2 Wakorintho 2 Swahili & English

Listen/Download Audio
2 Wakorintho 2 (Swahili) 2nd Corinthians 2 (English)

Lakini nafsini mwangu nalikusudia hivi, nisije kwenu tena kwa huzuni. 2 Wakorintho 2:1

But I determined this for myself, that I would not come to you again in sorrow.

Maana mimi nikiwatia huzuni, basi ni nani anifurahishaye mimi ila yeye ahuzunishwaye nami? 2 Wakorintho 2:2

For if I make you sorry, then who will make me glad but he who is made sorry by me?

Nami naliwaandikia neno lilo hilo, ili nijapo nisitiwe huzuni na wale ambao ilinipasa kuwafurahia; nikiwatumaini ninyi nyote kwamba furaha yangu ni yenu nyote pia. 2 Wakorintho 2:3

And I wrote this very thing to you, so that, when I came, I wouldn't have sorrow from them of whom I ought to rejoice; having confidence in you all, that my joy would be shared by all of you.

Maana katika dhiki nyingi na taabu ya moyo niliwaandikia na machozi mengi; si kwamba mhuzunishwe, bali mpate kujua upendo wangu nilio nao kwenu jinsi ulivyo mwingi. 2 Wakorintho 2:4

For out of much affliction and anguish of heart I wrote to you with many tears, not that you should be made sorry, but that you might know the love that I have so abundantly for you.

Lakini iwapo mtu amehuzunisha, hakunihuzunisha mimi tu, bali kwa sehemu (nisije nikalemea mno), amewahuzunisha ninyi nyote. 2 Wakorintho 2:5

But if any has caused sorrow, he has caused sorrow, not to me, but in part (that I not press too heavily) to you all.

Yamtosha mtu wa namna hii adhabu ile aliyopewa na walio wengi; 2 Wakorintho 2:6

Sufficient to such a one is this punishment which was inflicted by the many;

hata kinyume cha hayo, ni afadhali mmsamehe na kumfariji, mtu kama huyo asije akamezwa katika huzuni yake ipitayo kiasi. 2 Wakorintho 2:7

so that on the contrary you should rather forgive him and comfort him, lest by any means such a one should be swallowed up with his excessive sorrow.

Kwa hiyo nawasihi kumthibitishia upendo wenu. 2 Wakorintho 2:8

Therefore I beg you to confirm your love toward him.

Maana naliandika kwa sababu hii pia, ili nipate bayana kwenu kwamba mmekuwa wenye kutii katika mambo yote. 2 Wakorintho 2:9

For to this end I also wrote, that I might know the proof of you, whether you are obedient in all things.

Lakini kama mkimsamehe mtu neno lo lote, nami nimemsamehe; kwa maana mimi nami, ikiwa nimemsamehe mtu neno lo lote, nimemsamehe kwa ajili yenu mbele za Kristo, 2 Wakorintho 2:10

Now I also forgive whomever you forgive anything. For if indeed I have forgiven anything, I have forgiven that one for your sakes in the presence of Christ,

Shetani asije akapata kutushinda; kwa maana hatukosi kuzijua fikira zake. 2 Wakorintho 2:11

that no advantage may be gained over us by Satan; for we are not ignorant of his schemes.

Basi nilipofika Troa kwa ajili ya Injili ya Kristo, nikafunguliwa mlango katika Bwana, 2 Wakorintho 2:12

Now when I came to Troas for the Gospel of Christ, and when a door was opened to me in the Lord,

sikuona raha nafsini mwangu, kwa sababu sikumwona Tito ndugu yangu, bali niliagana nao, nikaondoka kwenda Makedonia. 2 Wakorintho 2:13

I had no relief for my spirit, because I didn't find Titus, my brother, but taking my leave of them, I went out into Macedonia.

Ila Mungu ashukuriwe, anayetushangiliza daima katika Kristo, na kuidhihirisha harufu ya kumjua yeye kila mahali kwa kazi yetu. 2 Wakorintho 2:14

Now thanks be to God, who always leads us in triumph in Christ, and reveals through us the sweet aroma of his knowledge in every place.

Kwa maana sisi tu manukato ya Kristo, mbele za Mungu, katika wao wanaookolewa, na katika wao wanaopotea; 2 Wakorintho 2:15

For we are a sweet aroma of Christ to God, in those who are saved, and in those who perish;

katika hao wa pili harufu ya mauti iletayo mauti; katika hao wa kwanza harufu ya uzima iletayo uzima. Naye ni nani atoshaye kwa mambo hayo? 2 Wakorintho 2:16

to the one a stench from death to death; to the other a sweet aroma from life to life. Who is sufficient for these things?

Kwa maana sisi si kama walio wengi, walighoshio neno la Mungu; bali kama kwa weupe wa moyo, kama kutoka kwa Mungu, mbele za Mungu, twanena katika Kristo. 2 Wakorintho 2:17

For we are not as so many, peddling the word of God. But as of sincerity, but as of God, in the sight of God, we speak in Christ.