Sifa Lyrics

Nipe Neema by Msanii Music Group cover art

Msanii Music Group - Nipe Neema Lyrics

Artist:
Msanii Music Group
Album:
Nipe Neema - Single
Official Release:
21 Mar 2026

Lyrics

The following are the lyrics for "Nipe Neema" by Msanii Music Group:


(Verse 1)
Wapo waliotembea kwa neema yako
Uliwafanya wakubalike kwa wengi
Na waliposimama katikati ya watu
Nyuso zao zikang’aa kwa kibali
Walizungukwa na wivu wa wengi
Lakini mipango yao haikusimama
Na ukanyanyua vichwa vyao juu
Kwa sababu mkono wako ulikuwa nao


(Chorus)
Nipe neema yako Bwana
Nikubalike machoni pa watu
Milango ifunguke mbele yangu
Pasipo nguvu zangu
Nipe neema yako Bwana
Fursa zinifuate kila mahali
Wakiinuka kunizuia, nisimame kwa ushindi


(Verse 2)
Wapo walioketi chini kwa muda
Baadaye wakati wao ukafika
Uliwatoa mahali pa chini
Na kuwaweka mbele ya wakuu
Walipopingwa na maneno ya watu
Na njama zikapangwa gizani
Lakini neema yako ikasema
Hakuna atakayewazuia


(Chorus)
Nipe neema yako Bwana
Nikubalike machoni pa watu
Milango ifunguke mbele yangu
Pasipo nguvu zangu
Nipe neema yako Bwana
Fursa zinifuate kila mahali
Wakiinuka kunizuia, nisimame kwa ushindi


(Bridge)
Neema yako initangulie Bwana
Kila mahali nimepanga kutafuta
Neema yako izungumze kwa ajili yangu
Hata kabla sijafika eh
Na Bwana kama kuna yule anayepanga kunizuia eh
Aone mkono wako juu yangu
Na yeyote anayehusika kufungua milango eh
Aone kibali chako kimevaka juu yangu oh


(Chorus)
Nipe neema yako Bwana
Nikubalike machoni pa watu
Milango ifunguke mbele yangu
Pasipo nguvu zangu
Nipe neema yako Bwana
Fursa zinifuate kila mahali
Wakiinuka kunizuia, nisimame kwa ushindi


Video