2 Samweli 23 Swahili & English

Listen/Download Audio
2 Samweli 23 (Swahili) 2nd Samuel 23 (English)

Basi haya ndiyo maneno ya mwisho ya Daudi. Daudi, mwana wa Yese, anena, anena huyo mtu aliyeinuliwa juu, Yeye, masihi wake Mungu wa Yakobo,Mtungaji wa nyimbo za Israeli mwenye kupendeza; 2 Samweli 23:1

Now these are the last words of David. David the son of Jesse says, The man who was raised on high says, The anointed of the God of Jacob, The sweet psalmist of Israel:

Roho ya Bwana ilinena ndani yangu, Na neno lake likawa ulimini mwangu. 2 Samweli 23:2

The Spirit of Yahweh spoke by me, His word was on my tongue.

Mungu wa Israeli alisema, Mwamba wa Israeli aliniambia, Atawalaye wanadamu kwa haki, Akitawala katika kicho cha Mungu, 2 Samweli 23:3

The God of Israel said, The Rock of Israel spoke to me: One who rules over men righteously, Who rules in the fear of God,

Atakuwa kama nuru ya asubuhi jua lichapo, Asubuhi isiyo na mawingu. 2 Samweli 23:4

[He shall be] as the light of the morning, when the sun rises, A morning without clouds, [When] the tender grass [springs] out of the earth, Through clear shining after rain.

Je! Sivyo ilivyo nyumba yangu mbele za Bwana? Kwa kuwa amefanya nami agano la milele; Ina taratibu katika yote, ni thabiti, Maana ni wokovu wangu wote, na shauku langu lote. 2 Samweli 23:5

Most assuredly my house is not so with God; Yet he has made with me an everlasting covenant, Ordered in all things, and sure: For it is all my salvation, and all [my] desire, Although he doesn't make it grow.

Lakini hatawachipuza watu wa ubatili; Watakuwa wote kama miiba ya nyikani ya kutupwa, Ambayo haivuniki kwa mkono, 2 Samweli 23:6

But the ungodly shall be all of them as thorns to be thrust away, Because they can't be taken with the hand

Mtu atakayeigusa hiyo, Na awe na chuma na mpini wa mkuki, Nao watateketezwa papo hapo kwa moto. 2 Samweli 23:7

But the man who touches them Must be armed with iron and the staff of a spear: They shall be utterly burned with fire in [their] place

Haya ndiyo majina ya mashujaa aliokuwa nao Daudi; Yashobeamu Mhakmoni,mkuu wa maakida ;huyo aliliinua shoka lake juu ya watu mia nane waliouawa pamoja. 2 Samweli 23:8

These are the names of the mighty men whom David had: Josheb Basshebeth a Tahchemonite, chief of the captains; the same was Adino the Eznite, against eight hundred slain at one time.

Na baada yake kulikuwa na Eleazari, mwana wa Dodai, Mwahohi, mmojawapo wa wale mashujaa watatu waliokuwa pamoja na Daudi; walipowatukana Wafilisti waliokuwa wamekusanyika huko ili kupigana, na watu wa Israeli walikuwa wamekwenda zao; 2 Samweli 23:9

After him was Eleazar the son of Dodai the son of an Ahohite, one of the three mighty men with David, when they defied the Philistines who were there gathered together to battle, and the men of Israel were gone away.

huyo aliinuka, akawapiga Wafilisti hata mkono wake ukachoka, na mkono wake ukaambatana na upanga; naye Bwana akafanya wokovu mkuu siku ile; nao watu wakarudi nyuma yake ili kuteka nyara tu. 2 Samweli 23:10

He arose, and struck the Philistines until his hand was weary, and his hand froze to the sword; and Yahweh worked a great victory that day; and the people returned after him only to take spoil.

