2 Samweli 19 Swahili & English

Listen/Download Audio
2 Samweli 19 (Swahili) 2nd Samuel 19 (English)

Kisha Yoabu akaambiwa, Angalia, mfalme anamlilia Absalomu na kumwombolezea. 2 Samweli 19:1

It was told Joab, Behold, the king weeps and mourns for Absalom.

Na kushinda kwao vitani siku ile kukageuzwa kuwa maombolezo kwa watu wote; maana watu walisikia siku ile ya kwamba, Mfalme anahuzunika kwa ajili ya mwanawe. 2 Samweli 19:2

The victory that day was turned into mourning to all the people; for the people heard say that day, The king grieves for his son.

Watu wakajificha siku ile, wakaingia mjini kama vile watu waonao fedheha wajifichavyo, hapo wakimbiapo vitani. 2 Samweli 19:3

The people got them by stealth that day into the city, as people who are ashamed steal away when they flee in battle.

Mfalme akajifunika uso; na mfalme akalia kwa sauti kuu, Mwanangu Absalomu, Absalomu, mwanangu, mwanangu! 2 Samweli 19:4

The king covered his face, and the king cried with a loud voice, my son Absalom, Absalom, my son, my son!

Basi Yoabu akaingia nyumbani kwa mfalme, akasema, Wewe leo umefedhehesha nyuso za watumishi wako wote, waliokuokoa leo roho yako, na roho za wanao, na za binti zako, na roho za wakezo, na roho za masuria wako; 2 Samweli 19:5

Joab came into the house to the king, and said, You have shamed this day the faces of all your servants, who this day have saved your life, and the lives of your sons and of your daughters, and the lives of your wives, and the lives of your concubines;

kwa kuwa unawapenda wakuchukiao, na unawachukia wakupendao. Maana umetangaza leo ya kuwa wakuu na watumishi wako si kitu kwako; maana leo nimetambua hivi; kama Absalomu angaliishi, na sisi sote tungalikufa leo, ingalikuwa vyema machoni pako. 2 Samweli 19:6

in that you love those who hate you, and hate those who love you. For you have declared this day, that princes and servants are nothing to you: for this day I perceive that if Absalom had lived, and all we had died this day, then it had pleased you well.

Basi sasa, ondoka, utoke nje, ukaseme na watumishi wako maneno ya kuwatuliza roho zao; maana mimi nakuapia kwa Bwana, usipotoka, hatabaki hata mtu mmoja pamoja nawe usiku huu; na mambo haya yatakuwa mabaya kwako kuliko mabaya yote yaliyokupata tokea ujana wako hata sasa. 2 Samweli 19:7

Now therefore arise, go forth, and speak comfortably to your servants; for I swear by Yahweh, if you don't go forth, there will not stay a man with you this night: and that will be worse to you than all the evil that has happened to you from your youth until now.

Ndipo mfalme akaondoka, akaketi langoni. Nao wote wakaambiwa ya kwamba, Angalieni, mfalme ameketi langoni; watu wote wakaenda huko mbele ya mfalme. Basi, Israeli wote walikuwa wamekimbia kila mtu hemani kwake. 2 Samweli 19:8

Then the king arose, and sat in the gate. They told to all the people, saying, Behold, the king is sitting in the gate: and all the people came before the king. Now Israel had fled every man to his tent.

Wakashindana watu wote katika kabila zote za Israeli, wakisema, Mfalme alitutoa mikononi mwa adui zetu, akatuokoa mikononi mwa Wafilisti; naye sasa amekimbia kutoka nchi hii mbele ya Absalomu. 2 Samweli 19:9

All the people were at strife throughout all the tribes of Israel, saying, The king delivered us out of the hand of our enemies, and he saved us out of the hand of the Philistines; and now he is fled out of the land from Absalom.

Na huyo Absalomu, tuliyemtia mafuta ili awe juu yetu, amekufa vitani. Basi sasa mbona ninyi hamsemi neno lo lote juu ya kumrudisha tena mfalme? 2 Samweli 19:10

Absalom, whom we anointed over us, is dead in battle. Now therefore why don't you speak a word of bringing the king back?

