2 Samweli 8 Swahili & English

Listen/Download Audio
2 Samweli 8 (Swahili) 2nd Samuel 8 (English)

Ikawa baadaye, Daudi akawapiga Wafilisti, akawashinda; Daudi akautwaa Gathi na vijiji vyake mikononi mwa hao Wafilisti. 2 Samweli 8:1

After this it happened that David struck the Philistines, and subdued them: and David took the bridle of the mother city out of the hand of the Philistines.

Akapiga Moabu, akawapima kwa kamba hali wamelazwa chini; akapima kamba mbili za kuuawa, na kamba moja nzima ya kuhifadhi hai. Wamoabi wakawa watumwa wa Daudi, wakaleta zawadi. 2 Samweli 8:2

He struck Moab, and measured them with the line, making them to lie down on the ground; and he measured two lines to put to death, and one full line to keep alive. The Moabites became servants to David, and brought tribute.

Tena Daudi akampiga Hadadezeri mwana wa Rehobu, mfalme wa Soba, alipokwenda kujipatia tena mamlaka yake huko Mtoni. 2 Samweli 8:3

David struck also Hadadezer the son of Rehob, king of Zobah, as he went to recover his dominion at the River.

Daudi akampokonya wapanda farasi elfu na mia saba na askari waliokwenda kwa miguu ishirini elfu; Daudi akawakata mshipa farasi wote wa magari, ila farasi wa magari mia akawasaza. 2 Samweli 8:4

David took from him one thousand seven hundred horsemen, and twenty thousand footmen: and David hamstrung all the chariot horses, but reserved of them for one hundred chariots.

Na Washami wa Dameski walipokuja kumsaidia Hadadezeri, mfalme wa Soba, Daudi akawapiga wa Washami watu ishirini na mbili elfu. 2 Samweli 8:5

When the Syrians of Damascus came to help Hadadezer king of Zobah, David struck of the Syrians two and twenty thousand men.

Daudi akaweka ngome katika Shamu ya Dameski, na hao Washami wakawa watumwa wa Daudi, wakaleta zawadi. Naye Bwana akampa Daudi kushinda kila alikokwenda. 2 Samweli 8:6

Then David put garrisons in Syria of Damascus; and the Syrians became servants to David, and brought tribute. Yahweh gave victory to David wherever he went.

Tena Daudi akazitwaa ngao za dhahabu zilizovaliwa na watumwa wa Hadadezeri, akazileta Yerusalemu. 2 Samweli 8:7

David took the shields of gold that were on the servants of Hadadezer, and brought them to Jerusalem.

Tena toka Tebhathi na toka Berothai, miji ya Hadadezeri, Daudi akatwaa shaba nyingi mno. 2 Samweli 8:8

From Betah and from Berothai, cities of Hadadezer, king David took exceeding much brass.

Na Tou, mfalme wa Hamathi, aliposikia ya kwamba Daudi amewapiga jeshi lote la Hadadezeri, 2 Samweli 8:9

When Toi king of Hamath heard that David had struck all the host of Hadadezer,

Tou akamtuma kwa Daudi Hadoramu mwanawe kusalimia, na kumbarikia, kwa sababu amepigana na Hadadezeri, na kumpiga; kwa maana Hadadezeri alikuwa amepigana vita juu ya Tou. Na mkononi mwake akaleta vyombo vya fedha, na vyombo vya dhahabu, na vyombo vya shaba; 2 Samweli 8:10

then Toi sent Joram his son to king David, to Greet him, and to bless him, because he had fought against Hadadezer and struck him: for Hadadezer had wars with Toi. [Joram] brought with him vessels of silver, and vessels of gold, and vessels of brass:

hivi pia mfalme Daudi akavifanya wakfu kwa Bwana, pamoja na hiyo fedha, na dhahabu alizofanya wakfu za mataifa yote aliowashinda; 2 Samweli 8:11

These also did king David dedicate to Yahweh, with the silver and gold that he dedicated of all the nations which he subdued;

za Edomu, na za Moabu, na za wana wa Amoni, na za Wafilisti, na za Amaleki, na za nyara za Hadadezeri, mwana wa Rehobu, mfalme wa Soba. 2 Samweli 8:12

of Syria, and of Moab, and of the children of Ammon, and of the Philistines, and of Amalek, and of the spoil of Hadadezer, son of Rehob, king of Zobah.

Basi Daudi akajipatia jina, aliporudi kutoka kuwapiga Waedomi katika Bonde la Chumvi, watu kumi na nane elfu. 2 Samweli 8:13

David got him a name when he returned from smiting the Syrians in the Valley of Salt, even eighteen thousand men.

Akaweka askari wenye kulinda ngome katika Edomu; katikati ya Edomu yote akaweka ngome, na Waedomi wote wakawa watumwa wa Daudi. Naye Bwana akampa Daudi kushinda kila alikokwenda. 2 Samweli 8:14

He put garrisons in Edom; throughout all Edom put he garrisons, and all the Edomites became servants to David. Yahweh gave victory to David wherever he went.

Daudi akatawala juu ya Israeli wote; naye Daudi akawafanyia hukumu na haki watu wake wote. 2 Samweli 8:15

David reigned over all Israel; and David executed justice and righteousness to all his people.

Huyo Yoabu, mwana wa Seruya alikuwa juu ya jeshi; na Yehoshafati, mwana wa Ahiludi, mwenye kuandika tarehe; 2 Samweli 8:16

Joab the son of Zeruiah was over the host; and Jehoshaphat the son of Ahilud was recorder;

na Sadoki, mwana wa Ahitubu, na Ahimeleki, mwana wa Abiathari walikuwa makuhani; na Shausha mwandishi; 2 Samweli 8:17

and Zadok the son of Ahitub, and Ahimelech the son of Abiathar, were priests; and Seraiah was scribe;

na Benaya, mwana wa Yehoyada, alikuwa juu ya Wakerethi na Wapelethi; nao wana wa Daudi wakawa makuhani.

2 Samweli 8:18

and Benaiah the son of Jehoiada [was over] the Cherethites and the Pelethites; and David's sons were chief ministers.