2 Samweli 12 Swahili & English

Listen/Download Audio
2 Samweli 12 (Swahili) 2nd Samuel 12 (English)

Ndipo Bwana akamtuma Nathani aende kwa Daudi. Naye akamwendea, akamwambia, Palikuwa na watu wawili katika mji mmoja; mmoja wao alikuwa tajiri, wa pili maskini. 2 Samweli 12:1

Yahweh sent Nathan to David. He came to him, and said to him, "There were two men in one city; the one rich, and the other poor.

Yule tajiri alikuwa na kondoo na ng'ombe wengi sana; 2 Samweli 12:2

The rich man had very many flocks and herds,

bali yule maskini hakuwa na kitu, ila mwana kondoo mmoja, mdogo, ambaye amemnunua na kumlea; naye akakua pamoja naye, na pamoja na wanawe; hula sehemu ya posho lake, na kukinywea kikombe chake, na kulala kifuani mwake, akawa kwake kama binti. 2 Samweli 12:3

but the poor man had nothing, except one little ewe lamb, which he had bought and raised. It grew up together with him, and with his children. It ate of his own food, drank of his own cup, and lay in his bosom, and was to him like a daughter.

Hata msafiri mmoja akamfikilia yule tajiri, naye akaacha kutwaa mmoja wa kondoo zake mwenyewe au mmoja wa ng'ombe zake mwenyewe, ili kumwandalia yule msafiri aliyemfikilia, bali alimnyang'anya yule maskini mwana-kondoo wake, akamwandalia yule mtu aliyemfikilia. 2 Samweli 12:4

A traveler came to the rich man, and he spared to take of his own flock and of his own herd, to dress for the wayfaring man who had come to him, but took the poor man's lamb, and dressed it for the man who had come to him."

Ndipo hasira ya Daudi ikawaka sana juu ya mtu yule; akamwambia Nathani, Aishivyo Bwana, mtu huyo aliyetenda jambo hili, hakika yake astahili kufa; 2 Samweli 12:5

David's anger was greatly kindled against the man, and he said to Nathan, "As Yahweh lives, the man who has done this is worthy to die!

naye atamrudishia yule mwana-kondoo mara nne, kwa sababu ametenda neno hili, na kwa sababu hakuwa na huruma. 2 Samweli 12:6

He shall restore the lamb fourfold, because he did this thing, and because he had no pity!"

Basi Nathani akamwambia Daudi, Wewe ndiwe mtu huyo. Bwana, Mungu wa Israeli, asema hivi, Nalikutia mafuta, uwe mfalme juu ya Israeli, nikakuokoa na mkono wa Sauli; 2 Samweli 12:7

Nathan said to David, "You are the man. This is what Yahweh, the God of Israel, says: 'I anointed you king over Israel, and I delivered you out of the hand of Saul.

nami nikakupa nyumba ya bwana wako, na wake za bwana wako kifuani mwako; nikakupa nyumba ya Israeli na ya Yuda; na kama hayo yangalikuwa machache, ningalikuongezea mambo kadha wa kadha. 2 Samweli 12:8

I gave you your master's house, and your master's wives into your bosom, and gave you the house of Israel and of Judah; and if that would have been too little, I would have added to you many more such things.

Kwa nini umelidharau neno la Bwana, na kufanya yaliyo mabaya machoni pake? Umempiga Uria, Mhiti, kwa upanga, nawe umemtwaa mkewe awe mke wako, nawe umemwua huyo kwa upanga wa wana wa Amoni. 2 Samweli 12:9

Why have you despised the word of Yahweh, to do that which is evil in his sight? You have struck Uriah the Hittite with the sword, and have taken his wife to be your wife, and have slain him with the sword of the children of Ammon.

Basi, sasa upanga hautaondoka nyumbani mwako, kwa sababu umenidharau, ukamtwaa mkewe Uria, Mhiti, kuwa mke wako. 2 Samweli 12:10

Now therefore the sword will never depart from your house, because you have despised me, and have taken the wife of Uriah the Hittite to be your wife.'

Bwana asema hivi, Angalia, nitakuondokeshea uovu katika nyumba yako, nami nitawatwaa wake zako mbele ya macho yako, na kumpa jirani yako, naye atalala na wake zako mbele ya jua hili. 2 Samweli 12:11

This is what Yahweh says: 'Behold, I will raise up evil against you out of your own house; and I will take your wives before your eyes, and give them to your neighbor, and he will lie with your wives in the sight of this sun.

Maana wewe ulifanya jambo lile kwa siri; bali mimi nitalifanya jambo hili mbele ya Israeli wote na mbele ya jua. 2 Samweli 12:12

For you did it secretly, but I will do this thing before all Israel, and before the sun.'"

Daudi akamwambia Nathani, Nimemfanyia Bwana dhambi. Nathani akamwambia Daudi, Bwana naye ameiondoa dhambi yako; hutakufa. 2 Samweli 12:13

David said to Nathan, "I have sinned against Yahweh." Nathan said to David, "Yahweh also has put away your sin. You will not die.

Lakini, kwa kuwa kwa tendo hili umewapa adui za Bwana nafasi kubwa ya kukufuru, mtoto atakayezaliwa kwako hakika yake atakufa. 2 Samweli 12:14

However, because by this deed you have given great occasion to Yahweh's enemies to blaspheme, the child also who is born to you shall surely die."

Naye Nathani akaondoka kwenda nyumbani kwake. Basi Bwana akampiga yule mtoto ambaye mkewe Uria alimzalia Daudi naye akawa hawezi sana. 2 Samweli 12:15

Nathan departed to his house. Yahweh struck the child that Uriah's wife bore to David, and it was very sick.

