Sifa Lyrics

Usinipite by Walter Chilambo cover art

Walter Chilambo - Usinipite Lyrics

Artist:
Walter Chilambo
Album:
Thank You Lord
Official Release:
30 Jan 2021

Lyrics

Ee Bwana nainamisha kichwa changu
Ninakuabudu we
Na tena nainua mikono yangu
Kukuadhimisha we


Na ninashuka kwa unyenyekevu
Madhahabuni pako
Maana majibu ya maswali yangu
Baba nitapata kwako


Kwanza nahitaji rehema zako
Nisafishe Bwana
Kwa yale nayajua na nisoyajua
Niwe safi Bwana ninaomba nehema yako
Na kibali chako juu yangu wee
Nitembee kifua mbele 


Yesu unapozuru wengine usinipite
Nikumbuke, usinipite
Maombi yangu, usinipite 
Baba uyakumbuke, usinipite


Nyakati za majaribu, usinipite
Uniguze, usinipite
Ingawa mi si mkamilifu, usinipite
Ah ah, usinipite


Natamani nikuone
Yesu niguse vazi lako
Natamani niwe Batimayo
Unifumbue macho


Unifundishe maana we mwalimu wa imani
Nitapita salama
Maana akili zangu zimefika mwisho
Tumaini lipo kwako bwana


Na unijaze roho wako mtakatifu
Ashike fahamu zangu
Nihisi niki kulingana nawe Bwana


Maana wajua ninayoyapitia 
Nahitaji huruma yako
Ee Mungu kadiri ya fadhili zako
Usinipite


Ninaomba neema yako
Zaidi nisimame nitangaze
Uzuri wako bwana


Yesu unapozuru wengine usinipite
Nikumbuke, usinipite
Maombi yangu, usinipite 
Baba uyakumbuke, usinipite


Nyakati za majaribu, usinipite
Uniguze, usinipite
Ingawa mi si mkamilifu, usinipite
Ah ah, usinipite


Maana hakuna nguvu ipitayo jina lako, usinipite
Ni we unaweza, usinipite
Navunja maagano yote
Nikumbuke, usinipite


Adui ni mkali, usinipite
We Yesu nakuomba, usinipite
Ninapokosa tumaini, usinipite
Unikumbuke, usinipite


Video