Na baada yake kulikuwa na Shama, mwana wa Agee, Mharari; nao Wafilisti walikuwa wamekusanyika huko Lehi, palipokuwapo konde lililojaa midengu; nao watu wakawakimbia Wafilisti; 2 Samweli 23:11

After him was Shammah the son of Agee a Hararite. The Philistines were gathered together into a troop, where was a plot of ground full of lentils; and the people fled from the Philistines.

ila huyo alisimama katikati ya konde lile, akalipigania, akawaua Wafilisti; naye Bwana akafanya wokovu mkuu. 2 Samweli 23:12

But he stood in the midst of the plot, and defended it, and killed the Philistines; and Yahweh worked a great victory.

Tena, watatu miongoni mwa wale thelathini waliokuwa wakuu wakashuka, wakamwendea Daudi wakati wa mavuno mpaka pango la Adulamu, na kikosi cha Wafilisti walikuwa wamefanya kambi katika bonde la Warefai. 2 Samweli 23:13

Three of the thirty chief men went down, and came to David in the harvest time to the cave of Adullam; and the troop of the Philistines was encamped in the valley of Rephaim.

Naye Daudi wakati ule alikuwako ngomeni, na jeshi la Wafilisti wakati ule walikuwako Bethlehemu. 2 Samweli 23:14

David was then in the stronghold; and the garrison of the Philistines was then in Bethlehem.

Daudi akatamani, akasema, Laiti mtu angeninywesha maji ya kisima cha Bethlehemu, kilicho karibu na lango! 2 Samweli 23:15

David longed, and said, Oh that one would give me water to drink of the well of Bethlehem, which is by the gate!

Basi hao mashujaa watatu wakapenya jeshi la Wafilisti, wakateka maji kutoka kile kisima cha Bethlehemu, kilicho karibu na lango, wakayachukua, wakamletea Daudi; walakini yeye hakukubali kuyanywa, akayamimina mbele za Bwana. 2 Samweli 23:16

The three mighty men broke through the host of the Philistines, and drew water out of the well of Bethlehem, that was by the gate, and took it, and brought it to David: but he would not drink of it, but poured it out to Yahweh.

Akasema, Hasha, Bwana, nisifanye hivi; je! Si damu hii ya watu hao waliohatirisha nafsi zao? Kwa hiyo hakukubali kuyanywa. Hayo ndiyo waliyoyafanya wale mashujaa watatu. 2 Samweli 23:17

He said, Be it far from me, Yahweh, that I should do this: [shall I drink] the blood of the men who went in jeopardy of their lives? therefore he would not drink it. These things did the three mighty men.

Tena, Abishai, nduguye Yoabu, mwana wa Seruya, alikuwa mkuu wa wale watatu. Huyo aliuinua mkuki wake juu ya watu mia tatu, akawaua, akawa na jina kati ya wale watatu. 2 Samweli 23:18

Abishai, the brother of Joab, the son of Zeruiah, was chief of the three. He lifted up his spear against three hundred and killed them, and had a name among the three.

Je! Huyo hakuwa na heshima maalumu miongoni mwa wale watatu? Kwa hiyo akawekwa kuwa akida wao; ila hakudiriki kuwamo katika wale watatu. 2 Samweli 23:19

Wasn't he most honorable of the three? therefore he was made their captain: however he didn't attain to the [first] three.

Tena Benaya, mwana wa Yehoyada, mtu hodari wa Kabseeli aliyekuwa amefanya mambo makuu; aliwaua simba wakali wawili wa Moabu, pia akashuka akamwua simba katikati ya shimo wakati wa theruji. 2 Samweli 23:20

Benaiah the son of Jehoiada, the son of a valiant man of Kabzeel, who had done mighty deeds, he killed the two [sons of] Ariel of Moab: he went down also and killed a lion in the midst of a pit in time of snow.

huyo naye akamwua Mmisri, mtu mrefu; naye huyo Mmisri alikuwa na mkuki mkononi; lakini yeye alimshukia na gongo, akamnyakulia Mmisri mkuki mkononi mwake, akamwua kwa mkuki wake mwenyewe. 2 Samweli 23:21

He killed an Egyptian, a goodly man: and the Egyptian had a spear in his hand; but he went down to him with a staff, and plucked the spear out of the Egyptian's hand, and killed him with his own spear.

