Sifa Lyrics

Nitakase by Walter Chilambo cover art

Walter Chilambo - Nitakase Lyrics

Artist:
Walter Chilambo
Album:
Ushuhuda
Official Release:
16 May 2022

Lyrics

Kuna wakati tunapitia mambo magumu
Nakujiona kwamba tunayaweza wenyewe
Kuna wakati yakitulemea twalaumu
Nakukufuru Mungu kumbe ni sisi wenyewe


Kuna wakati akili na mawazo yetu
Tunakusahau wewe tunavipa kipaumbele
Sikwamba huoni haya tunayofanya si sawa
Unatutazama kwa huruma


Vipi nikushukuru kwa nämna gani nikufae
Nami ukanifanye nuru ya ulimwengu na ikang'ae
Kwa maana umesema heri mtu yule
Asiyekwenda katika shauri la wasio haki
Bali sheria yako bwana


Unitengeneze niumbie moyo safi
Unitakase nikupendeze wewe
Unitengeneze uniumbie moyo safi
Unitakase nikupendeze wewe
Bali sheria yako bwana


Najua me nikiumbe dhaifu tu basi
Basi angalau na mimi nikupendeze wewe
Nilingane na wewe hata kwa machache tu
Niwakumbushe na wengine ili wajue upo
Maana kumeharibika


Tunaangamia kwa kukosa maarifa
Hakuna upendo ule umetufundisha
Wanadamu tumebadilika tumekuwa wabaya
Tumesahau kwamba upo
Tumesahau wewe upo
Yani kama hatuoni vile


Vipi nikushukuru kwa nämna gani nikufae
Nami ukanifanye nuru ya ulimwengu na ikang'ae
Kwa maana umesema heri mtu yule
Asiyekwenda katika shauri la wasio haki
Bali sheria yako bwana


Unitengeneze uniumbie moyo safi
Unitakase nikupendeze wewe
Bali sheria yako bwana
Unitengeneze uniumbie moyo safi
Unitakase nikupendeze wewe
Bali sheria yako bwana


Vipi nikushukuru kwa nämna gani nikufae
Nami ukanifanye nuru ya ulimwengu na ikang'ae
Kwa maana umesema heri mtu yule
Asiyekwenda katika shaur la wasio haki
Bali sheria yako bwana ikang'ae


Video