Naye mfalme Daudi akatuma kwa Sadoki na Abiathari, makuhani, kusema, Neneni na wazee wa Yuda, mkisema, Kwa nini ninyi mmekuwa wa mwisho wa kumrudisha tena mfalme nyumbani kwake? Kwa maana maneno ya Israeli wote yamemjia mfalme, ili kumleta nyumbani kwake. 2 Samweli 19:11

King David sent to Zadok and to Abiathar the priests, saying, Speak to the elders of Judah, saying, Why are you the last to bring the king back to his house? seeing the speech of all Israel is come to the king, [to bring him] to his house.

Ninyi ni ndugu zangu, ninyi ni mfupa wangu na nyama yangu; mbona basi ninyi mmekuwa wa mwisho wa kumrudisha tena mfalme. 2 Samweli 19:12

You are my brothers, you are my bone and my flesh: why then are you the last to bring back the king?

Kisha mkamwambie Amasa, Je! Si wewe uliye mfupa wangu, na nyama yangu? Mungu anifanyie hivyo, na kuzidi, usipokuwa wewe jemadari wa jeshi mbele yangu daima mahali pa Yoabu. 2 Samweli 19:13

Say you to Amasa, Aren't you my bone and my flesh? God do so to me, and more also, if you aren't captain of the host before me continually in the room of Joab.

Akawainamisha mioyo watu wote wa Yuda, kama mtu mmoja; basi wakatuma kwa mfalme, Rudi wewe na watumishi wako wote. 2 Samweli 19:14

He bowed the heart of all the men of Judah, even as [the heart of] one man; so that they sent to the king, [saying], Return you, and all your servants.

Hivyo mfalme akarudi, akafika Yordani. Kisha Yuda wakaja Gilgali kwenda kumlaki mfalme, na kumvusha mfalme Yordani. 2 Samweli 19:15

So the king returned, and came to the Jordan. Judah came to Gilgal, to go to meet the king, to bring the king over the Jordan.

Akafanya haraka Shimei, mwana wa Gera, Mbenyamini, wa Bahurimu akashuka pamoja na watu wa Yuda ili kumlaki mfalme Daudi. 2 Samweli 19:16

Shimei the son of Gera, the Benjamite, who was of Bahurim, hurried and came down with the men of Judah to meet king David.

Na Watu elfu wa Benyamini walikuwa pamoja naye, na huyo Siba mtumwa, nyumba ya Sauli, na hao wanawe kumi na watano, na watumwa wake ishirini pamoja naye; wakavuka Yordani mbele ya mfalme. 2 Samweli 19:17

There were a thousand men of Benjamin with him, and Ziba the servant of the house of Saul, and his fifteen sons and his twenty servants with him; and they went through the Jordan in the presence of the king.

Tena ikavuka mashua ili kuwavusha jamaa ya mfalme, na kufanya aliyoyaona kuwa mema. Ndipo Shimei, mwana wa Gera, akamwangukia mfalme alipokuwa amevuka Yordani. 2 Samweli 19:18

There went over a ferry-boat to bring over the king's household, and to do what he thought good. Shimei the son of Gera fell down before the king, when he was come over the Jordan.

Akamwambia mfalme, Bwana wangu asinihesabie uovu, wala usiyakumbuke yale niliyoyatenda mimi mtumwa wako kwa upotoe siku ile alipotoka Yerusalemu bwana wangu mfalme, hata mfalme ayatie moyoni mwake. 2 Samweli 19:19

He said to the king, Don't let my lord impute iniquity to me, neither do you remember that which your servant did perversely the day that my lord the king went out of Jerusalem, that the king should take it to his heart.

Kwa kuwa mimi mtumwa wako najua ya kwamba nimekosa; kwa hiyo, tazama, nimekuja leo, wa kwanza wa nyumba yote ya Yusufu, kushuka ili nimlaki bwana wangu mfalme. 2 Samweli 19:20

For your servant does know that I have sinned: therefore, behold, I am come this day the first of all the house of Joseph to go down to meet my lord the king.

Lakini Abishai, mwana wa Seruya, akajibu na kusema, Je! Shimei hatauawa kwa sababu hii, kwa kuwa amemlaani masihi wa BWANA? 2 Samweli 19:21

But Abishai the son of Zeruiah answered, Shall Shimei not be put to death for this, because he cursed Yahweh's anointed?

