2 Samweli 21 Swahili & English

Listen/Download Audio
2 Samweli 21 (Swahili) 2nd Samuel 21 (English)

Kulikuwa na njaa siku za Daudi muda wa miaka mitatu, mwaka kwa mwaka; naye Daudi akautafuta uso wa Bwana. Bwana akasema, Ni kwa ajili ya Sauli, na kwa nyumba yake yenye damu, kwa kuwa aliwaua hao Wagibeoni. 2 Samweli 21:1

There was a famine in the days of David three years, year after year; and David sought the face of Yahweh. Yahweh said, It is for Saul, and for his bloody house, because he put to death the Gibeonites.

Ndipo mfalme akawaita Wagibeoni akawaambia; (basi Wagibeoni si wa wana wa Israeli, ila ni wa masalio ya Waamori; na wana wa Israeli walikuwa wamewaapia; lakini Sauli akatafuta kuwaua katika juhudi yake kwa ajili ya wana wa Israeli na Yuda;) 2 Samweli 21:2

The king called the Gibeonites, and said to them (now the Gibeonites were not of the children of Israel, but of the remnant of the Amorites; and the children of Israel had sworn to them: and Saul sought to kill them in his zeal for the children of Israel and Judah);

basi Daudi akawaambia hao Wagibeoni, Niwatendee nini? Na kwa tendo gani nifanye upatanisho, mpate kuubariki urithi wa Bwana? 2 Samweli 21:3

and David said to the Gibeonites, What shall I do for you? And with what shall I make atonement, that you may bless the inheritance of Yahweh?

Na hao Wagibeoni wakamwambia, Si jambo la fedha wala dhahabu lililo kati ya sisi na Sauli, au nyumba yake; wala si juu yetu kumwua mtu ye yote katika Israeli. Akasema Mtakayoyanena, ndiyo nitakayowatendea ninyi. 2 Samweli 21:4

The Gibeonites said to him, It is no matter of silver or gold between us and Saul, or his house; neither is it for us to put any man to death in Israel. He said, What you shall say, that will I do for you.

Wakamwambia mfalme, Yule mtu aliyetupoteza, na kutufanyia shauri la kutuharibu, tusikae katika mipaka yo yote ya Israeli, 2 Samweli 21:5

They said to the king, The man who consumed us, and who devised against us, [that] we should be destroyed from remaining in any of the borders of Israel,

basi, na tutolewe watu saba katika wanawe, nasi tutawatundika mbele za Bwana katika Gibeoni, katika mlima wa Bwana. Mfalme akasema, Nitawatoa. 2 Samweli 21:6

let seven men of his sons be delivered to us, and we will hang them up to Yahweh in Gibeah of Saul, the chosen of Yahweh. The king said, I will give them.

Lakini mfalme akamwachilia Mefiboshethi, mwana wa Yonathani, mwana wa Sauli, kwa ajili ya kiapo cha Bwana kilichokuwa kati yao, yaani, kati ya Daudi na Yonathani, mwana wa Sauli. 2 Samweli 21:7

But the king spared Mephibosheth, the son of Jonathan the son of Saul, because of Yahweh's oath that was between them, between David and Jonathan the son of Saul.

Ila mfalme akawatwaa hao wana wawili wa Rispa, binti Aya, aliomzalia Sauli, Armoni na Mefiboshethi; na wana watano wa Merabu binti Sauli, aliomzalia Adrieli, mwana wa Barzilai, Mmeholathi; 2 Samweli 21:8

But the king took the two sons of Rizpah the daughter of Aiah, whom she bore to Saul, Armoni and Mephibosheth; and the five sons of Michal the daughter of Saul, whom she bore to Adriel the son of Barzillai the Meholathite:

akawatia mikononi mwa Wagibeoni, nao wakawatundika mlimani mbele za Bwana, nao wakaangamia wote saba pamoja; wakauawa siku za mavuno, za kwanza, mwanzo wa mavuno ya shayiri. 2 Samweli 21:9

He delivered them into the hands of the Gibeonites, and they hanged them in the mountain before Yahweh, and they fell [all] seven together. They were put to death in the days of harvest, in the first days, at the beginning of barley harvest.

Naye Rispa, binti Aya, akatwaa nguo ya magunia akajitandikia mwambani, tangu mwanzo wa mavuno hata waliponyeshewa mvua toka mbinguni; wala hakuacha ndege wa angani kukaa juu yao mchana, wala wanyama wa mwitu usiku. 2 Samweli 21:10

Rizpah the daughter of Aiah took sackcloth, and spread it for her on the rock, from the beginning of harvest until water was poured on them from the sky; and she allowed neither the birds of the sky to rest on them by day, nor the animals of the field by night.

