2 Samweli 6 Swahili & English

Listen/Download Audio
2 Samweli 6 (Swahili) 2nd Samuel 6 (English)

Basi Daudi akakusanya tena wateule wote wa Israeli, watu thelathini elfu. 2 Samweli 6:1

David again gathered together all the chosen men of Israel, thirty thousand.

Akaondoka Daudi akaenda pamoja na watu wote waliokuwa naye, mpaka Baala wa Yuda, ili kulipandisha kutoka huko sanduku la Mungu lililoitwa kwa jina, naam, jina la Bwana wa majeshi akaaye juu ya makerubi. 2 Samweli 6:2

David arose, and went with all the people who were with him, from Baale Judah, to bring up from there the ark of God, which is called by the Name, even the name of Yahweh of Hosts who sits [above] the cherubim.

Wakaliweka sanduku la Mungu juu ya gari jipya, wakalitoa katika nyumba ya Abinadabu, iliyoko kilimani; nao Uza na Ahio wana wa Abinadabu wakaliendesha lile gari jipya. 2 Samweli 6:3

They set the ark of God on a new cart, and brought it out of the house of Abinadab that was in the hill: and Uzzah and Ahio, the sons of Abinadab, drove the new cart.

Wakalitoa katika nyumba ya Abinadabu iliyoko kilimani, pamoja na sanduku la Bwana; na huyo Ahio akatangulia mbele ya sanduku. 2 Samweli 6:4

They brought it out of the house of Abinadab, which was in the hill, with the ark of God: and Ahio went before the ark.

Daudi na nyumba yote ya Israeli wakacheza mbele za Bwana kwa nguvu zao zote, kwa nyimbo, na kwa vinubi, na kwa vinanda, na kwa matari, na kwa kayamba, na kwa matoazi. 2 Samweli 6:5

David and all the house of Israel played before Yahweh with all manner of [instruments made of] fir-wood, and with harps, and with psalteries, and with tambourines, and with castanets, and with cymbals.

Hata walipofika kwa uga ya Nakoni, Uza akalinyoshea mkono sanduku la Mungu, akalikamata kwa maana wale ng'ombe walikunguwaa. 2 Samweli 6:6

When they came to the threshing floor of Nacon, Uzzah put forth [his hand] to the ark of God, and took hold of it; for the oxen stumbled.

Ndipo hasira ya Bwana ikawaka juu ya Uza; naye Mungu akampiga huko kwa kosa lake; hata akafa pale pale penye sanduku la Mungu. 2 Samweli 6:7

The anger of Yahweh was kindled against Uzzah; and God struck him there for his error; and there he died by the ark of God.

Daudi akaona uchungu kwa kuwa Bwana amemfurikia Uza; akapaita mahali pale Peres-uza hata leo. 2 Samweli 6:8

David was displeased, because Yahweh had broken forth on Uzzah; and he called that place Perez Uzzah, to this day.

Naye Daudi akamwogopa Bwana siku ile; akasema, Litanijiaje sanduku la Bwana? 2 Samweli 6:9

David was afraid of Yahweh that day; and he said, How shall the ark of Yahweh come to me?

Basi Daudi hakutaka kulileta sanduku la Bwana kwake mjini mwa Daudi; ila Daudi akalihamisha nyumbani kwa Obed-edomu, Mgiti. 2 Samweli 6:10

So David would not remove the ark of Yahweh to him into the city of David; but David carried it aside into the house of Obed-edom the Gittite.

Sanduku la Bwana akalitia katika nyumba ya Obed-edomu, Mgiti, muda wa miezi mitatu; naye Bwana akambarikia Obed-edomu, na nyumba yake yote. 2 Samweli 6:11

The ark of Yahweh remained in the house of Obed-edom the Gittite three months: and Yahweh blessed Obed-edom, and all his house.

Kisha mfalme Daudi akaambiwa ya kwamba, Bwana ameibarikia nyumba ya Obed-edomu, na vitu vyote alivyo navyo kwa ajili ya sanduku la Mungu. Daudi akaenda, akalileta sanduku la Mungu, toka nyumba ya Obed-edomu mpaka mji wa Daudi, kwa shangwe. 2 Samweli 6:12

It was told king David, saying, Yahweh has blessed the house of Obed-edom, and all that pertains to him, because of the ark of God. David went and brought up the ark of God from the house of Obed-edom into the city of David with joy.