Lakini Daudi akasema, Mimi nina nini nanyi, enyi wana wa Seruya, hata mmekuwa adui zangu leo? Je! Atauawa mtu ye yote leo katika Israeli? Kwa maana sijui mimi leo ya kwamba ndimi mfalme juu ya Israeli? 2 Samweli 19:22

David said, What have I to do with you, you sons of Zeruiah, that you should this day be adversaries to me? shall there any man be put to death this day in Israel? for don't I know that I am this day king over Israel?

Kisha mfalme akamwambia Shimei, Hutakufa. Mfalme akamwapia. 2 Samweli 19:23

The king said to Shimei, You shall not die. The king swore to him.

Kisha Mefiboshethi, mwana wa Sauli, akashuka ili amlaki mfalme; alikuwa hakukata kucha za miguu yake wala kukata ndevu zake, wala kufua nguo zake, tangu siku alipoondoka mfalme, hata siku hiyo aliporudi kwake kwa amani. 2 Samweli 19:24

Mephibosheth the son of Saul came down to meet the king; and he had neither dressed his feet, nor trimmed his beard, nor washed his clothes, from the day the king departed until the day he came home in peace.

Basi ikawa, alipofika Yerusalemu kumlaki mfalme, mfalme akamwambia, Mbona hukwenda pamoja nami, Mefiboshethi? 2 Samweli 19:25

It happened, when he was come to Jerusalem to meet the king, that the king said to him, Why didn't you go with me, Mephibosheth?

Naye akajibu, Bwana wangu, Ee mfalme, mtumwa wangu alinidanganya; kwa kuwa mimi mtumwa wako nilisema, Nitajitandikia punda, nipate kumpanda, na kwenda pamoja na mfalme; kwa sababu mimi mtumwa wako ni kiwete. 2 Samweli 19:26

He answered, My lord, O king, my servant deceived me: for your servant said, I will saddle me a donkey, that I may ride thereon, and go with the king; because your servant is lame.

Naye amenisingizia mimi mtumwa wako kwa bwana wangu mfalme; lakini bwana wangu mfalme ni kama malaika wa Mungu; utende basi yaliyo mema machoni pako. 2 Samweli 19:27

He has slandered your servant to my lord the king; but my lord the king is as an angel of God: do therefore what is good in your eyes.

Kwa kuwa jamaa yote ya baba yangu walikuwa kama watu wa kufa tu mbele ya bwana wangu mfalme; ila uliniweka mimi mtumwa wako kati ya hao walao mezani pako. Basi ni haki gani sasa niliyo nayo, hata nimlilie mfalme zaidi? 2 Samweli 19:28

For all my father's house were but dead men before my lord the king; yet you set your servant among those who ate at your own table. What right therefore have I yet that I should cry any more to the king?

Basi mfalme akamwambia, Kwa nini unazidi kuyanena mambo yako? Mimi naamua, Wewe na Siba mwigawanye hiyo nchi. 2 Samweli 19:29

The king said to him, Why speak you any more of your matters? I say, You and Ziba divide the land.

Naye Mefiboshethi akamwambia mfalme, Naam, hata yote na atwae yeye, kwa kuwa bwana wangu mfalme amekuja kwa amani nyumbani kwake. 2 Samweli 19:30

Mephibosheth said to the king, yes, let him take all, because my lord the king is come in peace to his own house.

Tena Barzilai, Mgileadi, akashuka kutoka Rogelimu; akavuka Yordani pamoja na mfalme, amvushe Yordani. 2 Samweli 19:31

Barzillai the Gileadite came down from Rogelim; and he went over the Jordan with the king, to conduct him over the Jordan.

Naye huyo Barzilai alikuwa mzee sana, amepata umri wa miaka themanini; naye amemlisha mfalme hapo alipokuwapo Mahanaimu; kwa kuwa alikuwa mtu mwenye cheo kikubwa. 2 Samweli 19:32

Now Barzillai was a very aged man, even eighty years old: and he had provided the king with sustenance while he lay at Mahanaim; for he was a very great man.

Naye mfalme akamwambia Barzilai, Uvuke pamoja nami; nami nitakulisha kwangu huko Yerusalemu. 2 Samweli 19:33

The king said to Barzillai, Come you over with me, and I will sustain you with me in Jerusalem.

