2 Wakorintho 3 Swahili & English

Listen/Download Audio
2 Wakorintho 3 (Swahili) 2nd Corinthians 3 (English)

Je! Tunaanza tena kujisifu wenyewe? Au tunahitaji, kama wengine, barua zenye sifa kuja kwenu, au kutoka kwenu? 2 Wakorintho 3:1

Are we beginning again to commend ourselves? Or do we need, as do some, letters of commendation to you or from you?

Ninyi ndinyi barua yetu, iliyoandikwa mioyoni mwetu, inajulikana na kusomwa na watu wote; 2 Wakorintho 3:2

You are our letter, written in our hearts, known and read by all men;

mnadhihirishwa kwamba mmekuwa barua ya Kristo tuliyoikatibu, iliyoandikwa si kwa wino, bali kwa Roho wa Mungu aliye hai; si katika vibao vya mawe, ila katika vibao ambavyo ni mioyo ya nyama. 2 Wakorintho 3:3

being revealed that you are a letter of Christ, ministered by us, written not with ink, but with the Spirit of the living God; not in tablets of stone, but in tablets that are hearts of flesh.

Na tumaini hilo tunalo mbele za Mungu kwa njia ya Kristo. 2 Wakorintho 3:4

Such confidence we have through Christ toward God;

Si kwamba twatosha sisi wenyewe kufikiri neno lo lote kwamba ni letu wenyewe, bali utoshelevu wetu watoka kwa Mungu. 2 Wakorintho 3:5

not that we are sufficient of ourselves, to account anything as from ourselves; but our sufficiency is from God;

Naye ndiye aliyetutosheleza kuwa wahudumu wa agano jipya; si wa andiko, bali wa roho; kwa maana andiko huua, bali roho huhuisha. 2 Wakorintho 3:6

who also made us sufficient as servants of a new covenant; not of the letter, but of the Spirit. For the letter kills, but the Spirit gives life.

Basi, ikiwa huduma ya mauti, iliyoandikwa na kuchorwa katika mawe, ilikuja katika utukufu, hata Waisraeli hawakuweza kuukazia macho uso wa Musa, kwa sababu ya utukufu wa uso wake; nao ni utukufu uliokuwa ukibatilika; 2 Wakorintho 3:7

But if the service of death, written engraved on stones, came with glory, so that the children of Israel could not look steadfastly on the face of Moses for the glory of his face; which was passing away:

je! Huduma ya roho haitazidi kuwa katika utukufu? 2 Wakorintho 3:8

won't service of the Spirit be with much more glory?

Kwa maana ikiwa huduma ya adhabu ina utukufu, siuze huduma ya haki ina utukufu unaozidi. 2 Wakorintho 3:9

For if the service of condemnation has glory, the service of righteousness exceeds much more in glory.

Maana hata ile iliyotukuzwa haikuwa na utukufu hivi, kwa sababu ya utukufu uzidio sana. 2 Wakorintho 3:10

For most assuredly that which has been made glorious has not been made glorious in this respect, by reason of the glory that surpasses.

Kwa maana, ikiwa ile inayobatilika ilikuwa na utukufu, zaidi sana ile ikaayo ina utukufu. 2 Wakorintho 3:11

For if that which passes away was with glory, much more that which remains is in glory.

Basi, kwa kuwa mna taraja la namna hii, twatumia ujasiri mwingi; 2 Wakorintho 3:12

Having therefore such a hope, we use great boldness of speech,

nasi si kama Musa alivyotia utaji juu ya uso wake, ili kwamba Waisraeli wasitazame sana mwisho wa ile iliyokuwa ikibatilika; 2 Wakorintho 3:13

and not as Moses, who put a veil on his face, that the children of Israel wouldn't look steadfastly on the end of that which was passing away.

ila fikira zao zilitiwa uzito. Kwa maana hata leo hivi, wakati lisomwapo Agano la Kale, utaji uo huo wakaa; yaani, haikufunuliwa kwamba huondolewa katika Kristo; 2 Wakorintho 3:14

But their minds were hardened, for until this very day at the reading of the old covenant the same veil remains, because in Christ it passes away.

ila hata leo, torati ya Musa isomwapo, utaji huikalia mioyo yao. 2 Wakorintho 3:15

But to this day, when Moses is read, a veil lies on their heart.

Lakini wakati wo wote watakapomgeukia Bwana, ule utaji huondolewa. 2 Wakorintho 3:16

But whenever one turns to the Lord, the veil is taken away.

Basi ndiye Roho; walakini alipo Roho wa Bwana, hapo ndipo penye uhuru. 2 Wakorintho 3:17

Now the Lord is the Spirit and where the Spirit of the Lord is, there is liberty.

Lakini sisi sote, kwa uso usiotiwa utaji, tukiurudisha utukufu wa Bwana, kama vile katika kioo, tunabadilishwa tufanane na mfano uo huo, toka utukufu hata utukufu, kama vile kwa utukufu utokao kwa Bwana, aliye Roho. 2 Wakorintho 3:18

But we all, with unveiled face beholding as in a mirror the glory of the Lord, are transformed into the same image from glory to glory, even as from the Lord, the Spirit.