2 Wakorintho 11 Swahili & English

Listen/Download Audio
2 Wakorintho 11 (Swahili) 2nd Corinthians 11 (English)

Laiti mngechukuliana nami katika upumbavu wangu kidogo! Naam, mchukuliane nami. 2 Wakorintho 11:1

I wish that you would bear with me in a little foolishness, but indeed you do bear with me.

Maana nawaonea wivu, wivu wa Mungu; kwa kuwa naliwaposea mume mmoja, ili nimletee Kristo bikira safi. 2 Wakorintho 11:2

For I am jealous over you with a godly jealousy. For I married you to one husband, that I might present you as a pure virgin to Christ.

Lakini nachelea; kama yule nyoka alivyomdanganya Hawa kwa hila yake, asije akawaharibu fikira zenu, mkauacha unyofu na usafi kwa Kristo. 2 Wakorintho 11:3

But I am afraid that somehow, as the serpent deceived Eve in his craftiness, so your minds might be corrupted from the simplicity that is in Christ.

Maana yeye ajaye akihubiri Yesu mwingine ambaye sisi hatukumhubiri, au mkipokea roho nyingine msiyoipokea, au injili nyingine msiyoikubali, mnatenda vema kuvumiliana naye! 2 Wakorintho 11:4

For if he who comes preaches another Jesus, whom we did not preach, or if you receive a different spirit, which you did not receive, or a different gospel, which you did not accept, you put up with that well enough.

Maana nadhani ya kuwa mimi sikupungukiwa na kitu walicho nacho mitume walio wakuu. 2 Wakorintho 11:5

For I reckon that I am not at all behind the very best apostles.

Lakini nijapokuwa mimi ni mtu asiyejua kunena, hii si hali yangu katika elimu; ila katika kila neno tumedhihirishwa kwenu. 2 Wakorintho 11:6

But though I am unskilled in speech, yet I am not unskilled in knowledge. No, in every way we have been revealed to you in all things.

Je! Nalifanya dhambi kwa kunyenyekea ili ninyi mtukuzwe, kwa sababu naliwahubiri Injili ya Mungu bila ujira? 2 Wakorintho 11:7

Or did I commit a sin in humbling myself that you might be exalted, because I preached to you God's Gospel free of charge?

Naliwanyang'anya makanisa mengine mali yao, nikitwaa posho langu ili niwahudumie ninyi. 2 Wakorintho 11:8

I robbed other assemblies, taking wages from them that I might serve you.

Nami nilipokuwa pamoja nanyi na kuhitaji sikumlemea mtu. Maana hao ndugu waliokuja kutoka Makedonia walinipa kadiri ya mahitaji yangu; nami katika mambo yote najilinda nafsi yangu nisiwalemee hata kidogo; tena najilinda. 2 Wakorintho 11:9

When I was present with you and was in need, I wasn't a burden on anyone, for the brothers, when they came from Macedonia, supplied the measure of my need. In everything I kept myself from being burdensome to you, and I will continue to do so.

Kama vile ile kweli ya Kristo ilivyo ndani yangu, hakuna mtu atakayenifumba kinywa katika kujisifu huku, katika mipaka ya Akaya. 2 Wakorintho 11:10

As the truth of Christ is in me, no one will stop me from this boasting in the regions of Achaia.

Kwa nini? Je! Ni kwa sababu siwapendi ninyi? Mungu anajua. 2 Wakorintho 11:11

Why? Because I don't love you? God knows.

Lakini nifanyalo nitalifanya, ili niwapinge hao watafutao nafasi wasipate nafasi; ili kwamba katika neno hilo wajisifialo waonekane kuwa kama sisi. 2 Wakorintho 11:12

But what I do, that I will do, that I may cut off occasion from them that desire an occasion, that in which they boast, they may be found even as we.

Maana watu kama hao ni mitume wa uongo, watendao kazi kwa hila, wanaojigeuza wawe mfano wa mitume wa Kristo. 2 Wakorintho 11:13

For such men are false apostles, deceitful workers, masquerading as Christ's apostles.

Wala si ajabu. Maana Shetani mwenyewe hujigeuza awe mfano wa malaika wa nuru. 2 Wakorintho 11:14

And no wonder, for even Satan masquerades as an angel of light.

Basi si neno kubwa watumishi wake nao wakijigeuza wawe mfano wa watumishi wa haki, ambao mwisho wao utakuwa sawasawa na kazi zao. 2 Wakorintho 11:15

It is no great thing therefore if his ministers also masquerade as servants of righteousness, whose end will be according to their works.

Nasema tena, mtu asidhani ya kuwa mimi ni mpumbavu; lakini mjaponidhania hivi, mnikubali kama mpumbavu; ili mimi nami nipate kujisifu ngaa kidogo. 2 Wakorintho 11:16

I say again, let no one think me foolish. But if so, yet receive me as foolish, that I also may boast a little.