Lakini Barzilai akamjibu mfalme, Siku ni ngapi za miaka ya maisha yangu, hata mimi nipande pamoja na mfalme kwenda Yerusalemu? 2 Samweli 19:34

Barzillai said to the king, How many are the days of the years of my life, that I should go up with the king to Jerusalem?

Nimepata leo miaka themanini; nami je! Naweza kupambanua mema na mabaya? Mimi mtumwa wako, je! Naweza kuonja nilacho au ninywacho? Naweza kusikia tena sauti ya waimbaji waume na wake? Kwa nini basi mtumwa wako amlemee bado bwana wangu mfalme? 2 Samweli 19:35

I am this day eighty years old: can I discern between good and bad? can your servant taste what I eat or what I drink? can I hear any more the voice of singing men and singing women? why then should your servant be yet a burden to my lord the king?

Mtumwa wako ataka kuvuka Yordani tu pamoja na mfalme; tena mbona mfalme anilipie thawabu ya namna hii? 2 Samweli 19:36

Your servant would but just go over the Jordan with the king: and why should the king recompense it me with such a reward?

Niache nirudi basi, mimi mtumwa wako, ili nife katika mji wangu mwenyewe, karibu na kaburi la baba yangu na la mama yangu. Lakini tazama, mtumwa wako Kimhamu; na avuke yeye pamoja na bwana wangu mfalme; nawe ukamtendee yeye yaliyo mema machoni pako. 2 Samweli 19:37

Please let your servant turn back again, that I may die in my own city, by the grave of my father and my mother. But behold, your servant Chimham; let him go over with my lord the king; and do to him what shall seem good to you.

Mfalme akajibu, Haya, Kimhamu na avuke pamoja nami, nami nitamtendea yaliyo mema machoni pako wewe; na kila utakalotaka kwangu, mimi nitalifanya kwa ajili yako. 2 Samweli 19:38

The king answered, Chimham shall go over with me, and I will do to him that which shall seem good to you: and whatever you shall require of me, that will I do for you.

Basi watu wote wakavuka Yordani, naye mfalme akavuka; kisha mfalme akambusu Barzilai, akambariki; naye akarejea mahali pake. 2 Samweli 19:39

All the people went over the Jordan, and the king went over: and the king kissed Barzillai, and blessed him; and he returned to his own place.

Hivyo mfalme akavuka, akafika Gilgali; Kimhamu akavuka pamoja naye; na watu wote wa Yuda wakamvusha mfalme, na nusu ya watu wa Israeli. 2 Samweli 19:40

So the king went over to Gilgal, and Chimham went over with him: and all the people of Judah brought the king over, and also half the people of Israel.

Tena, angalia, watu wote wa Israeli wakamjia mfalme wakamwambia mfalme, Kwa nini ndugu zetu, watu wa Yuda wamekuiba, na kumvusha Yordani mfalme, na jamaa yake, na watu wote wa Daudi pamoja naye? 2 Samweli 19:41

Behold, all the men of Israel came to the king, and said to the king, Why have our brothers the men of Judah stolen you away, and brought the king, and his household, over the Jordan, and all David's men with him?

Ndipo watu wote wa Yuda wakawajibu hao watu wa Israeli, Ni kwa sababu mfalme ndiye wa jamaa yetu; mbona basi ninyi mmekasirika kwa ajili ya jambo hili? Je! Sisi tumekula kitu cha mfalme? Ama ametupa sisi zawadi yo yote? 2 Samweli 19:42

All the men of Judah answered the men of Israel, Because the king is a close relative to us: why then are you angry for this matter? have we eaten at all at the king's cost? or has he given us any gift?

Hao watu wa Israeli wakawajibu watu wa Yuda, wakasema, Sisi tunazo sehemu kumi katika mfalme, tena tunayo haki yetu katika Daudi zaidi kuliko ninyi; mbona basi ninyi mmetudharau sisi, lisitakwe kwanza shauri letu katika kumrudisha tena mfalme wetu? Na maneno ya watu wa Yuda yakawa makali kuliko maneno ya watu wa Israeli. 2 Samweli 19:43

The men of Israel answered the men of Judah, and said, We have ten parts in the king, and we have also more [right] in David than you: why then did you despise us, that our advice should not be first had in bringing back our king? The words of the men of Judah were fiercer than the words of the men of Israel.