Basi Daudi akamwomba Mungu kwa ajili ya mtoto; Daudi akafunga, akaingia, akalala usiku kucha chini. 2 Samweli 12:16

David therefore begged God for the child; and David fasted, and went in, and lay all night on the earth.

Nao wazee wa nyumba yake wakaondoka, wakasimama karibu naye, ili wamwinue katika nchi; lakini hakukubali, wala hakula chakula pamoja nao. 2 Samweli 12:17

The elders of his house arose, [and stood] beside him, to raise him up from the earth: but he would not, neither did he eat bread with them.

Ikawa siku ya saba, yule mtoto akafa. Nao watumishi wa Daudi wakaogopa kumwambia ya kuwa mtoto amekufa, maana, walisema, Angalieni, yule mtoto alipokuwa angali hai, tulisema naye, asitusikilize sauti zetu; basi hatazidi kujisumbua, tukimwambia ya kuwa mtoto amekufa? 2 Samweli 12:18

It happened on the seventh day, that the child died. The servants of David feared to tell him that the child was dead; for they said, Behold, while the child was yet alive, we spoke to him, and he didn't listen to our voice: how will he then vex himself, if we tell him that the child is dead!

Lakini alipoona ya kuwa watumishi wake wananong'onezana, Daudi alitambua ya kuwa mtoto amekufa; basi Daudi akawauliza watumishi wake, Je! Mtoto amekufa? Nao wakasema, Amekufa. 2 Samweli 12:19

But when David saw that his servants were whispering together, David perceived that the child was dead; and David said to his servants, Is the child dead? They said, He is dead.

Ndipo Daudi akainuka pale chini akaoga, akajipaka mafuta, akabadili mavazi yake; akaingia nyumbani mwa Bwana, akasali; kisha akaenda nyumbani kwake, na alipotaka wakamwandalia chakula, naye akala. 2 Samweli 12:20

Then David arose from the earth, and washed, and anointed himself, and changed his clothing; and he came into the house of Yahweh, and worshiped: then he came to his own house; and when he required, they set bread before him, and he ate.

Watumishi wake wakamwambia, Ni neno gani hili ulilolitenda? Ulifunga na kulia kwa ajili ya mtoto, alipokuwa hai; lakini mtoto alipokuwa amekufa, uliinuka ukala chakula. 2 Samweli 12:21

Then said his servants to him, What thing is this that you have done? you did fast and weep for the child, while it was alive; but when the child was dead, you did rise and eat bread.

Akasema, Mtoto alipokuwa hai, nalifunga, nikalia; kwa maana nalisema, Ni nani ajuaye kwamba Bwana atanihurumia, mtoto apate kuishi? 2 Samweli 12:22

He said, While the child was yet alive, I fasted and wept: for I said, Who knows whether Yahweh will not be gracious to me, that the child may live?

Lakini sasa amekufa nifungie nini? Je! Naweza kumrudisha tena? Mimi nitakwenda kwake lakini yeye hatanirudia mimi. 2 Samweli 12:23

But now he is dead, why should I fast? can I bring him back again? I shall go to him, but he will not return to me.

Naye Daudi akamfariji Bath-sheba mkewe, akaingia kwake, akalala naye; naye akazaa mwana, akamwita jina lake Sulemani. Naye Bwana akampenda; 2 Samweli 12:24

David comforted Bathsheba his wife, and went in to her, and lay with her: and she bore a son, and he called his name Solomon. Yahweh loved him;

akapeleka kwa mkono wa Nathani, nabii, naye akamwita jina lake Yedidia, kwa ajili ya Bwana. 2 Samweli 12:25

and he sent by the hand of Nathan the prophet; and he named him Jedidiah, for Yahweh's sake.

Yoabu akapigana juu ya Raba wa wana wa Amoni, akautwaa mji wa kifalme. 2 Samweli 12:26

Now Joab fought against Rabbah of the children of Ammon, and took the royal city.

Yoabu akatuma wajumbe waende kwa Daudi, kusema Nimeshindana na Raba, hata nimeutwaa huo mji wa maji. 2 Samweli 12:27

Joab sent messengers to David, and said, I have fought against Rabbah; yes, I have taken the city of waters.

Basi sasa kusanya watu waliobaki, ukauzunguke mji, na kuutwaa; nisije mimi nikautwaa mji, ukaitwe jina langu. 2 Samweli 12:28

Now therefore gather the rest of the people together, and encamp against the city, and take it; lest I take the city, and it be called after my name.

Basi Daudi akawakusanya watu wote akaenda Raba, akapigana nao, akautwaa. 2 Samweli 12:29

David gathered all the people together, and went to Rabbah, and fought against it, and took it.

Kisha akamnyang'anya mfalme wao taji toka kichwani pake; na uzani wake ulikuwa talanta ya dhahabu, nayo ilikuwa na vito vya thamani ndani yake; akavikwa Daudi kichwani. Akazitoa nyara za huo mji, nyingi sana. 2 Samweli 12:30

He took the crown of their king from off his head; and the weight of it was a talent of gold, and [in it were] precious stones; and it was set on David's head. He brought forth the spoil of the city, exceeding much.

Naye akawatoa watu waliokuwamo, akawaweka kwenye kazi ya misumeno,na sululu za chuma,na mashoka ya chuma,akawatumikisha,tanuuni mwa matofali ndivyo alivyoifanya miji yote ya wana wa Amoni.Kisha Daudi akarudi na watu wote Yerusalemu. 2 Samweli 12:31

He brought forth the people who were therein, and put them under saws, and under harrows of iron, and under axes of iron, and made them pass through the brick kiln: and thus did he to all the cities of the children of Ammon. David and all the people returned to Jerusalem.