Esta 3 Swahili & English

Listen/Download Audio
Esta 3 (Swahili) Esther 3 (English)

Baada ya hayo mfalme Ahasuero alimwongezea cheo Hamani bin Hamedatha, Mwagagi, akampandisha, akamwekea kiti chake juu ya maakida wote waliokuwapo pamoja naye. Esta 3:1

After these things did king Ahasuerus promote Haman the son of Hammedatha the Agagite, and advanced him, and set his seat above all the princes who were with him.

Nao watumishi wote wa mfalme, walioketi mlangoni pa mfalme, wakainama na kumsujudia Hamani, maana ndivyo alivyoamuru mfalme kwa habari zake. Bali Mordekai hakuinama, wala kumsujudia. Esta 3:2

All the king's servants, who were in the king's gate, bowed down, and did reverence to Haman; for the king had so commanded concerning him. But Mordecai didn't bow down, nor did him reverence.

Basi watumishi wa mfalme walioketi mlangoni pa mfalme wakamwambia Mordekai, Mbona wewe waihalifu amri ya mfalme? Esta 3:3

Then the king's servants, who were in the king's gate, said to Mordecai, Why disobey you the king's commandment?

Ikawa, waliposema naye kila siku asiwasikilize, wakamwarifu Hamani, ili kuona kama mambo yake Mordekai yatasimama; maana alikuwa amewaambia ya kuwa yeye ni Myahudi. Esta 3:4

Now it came to pass, when they spoke daily to him, and he didn't listen to them, that they told Haman, to see whether Mordecai's matters would stand: for he had told those who he was a Jew.

Hata Hamani alipoona ya kwamba Mordekai hainami wala kumsujudia, alighadhibika sana. Esta 3:5

When Haman saw that Mordecai didn't bow down, nor did him reverence, then was Haman full of wrath.

Akaona si shani kumtia mikono Mordekai peke yake; maana wamemjulisha kabila yake Mordekai; kwa hiyo Hamani alitaka kuwaangamiza Wayahudi wote waliokuwa wakikaa katika ufalme wote mzima wa Ahasuero, yaani, watu wake Mordekai. Esta 3:6

But he scorned the thought of laying hands on Mordecai alone; for they had made known to him the people of Mordecai: therefore Haman sought to destroy all the Jews who were throughout the whole kingdom of Ahasuerus, even the people of Mordecai.

Basi mwezi wa kwanza, ndio mwezi wa Nisani, mwaka wa kumi na mbili wa mfalme Ahasuero, wakapiga Puri, yaani kura, mbele yake Hamani; siku kwa siku, na mwezi kwa mwezi, hata mwezi wa kumi na mbili, ndio mwezi wa Adari. Esta 3:7

In the first month, which is the month Nisan, in the twelfth year of king Ahasuerus, they cast Pur, that is, the lot, before Haman from day to day, and from month to month, [to] the twelfth [month], which is the month Adar.

Basi Hamani akamwambia mfalme Ahasuero, Kuna taifa moja waliotawanyika na kukaa mahali mahali katikati ya mataifa walioko katika majimbo yote ya ufalme wako. Nao sheria zao zimefarakana na sheria za kila taifa; wala hawazishiki amri za mfalme; kwa hiyo haimpasi mfalme kuchukuliana nao. Esta 3:8

Haman said to king Ahasuerus, There is a certain people scattered abroad and dispersed among the peoples in all the provinces of your kingdom; and their laws are diverse from [those of] every people; neither keep they the king's laws: therefore it is not for the king's profit to allow them.

Basi, mfalme akiona vema, na iandikwe kwamba waangamizwe; nami nitalipa talanta kumi elfu za fedha mikononi mwao watakaosimamia shughuli hiyo, waziweke katika hazina ya mfalme. Esta 3:9

If it please the king, let it be written that they be destroyed: and I will pay ten thousand talents of silver into the hands of those who have the charge of the [king's] business, to bring it into the king's treasuries.

Ndipo mfalme alipoivua pete yake mkononi, akampa Hamani bin Hamedatha, Mwagagi, adui ya Wayahudi. Esta 3:10

The king took his ring from his hand, and gave it to Haman the son of Hammedatha the Agagite, the Jews' enemy.

Kisha mfalme akamwambia Hamani, Hiyo fedha umepewa, na watu pia, fanya uonavyo vema. Esta 3:11

The king said to Haman, The silver is given to you, the people also, to do with them as it seems good to you.

Basi, waandishi wa mfalme wakaitwa, siku ya kumi na tatu ya mwezi wa kwanza; na barua zikaandikwa, kama vile Hamani alivyoagiza vyote, kwa maakida wa mfalme, na maliwali waliokuwa juu ya kila jimbo, na wakuu wa kila taifa; kila jimbo kwa mwandiko wake, na kila taifa kwa lugha yake; zikaandikwa kwa jinsi la mfalme Ahasuero, na kutiwa muhuri kwa pete yake. Esta 3:12

Then were the king's scribes called in the first month, on the thirteenth day of it; and there was written according to all that Haman commanded to the king's satraps, and to the governors who were over every province, and to the princes of every people, to every province according to the writing of it, and to every people after their language; in the name of king Ahasuerus was it written, and it was sealed with the king's ring.

Barua zikapelekwa kwa mikono ya matarishi mpaka majimbo yote ya mfalme kuwaangamiza Wayahudi wote, na kuwaua, na kuwafisha, vijana kwa wazee, watoto wachanga na wanawake pia, siku moja, yaani, siku ya kumi na tatu ya mwezi wa kumi na mbili ndio mwezi wa Adari; na kuyachukua mali yao kuwa nyara. Esta 3:13

Letters were sent by posts into all the king's provinces, to destroy, to kill, and to cause to perish, all Jews, both young and old, little children and women, in one day, even on the thirteenth [day] of the twelfth month, which is the month Adar, and to take the spoil of them for a prey.

Nakili ya andiko, ya kupigwa mbiu katika kila jimbo, ilitangazwa kwa mataifa yote wawe tayari siku ile ile. Esta 3:14

A copy of the writing, that the decree should be given out in every province, was published to all the peoples, that they should be ready against that day.

Matarishi wakaondoka wakaenda haraka kwa amri ya mfalme; kukapigwa mbiu huko Shushani ngomeni. Mfalme na Hamani wakaketi ili kunywa divai; bali mji wa Shushani ukafadhaika. Esta 3:15

The posts went forth in haste by the king's commandment, and the decree was given out in Shushan the palace. The king and Haman sat down to drink; but the city of Shushan was perplexed.