Sifa Lyrics

Utachipuka Tena by Annastacia Mukabwa cover art

Annastacia Mukabwa - Utachipuka Tena Lyrics

Artist:
Annastacia Mukabwa
Album:
Utachipuka Tena - Single
Official Release:
01 Feb 2021

Lyrics

Yaapo matumaini makubwa
Kwa muuti, uliokatwa
Yaapo matumaini makubwa
Kwa muuti, uliokatwa


Kwa harufu ya maji, utachipuka tena
Kwa harufu ya maji, utachipuka tena
Kwa harufu ya maji, utachipuka tena
Kwa harufu ya maji, utachipuka tena


Watu wengi wanaiona leo yangu
Lakini kesho yangu wengi hawaijui
Watu wengi wanaiona leo yangu
Lakini kesho yangu wengi hawaijui


Watu wengi wanaiona leo yako
Lakini kesho yako hawaijui
Watu wengi wanaiona leo yako ndugu
Lakini kesho yako hawaijui


Ujapo katwa utasimama tena
Ujapo katwa utachipuka tena weeh
Ujapo katwa utastawi tena
Ujapo katwa utainuka tena weeh


We ndugu yangu, utachipuka tena
Usikate tamaa Mungu yupo, utachipuka tena
Usiwaze kurudi nyuma, utachipuka tena
Usichoshwe na maneno ya wanadamu, utachipuka tena


Utachipuka tena, utachipuka tena
Kwa harufu ya maji, utachipuka tena
Utachipuka tena, utachipuka tena
Japo anguka utachipuka, utachipuka tena


Halleluyah, Halleluyah
Aaah


Kila jambo analolitenda Mungu maishani mwako
Tambua lina kusudi
Jaribu unalopitia leo sikwamba hakuoni 
Jua lipo kusudi


Yusufu aliuzwa na nduguze
Utumwani kule Misri
Alidharauliwa na kutukwanwa
Kunenewa vibaya na kusingiziwa


Mawazo yao walidhani wamemmaliza
Wamempoteza eeeg
Kumbe ndiye waziri 
Aliyeandaliwa na Mungu


Mapito yako ya leo
Ni ushuhuda wa kesho, usikate tamaa
Kukosa kwako kwa leo
Ni kupata kwako kwa kesho, usikate tamaa


Ooh kwa jina la Yesu wee, utachipuka tena
Oooh kwa neno la Mungu, utachipuka tena
Adui zako watakuona juu juu, utachipuka tena
Mungu wetu yeye atakuinua, utachipuka tena


Heshima yako unarejeshewa wewe, utachipuka tena
Afya yako unarejeshewa upya, utachipuka tena
Magonjwa kwako yatakoma kabisa, utachipuka tena
Milango yako inafunguliwa tena, utachipuka tena


Eeh mama weee, eeh baba wee...


Video