Hayo ndiyo aliyoyafanya Benaya, mwana wa Yehoyada, akawa na jina kati ya wale mashujaa watatu. 2 Samweli 23:22

These things did Benaiah the son of Jehoiada, and had a name among the three mighty men.

Alikuwa mwenye heshima kuliko wale thelathini, ila hakudiriki kuwamo katika wale watatu. Naye Daudi akamweka juu ya walinzi wake. 2 Samweli 23:23

He was more honorable than the thirty, but he didn't attain to the [first] three. David set him over his guard.

Asaheli, nduguye Yoabu, alikuwa mmojawapo wa wale thelathini; na Elhanani, mwana wa Dodo, wa Bethlehemu; 2 Samweli 23:24

Asahel the brother of Joab was one of the thirty; Elhanan the son of Dodo of Bethlehem,

na Shama, Mharodi, na Elika, Mharodi; 2 Samweli 23:25

Shammah the Harodite, Elika the Harodite,

na Helesi, Mpeloni, na Ira, mwana wa Ikeshi, Mtekoi; 2 Samweli 23:26

Helez the Paltite, Ira the son of Ikkesh the Tekoite,

na Abiezeri, Mwanathothi, na Sibekai, Mhushathi; 2 Samweli 23:27

Abiezer the Anathothite, Mebunnai the Hushathite,

na Salmoni, Mwahohi, na Maharai, Mnetofathi; 2 Samweli 23:28

Zalmon the Ahohite, Maharai the Netophathite,

na Heledi, mwana wa Baana, Mnetofathi, na Itai, mwana wa Ribai, wa Gibea wa wana wa Benyamini; 2 Samweli 23:29

Heleb the son of Baanah the Netophathite, Ittai the son of Ribai of Gibeah of the children of Benjamin,

na Benaya, Mpirathoni, na Hurai, wa vijito vya Gaashi; 2 Samweli 23:30

Benaiah a Pirathonite, Hiddai of the brooks of Gaash.

na Abieli, Mwarbathi, na Azmawethi, Mbarhumi; 2 Samweli 23:31

Abialbon the Arbathite, Azmaveth the Barhumite,

na Eliaba, Mshaalboni, na wana wa Yasheni; na Yonathani, 2 Samweli 23:32

Eliahba the Shaalbonite, the sons of Jashen, Jonathan,

mwana wa Shama, Mharari, na Ahiamu, mwana wa Shalali, Mharari; 2 Samweli 23:33

Shammah the Hararite, Ahiam the son of Sharar the Ararite,

na Elifeleti, mwana wa Ahasbai, na Heferi, Mmaakathi, na Eliamu, mwana wa Ahithofeli, Mgiloni; 2 Samweli 23:34

Eliphelet the son of Ahasbai, the son of the Maacathite, Eliam the son of Ahithophel the Gilonite,

na Hezro, Mkarmeli, na Paarai, Mwarbi; 2 Samweli 23:35

Hezro the Carmelite, Paarai the Arbite,

na Igali, mwana wa Nathani, wa Soba, na Bani, Mgadi; 2 Samweli 23:36

Igal the son of Nathan of Zobah, Bani the Gadite,

na Seleki, Mwamoni, na Naharai, Mbeerothi, ambao ni wachukua silaha wa Yoabu, mwana wa Seruya; 2 Samweli 23:37

Zelek the Ammonite, Naharai the Beerothite, armor bearers to Joab the son of Zeruiah,

na Ira, Mwithri, na Garebu, Mwithri; 2 Samweli 23:38

Ira the Ithrite, Gareb the Ithrite,

na Uria, Mhiti; jumla yao ilikuwa watu thelathini na saba. 2 Samweli 23:39

Uriah the Hittite: thirty-seven in all.