Hata ikawa, watu waliolichukua sanduku la Bwana walipokwisha kwenda hatua sita, akachinja ng'ombe na kinono. 2 Samweli 6:13

It was so, that, when those who bore the ark of Yahweh had gone six paces, he sacrificed an ox and a fattened calf.

Daudi akacheza mbele za Bwana kwa nguvu zake zote; na Daudi alikuwa amevaa naivera ya kitani. 2 Samweli 6:14

David danced before Yahweh with all his might; and David was girded with a linen ephod.

Basi Daudi na nyumba yote ya Israeli wakalileta sanduku la Bwana kwa shangwe, na kwa sauti ya tarumbeta. 2 Samweli 6:15

So David and all the house of Israel brought up the ark of Yahweh with shouting, and with the sound of the trumpet.

Ikawa, sanduku la Bwana lilipoingia mji wa Daudi Mikali, binti Sauli, akachungulia dirishani, akamwona mfalme Daudi akiruka-ruka na kucheza mbele za Bwana; akamdharau moyoni mwake. 2 Samweli 6:16

It was so, as the ark of Yahweh came into the city of David, that Michal the daughter of Saul looked out at the window, and saw king David leaping and dancing before Yahweh; and she despised him in her heart.

Wakaliingiza sanduku la Bwana, na kuliweka mahali pake, katikati ya hema aliyoipiga Daudi kwa ajili yake, naye Daudi akatoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani mbele za Bwana. 2 Samweli 6:17

They brought in the ark of Yahweh, and set it in its place, in the midst of the tent that David had pitched for it; and David offered burnt offerings and peace-offerings before Yahweh.

Kisha Daudi alipokwisha kutoa sadaka ya kuteketezwa na sadaka za amani akawabarikia watu kwa jina la Bwana wa majeshi. 2 Samweli 6:18

When David had made an end of offering the burnt offering and the peace-offerings, he blessed the people in the name of Yahweh of Hosts.

Akawagawia watu wote, mkutano wote wa Israeli, wanaume kwa wanawake, kila mtu mkate wa ngano, na kipande cha nyama, na mkate wa zabibu. Basi watu wote wakaenda zao, kila mtu nyumbani kwake. 2 Samweli 6:19

He dealt among all the people, even among the whole multitude of Israel, both to men and women, to everyone a cake of bread, and a portion [of flesh], and a cake of raisins. So all the people departed everyone to his house.

Ndipo Daudi akarudi ili awabarikie watu wa nyumbani mwake. Na Mikali, binti Sauli, akatoka nje aende kumlaki Daudi, naye akasema, Mfalme wa Israeli alikuwa mtukufu leo namna gani, akijifunua mwili wake mbele ya vijakazi vya watumishi wake, mfano wa watu baradhuli mmojawapo, ajifunuavyo mwili wake mbele ya watu, asipokuwa na haya! 2 Samweli 6:20

Then David returned to bless his household. Michal the daughter of Saul came out to meet David, and said, How glorious was the king of Israel today, who uncovered himself today in the eyes of the handmaids of his servants, as one of the vain fellows shamelessly uncovers himself!

Daudi akamwambia Mikali, Ilikuwa mbele za Bwana, aliyenichagua mimi juu ya baba yako, na juu ya nyumba yake, ili kuniweka niwe mkuu juu ya watu wa Bwana, juu ya Israeli; kwa hiyo mimi nitacheza mbele za Bwana. 2 Samweli 6:21

David said to Michal, [It was] before Yahweh, who chose me above your father, and above all his house, to appoint me prince over the people of Yahweh, over Israel: therefore will I play before Yahweh.

Kisha nitakuwa hafifu zaidi, nami nitakuwa mnyonge machoni pangu mimi mwenyewe; lakini kwa wale vijakazi uliowanena, kwao nitaheshimiwa. 2 Samweli 6:22

I will be yet more vile than this, and will be base in my own sight: but of the handmaids of whom you have spoken, they shall honor me.

Basi Mikali, binti Sauli, hakuwa na mtoto hata siku ya kufa kwake. 2 Samweli 6:23

Michal the daughter of Saul had no child to the day of her death.