Walter Chilambo - Inatosha Lyrics
Lyrics
Kwangu ni sawa Ata niwe kiziwi nisisikie lolote Ila sauti yako tu Kwangu ni sawa Ata niwe na upofu nisione lolote Nikuone wewe tu Wala sitojali lolote Sitoshika chochote Kiu ya moyo wangu Nishike neno lako tu Ata nitengwe na dunia nzima Wanifanye vibaya Nikiwa nawe inatosha Ata iweje, Nitalisifu jina lako Maana unajua vile unanisemesha
Sauti yako ikiongea nami Inatosha, Inatosha Uwepo wako roho ndani yangu Inatosha, Inatosha Ulinzi wako ukinizunguka Inatosha, Inatosha Upendo wako unavyonipenda mimi Inatosha, Inatosha
Pekee yako, Pekee yako Pekee yako wewe Pekee yako unatosha Pekee yako, Pekee yako Pekee yako wewe Pekee yako unatosha
Bwana Mungu ukamuita Adamu Uko wapi mwanangu Mbona sikupati, Nakutafuta Adamu naye akajibu Niko huku nimejificha Kwani niko uchi Nimeogopa sauti yako Nani amekuambia ya kwamba uko uchi Kumbe Adamu kafungua sikio lake kwa adui Nataka kusikia sauti yako tu Sauti ya ukamilifu Ambayo hapo mwanzo Ilinifanya niwe kamili Nataka kusikia sauti yako tu Ambayo moyo wangu utajaa utoshelevu
Sauti yako ikiongea nami Inatosha, Inatosha Uwepo wako, Roho ndani yangu Inatosha, Inatosha Ulinzi wako ukinizunguka Inatosha, Inatosha Upendo wako Unavyonipenda mimi (Upendo wako kwangu) Unanipenda upeo Inatosha, Inatosha
Bwana Pekee yako, Pekee yako Unatosha Pekee yako wewe Pekee yako Bwana, Unatosha Pekee yako, Pekee yako Pekee yako unatosha Pekee yako Pekee yako unatoshaa
Video
Walter Chilambo Feat. Ambwene Mwasongwe - Inatosha (Official Music Video)