekaria 10:11

He will pass through the sea of affliction, And will strike the waves in the sea, And all the depths of the Nile will dry up; And the pride of Assyria will be brought down, And the scepter of Egypt will depart.

Nami nitawatia nguvu katika Bwana; nao watatembea huko na huko katika jina lake, asema Bwana. Zekaria 10:12

I will strengthen them in Yahweh; And they will walk up and down in his name," says Yahweh.