Kisha akaambiwa Daudi hayo aliyoyafanya huyo Rispa binti Aya, suria wa Sauli. 2 Samweli 21:11

It was told David what Rizpah the daughter of Aiah, the concubine of Saul, had done.

Akaenda Daudi, akaitwaa mifupa ya Sauli na mifupa ya Yonathani mwanawe mikononi mwa watu wa Yabesh-gileadi; waliyoiiba katika njia ya Bethshani, hapo Wafilisti walipowatungika, katika siku hiyo waliyomwua Sauli huko Gilboa; 2 Samweli 21:12

David went and took the bones of Saul and the bones of Jonathan his son from the men of Jabesh Gilead, who had stolen them from the street of Beth-shan, where the Philistines had hanged them, in the day that the Philistines killed Saul in Gilboa;

naye akaileta toka huko hiyo mifupa ya Sauli, na mifupa ya Yonathani mwanawe; nao wakaizoa mifupa yao waliotundikwa. 2 Samweli 21:13

and he brought up from there the bones of Saul and the bones of Jonathan his son: and they gathered the bones of those who were hanged.

Kisha wakaizika mifupa ya Sauli na ya Yonathani mwanawe katika nchi ya Benyamini, huko Zela, kaburini mwa Kishi babaye; wakafanya yote aliyoyaamuru mfalme. Na baadaye Mungu aliiridhia hiyo nchi. 2 Samweli 21:14

They buried the bones of Saul and Jonathan his son in the country of Benjamin in Zela, in the tomb of Kish his father: and they performed all that the king commanded. After that God was entreated for the land.

Basi kulikuwa na vita tena kati ya Wafilisti na Israeli; Daudi akashuka mpaka Gobu, na watumishi wake pamoja naye, akapigana na Wafilisti; naye Daudi akaishiwa na nguvu. 2 Samweli 21:15

The Philistines had war again with Israel; and David went down, and his servants with him, and fought against the Philistines. David grew faint;

Naye Ishi-benobu, aliyekuwa mmojawapo wa Warefai, ambaye uzito wa mkuki wake ulikuwa shekeli mia tatu za shaba kwa uzani ,naye amejifungia upanga mpya,alijaribu kumwua Daudi. 2 Samweli 21:16

and Ishbibenob, who was of the sons of the giant, the weight of whose spear was three hundred [shekels] of brass in weight, he being girded with a new [sword], thought to have slain David.

Lakini Abishai, mwana wa Seruya, akamsaidia, akampiga Mfilisti, akamwua. Ndipo watu wa Daudi wakamwapia, wakasema, Wewe hutatoka tena pamoja nasi kwenda vitani, usije ukaizima taa ya Israeli. 2 Samweli 21:17

But Abishai the son of Zeruiah helped him, and struck the Philistine, and killed him. Then the men of David swore to him, saying, You shall go no more out with us to battle, that you don't quench the lamp of Israel.

Ikawa baada ya hayo, kulikuwa na vita tena na Wafilisti huko Gobu; ndipo Sibekai, Mhushathi, alipomwua Safu, aliyekuwa mmojawapo wa Warefai. 2 Samweli 21:18

It came to pass after this, that there was again war with the Philistines at Gob: then Sibbecai the Hushathite killed Saph, who was of the sons of the giant.

Kulikuwa na vita tena na Wafilisti huko Gobu; na Elhanani, mwana wa Yairi, Mbethlehemi, alimwua Goliathi, Mgiti, ambaye mti wa mkuki wake ulikuwa kama mti wa mfumaji. 2 Samweli 21:19

There was again war with the Philistines at Gob; and Elhanan the son of Jaareoregim the Bethlehemite killed Goliath the Gittite's brother, the staff of whose spear was like a weaver's beam.

Kulikuwa na vita tena huko Gathi; ambako kulikuwa na mtu mrefu sana, mwenye vidole sita katika kila mkono, na vidole sita katika kila mguu, jumla yake ishirini na vinne; yeye naye alizaliwa kwa Mrefai. 2 Samweli 21:20

There was again war at Gath, where was a man of great stature, who had on every hand six fingers, and on every foot six toes, four and twenty in number; and he also was born to the giant.

Naye huyo alipowatukana Israeli, ndipo Yonathani, mwana wa Shama, nduguye Daudi, akamwua. 2 Samweli 21:21

When he defied Israel, Jonathan the son of Shimei, David's brother, killed him.

Hao wanne walizaliwa kwake huyo Mrefai wa Gathi; wakaanguka kwa mkono wa Daudi, na kwa mikono ya watumishi wake.

2 Samweli 21:22

These four were born to the giant in Gath; and they fell by the hand of David, and by the hand of his servants.