Ninenalo silineni agizo la Bwana, bali kama kwa upumbavu, katika ujasiri huu wa kujisifu. 2 Wakorintho 11:17

That which I speak, I don't speak according to the Lord, but as in foolishness, in this confidence of boasting.

Kwa sababu wengi wanajisifu kwa jinsi ya mwili, mimi nami nitajisifu. 2 Wakorintho 11:18

Seeing that many boast after the flesh, I will also boast.

Ninyi, kwa kuwa mna akili, mnachukuliana na wajinga kwa furaha. 2 Wakorintho 11:19

For you bear with the foolish gladly, being wise.

Maana mwachukuliana na mtu akiwatia utumwani, akiwameza, akiwateka nyara, akijikuza, akiwapiga usoni. 2 Wakorintho 11:20

For you bear with a man, if he brings you into bondage, if he devours you, if he takes you captive, if he exalts himself, if he strikes you on the face.

Nanena kwa jinsi ya kujidhili kana kwamba sisi tulikuwa dhaifu. Walakini, akiwa mtu anao ujasiri kwa lo lote, (nanena kipuuzi), mimi nami ninao ujasiri. 2 Wakorintho 11:21

I speak by way of disparagement, as though we had been weak. Yet however any is bold (I speak in foolishness), I am bold also.

Wao ni Waebrania? Na mimi pia. Wao ni Waisraeli? Na mimi pia. Wao ni uzao wa Ibrahimu? Na mimi pia. 2 Wakorintho 11:22

Are they Hebrews? So am I. Are they Israelites? So am I. Are they the seed of Abraham? So am I.

Wao ni wahudumu wa Kristo? (Nanena kiwazimu), mimi ni zaidi; katika taabu kuzidi sana; katika vifungo kuzidi sana; katika mapigo kupita kiasi; katika mauti mara nyingi. 2 Wakorintho 11:23

Are they servants of Christ? (I speak as one beside himself) I am more so; in labors more abundantly, in prisons more abundantly, in stripes above measure, in deaths often.

Kwa Wayahudi mara tano nalipata mapigo arobaini kasoro moja. 2 Wakorintho 11:24

Five times from the Jews I received forty stripes minus one.

Mara tatu nalipigwa kwa bakora; mara moja nalipigwa kwa mawe; mara tatu nalivunjikiwa jahazi; kuchwa kucha nimepata kukaa kilindini; 2 Wakorintho 11:25

Three times I was beaten with rods. Once I was stoned. Three times I suffered shipwreck. I have been a night and a day in the deep.

katika kusafiri mara nyingi; hatari za mito; hatari za wanyang'anyi; hatari kwa taifa langu; hatari kwa mataifa mengine; hatari za mjini; hatari za jangwani; hatari za baharini; hatari kwa ndugu za uongo; 2 Wakorintho 11:26

I have been in travels often, perils of rivers, perils of robbers, perils from my countrymen, perils from the Gentiles, perils in the city, perils in the wilderness, perils in the sea, perils among false brothers;

katika taabu na masumbufu; katika kukesha mara nyingi; katika njaa na kiu; katika kufunga mara nyingi; katika baridi na kuwa uchi. 2 Wakorintho 11:27

in labor and travail, in watchings often, in hunger and thirst, in fastings often, and in cold and nakedness.

Baghairi ya mambo ya nje, yako yanijiayo kila siku, ndiyo maangalizi ya makanisa yote. 2 Wakorintho 11:28

Besides those things that are outside, there is that which presses on me daily, anxiety for all the assemblies.

Ni nani aliye dhaifu, nisiwe dhaifu nami? Ni nani aliyekwazwa nami nisichukiwe? 2 Wakorintho 11:29

Who is weak, and I am not weak? Who is caused to stumble, and I don't burn with indignation?

Ikinibidi kujisifu, nitajisifia mambo ya udhaifu wangu. 2 Wakorintho 11:30

If I must boast, I will boast of the things that concern my weakness.

Mungu, Baba wa Bwana Yesu, aliye mtukufu hata milele, anajua ya kuwa sisemi uongo. 2 Wakorintho 11:31

The God and Father of the Lord Jesus Christ, he who is blessed forevermore, knows that I don't lie.

Huko Dameski liwali wa mfalme Areta alikuwa akiulinda mji wa Wadameski, ili kunikamata; 2 Wakorintho 11:32

In Damascus the governor under Aretas the king guarded the city of the Damascenes desiring to arrest me.

nami nikatelemshwa ndani ya kapu, katika dirisha la ukutani, nikaokoka katika mikono yake. 2 Wakorintho 11:33

Through a window I was let down in a basket by the wall, and escaped his hands.