2 Wakorintho 5 Swahili & English

Listen/Download Audio
2 Wakorintho 5 (Swahili) 2nd Corinthians 5 (English)

Kwa maana twajua ya kuwa nyumba ya maskani yetu iliyo ya dunia hii ikiharibiwa, tunalo jengo litokalo kwa Mungu, nyumba isiyofanywa kwa mikono, iliyo ya milele mbinguni. 2 Wakorintho 5:1

For we know that if the earthly house of our tent is dissolved, we have a building from God, a house not made with hands, eternal, in the heavens.

Maana katika nyumba hii twaugua, tukitamani sana kuvikwa kao letu litokalo mbinguni; 2 Wakorintho 5:2

For most assuredly in this we groan, longing to be clothed with our habitation which is from heaven;

ikiwa tukiisha kuvikwa hatutaonekana tu uchi. 2 Wakorintho 5:3

if so be that being clothed we will not be found naked.

Kwa sababu sisi tulio katika maskani hii twaugua, tukilemewa; si kwamba twataka kuvuliwa, bali kuvikwa, ili kitu kile kipatikanacho na mauti kimezwe na uzima. 2 Wakorintho 5:4

For indeed we who are in this tent do groan, being burdened; not that we desire to be unclothed, but that we desire to be clothed, that what is mortal may be swallowed up by life.

Basi yeye aliyetufanya kwa ajili ya neno lilo hilo ni Mungu, aliyetupa arabuni ya Roho. 2 Wakorintho 5:5

Now he who made us for this very thing is God, who also gave to us the down payment of the Spirit.

Basi siku zote tuna moyo mkuu; tena twajua ya kuwa, wakati tuwapo hapa katika mwili, tunakaa mbali na Bwana. 2 Wakorintho 5:6

Being therefore always of good courage, and knowing that, while we are at home in the body, we are absent from the Lord;

(Maana twaenenda kwa imani, si kwa kuona.) 2 Wakorintho 5:7

for we walk by faith, not by sight.

Lakini tuna moyo mkuu; nasi tunaona ni afadhali kutokuwamo katika mwili na kukaa pamoja na Bwana. 2 Wakorintho 5:8

We are of good courage, I say, and are willing rather to be absent from the body, and to be at home with the Lord.

Kwa hiyo, tena, ikiwa tupo hapa, au ikiwa hatupo hapa, twajitahidi kumpendeza yeye. 2 Wakorintho 5:9

Therefore also we make it our aim, whether at home or absent, to be well pleasing to him.

Kwa maana imetupasa sisi sote kudhihirishwa mbele ya kiti cha hukumu cha Kristo, ili kila mtu apokee ijara ya mambo aliyotenda kwa mwili, kadiri alivyotenda, kwamba ni mema au mabaya. 2 Wakorintho 5:10

For we must all be revealed before the judgment seat of Christ; that each one may receive the things in the body, according to what he has done, whether good or bad.

Basi tukiijua hofu ya Bwana, twawavuta wanadamu; lakini tumedhihirishwa mbele za Mungu. Nami natumaini ya kuwa tumedhihirishwa katika dhamiri zenu pia. 2 Wakorintho 5:11

Knowing therefore the fear of the Lord, we persuade men, but we are revealed to God; and I hope that we are revealed also in your consciences.

Maana hatujisifu wenyewe mbele yenu tena, bali tunawapa sababu ya kujisifu kwa ajili yetu, ili mpate kuwa nayo mbele yao wanaojisifu kwa mambo ya nje tu, wala si kwa mambo ya moyoni. 2 Wakorintho 5:12

For we are not commending ourselves to you again, but speak as giving you occasion of boasting on our behalf, that you may have something to answer those who boast in appearance, and not in heart.

Maana ikiwa tumerukwa na akili zetu, ni kwa ajili ya Mungu; au ikiwa tunazo akili zetu timamu, ni kwa ajili yenu. 2 Wakorintho 5:13

For if we are beside ourselves, it is for God. Or if we are of sober mind, it is for you.

Maana, upendo wa Kristo watubidisha; maana tumehukumu hivi, ya kwamba mmoja alikufa kwa ajili ya wote, basi walikufa wote; 2 Wakorintho 5:14

For the love of Christ constrains us; because we judge thus, that one died for all, therefore all died.

tena alikufa kwa ajili ya wote, ili walio hai wasiwe hai tena kwa ajili ya nafsi zao wenyewe, bali kwa ajili yake yeye aliyekufa akafufuka kwa ajili yao. 2 Wakorintho 5:15

He died for all, that those who live should no longer live to themselves, but to him who for their sakes died and rose again.

Hata imekuwa, sisi tangu sasa hatumjui mtu awaye yote kwa jinsi ya mwili. Ingawa sisi tumemtambua Kristo kwa jinsi ya mwili, lakini sasa hatumtambui hivi tena. 2 Wakorintho 5:16

Therefore we know no one after the flesh from now on. Even though we have known Christ after the flesh, yet now we know him so no more.

Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita tazama! Yamekuwa mapya. 2 Wakorintho 5:17

Therefore if anyone is in Christ, he is a new creation. The old things have passed away. Behold, all things have become new.

Lakini vyote pia vyatokana na Mungu, aliyetupatanisha sisi na nafsi yake kwa Kristo, naye alitupa huduma ya upatanisho; 2 Wakorintho 5:18

But all things are of God, who reconciled us to himself through Jesus Christ, and gave to us the ministry of reconciliation;

yaani, Mungu alikuwa ndani ya Kristo, akiupatanisha ulimwengu na nafsi yake, asiwahesabie makosa yao; naye ametia ndani yetu neno la upatanisho. 2 Wakorintho 5:19

namely, that God was in Christ reconciling the world to himself, not reckoning to them their trespasses, and having committed to us the word of reconciliation.

Basi tu wajumbe kwa ajili ya Kristo, kana kwamba Mungu anasihi kwa vinywa vyetu; twawaomba ninyi kwa ajili ya Kristo mpatanishwe na Mungu. 2 Wakorintho 5:20

We are therefore ambassadors on behalf of Christ, as though God were entreating by us. We beg you on behalf of Christ, be reconciled to God.

Yeye asiyejua dhambi alimfanya kuwa dhambi kwa ajili yetu, ili sisi tupate kuwa haki ya Mungu katika Yeye. 2 Wakorintho 5:21

For him who knew no sin he made to be sin on our behalf; so that in him we might become the righteousness of God.