2 Wakorintho 10 Swahili & English

Listen/Download Audio
2 Wakorintho 10 (Swahili) 2nd Corinthians 10 (English)

Basi, mimi Paulo mwenyewe nawasihi kwa upole na utaratibu wa Kristo; mimi niliye mnyenyekevu nikiwapo pamoja nanyi, bali nisipokuwapo ni mwenye ujasiri kwenu; 2 Wakorintho 10:1

Now I Paul, myself, entreat you by the humility and gentleness of Christ; I who in your presence am lowly among you, but being absent am of good courage toward you.

naam, naomba kwamba nikiwapo, nisiwe na ujasiri kwa uthabiti ambao nahesabu kuwa nao juu ya wale wanaodhania ya kuwa sisi tunaenenda kwa jinsi ya mwili. 2 Wakorintho 10:2

Yes, I beg you that I may not, when present, show courage with the confidence with which I intend to be bold against some, who consider us to be walking according to the flesh.

Maana ingawa tunaenenda katika mwili, hatufanyi vita kwa jinsi ya mwili; 2 Wakorintho 10:3

For though we walk in the flesh, we don't wage war according to the flesh;

(maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome;) 2 Wakorintho 10:4

for the weapons of our warfare are not of the flesh, but mighty before God to the throwing down of strongholds,

tukiangusha mawazo na kila kitu kilichoinuka, kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu; na tukiteka nyara kila fikira ipate kumtii Kristo; 2 Wakorintho 10:5

throwing down imaginations and every high thing that is exalted against the knowledge of God, and bringing every thought into captivity to the obedience of Christ;

tena tukiwa tayari kupatiliza maasi yote, kutii kwenu kutakapotimia. 2 Wakorintho 10:6

and being in readiness to avenge all disobedience, when your obedience will be made full.

Yaangalieni yaliyo mbele ya macho yenu. Mtu akijitumainia mwenyewe ya kuwa ni mtu wa Kristo, na afikiri hivi pia nafsini mwake, ya kwamba kama yeye alivyo mtu wa Kristo, vivyo hivyo na sisi. 2 Wakorintho 10:7

Do you look at things only as they appear in front of your face? If anyone trusts in himself that he is Christ's, let him consider this again with himself, that, even as he is Christ's, so also we are Christ's.

Maana, nijapojisifu zaidi kidogo kwa ajili ya mamlaka yetu, (tuliyopewa na Bwana, tupate kuwajenga wala si kuwaangusha), sitatahayarika; 2 Wakorintho 10:8

For though I should boast somewhat abundantly concerning our authority, (which the Lord gave for building you up, and not for casting you down) I will not be disappointed,

nisije nikaonekana kana kwamba nataka kuwaogofya kwa nyaraka zangu. 2 Wakorintho 10:9

that I may not seem as if I desire to terrify you by my letters.

Maana wasema, Nyaraka zake ni nzito, hodari; bali akiwapo mwenyewe mwilini ni dhaifu, na maneno yake si kitu. 2 Wakorintho 10:10

For, "His letters," they say, "are weighty and strong, but his bodily presence is weak, and his speech is despised."

Mtu kama huyo na afikiri hivi, ya kwamba jinsi tulivyo kwa maneno katika nyaraka tusipokuwapo, ndivyo tulivyo kwa matendo tukiwapo. 2 Wakorintho 10:11

Let such a person consider this, that what we are in word by letters when we are absent, such are we also in deed when we are present.

Kwa kuwa hatuthubutu kujihesabu pamoja na baadhi yao wanaojisifu wenyewe, wala kujilinganisha nao; bali wao wenyewe wakijipima nafsi zao na nafsi zao, na wakijilinganisha nafsi zao na nafsi zao, hawana akili. 2 Wakorintho 10:12

For we are not bold to number or compare ourselves with some of those who commend themselves. But they themselves, measuring themselves by themselves, and comparing themselves with themselves, are without understanding.

Lakini sisi hatutajisifu zaidi ya kadiri yetu; bali kwa kadiri ya kipimo tulichopimiwa na Mungu, yaani, kadiri ya kufika hata kwenu. 2 Wakorintho 10:13

But we will not boast beyond proper limits, but within the boundaries with which God appointed to us, which reach even to you.

Maana hatujitanui nafsi zetu kupita kadiri yetu, kana kwamba hatuwafikii ninyi; kwa sababu tulitangulia kufika mpaka kwenu katika injili ya Kristo; 2 Wakorintho 10:14

For we don't stretch ourselves too much, as though we didn't reach to you. For we came even as far as to you with the Gospel of Christ,

wala hatujisifu zaidi ya kadiri yetu, yaani, katika taabu za watu wengine; bali tukiwa na tumaini ya kwamba, imani yenu ikuapo, tutakuzwa kwenu kwa kadiri ya kipimo chetu, na kupata ziada; 2 Wakorintho 10:15

not boasting beyond proper limits in other men's labors, but having hope that as your faith grows, we will be abundantly enlarged by you in our sphere of influence,

hata kuihubiri Injili katika nchi zilizo mbele kupita nchi zenu; tusijisifu katika kipimo cha mtu mwingine kwa mambo yaliyokwisha kutengenezwa. 2 Wakorintho 10:16

so as to preach the Gospel even to the parts beyond you, not to boast in what someone else has already done.

Lakini, Yeye ajisifuye, na ajisifu katika Bwana. 2 Wakorintho 10:17

But "he who boasts, let him boast in the Lord."

Maana mtu mwenye kukubaliwa si yeye ajisifuye, bali yeye asifiwaye na Bwana. 2 Wakorintho 10:18

For it isn't he who commends himself who is approved, but whom the Lord commends.