Esta 2 Swahili & English

Listen/Download Audio
Esta 2 (Swahili) Esther 2 (English)

Baada ya hayo, hasira yake mfalme Ahasuero ilipotulia, alimkumbuka Vashti, na vile alivyotenda, na yale yaliyoamriwa juu yake. Esta 2:1

After these things, when the wrath of king Ahasuerus was pacified, he remembered Vashti, and what she had done, and what was decreed against her.

Basi watumishi wa mfalme waliomhudumu walimwambia, Mfalme na atafutiwe mabikira vijana wazuri; Esta 2:2

Then said the king's servants who ministered to him, Let there be beautiful young virgins sought for the king:

naye mfalme aweke wasimamizi katika majimbo yote ya ufalme wake, ili wakusanye pamoja mabikira vijana wazuri wote waende Shushani ngomeni, kwenye nyumba ya wanawake mikononi mwa Hegai, msimamizi-wa-nyumba wa mfalme, mwenye kuwalinda wanawake; tena wapewe vifaa vya utakaso. Esta 2:3

and let the king appoint officers in all the provinces of his kingdom, that they may gather together all the beautiful young virgins to Shushan the palace, to the house of the women, to the custody of Hegai the king's chamberlain, keeper of the women; and let their things for purification be given them;

Naye yule msichana atakayempendeza mfalme na awe malkia badala ya Vashti. Neno hilo likampendeza mfalme, naye akafanya hivyo. Esta 2:4

and let the maiden who pleases the king be queen instead of Vashti. The thing pleased the king; and he did so.

Basi palikuwa na Myahudi mmoja huko Shushani ngomeni; jina lake Mordekai, bin Yairi, bin Shimei, bin Kishi, wa kabila ya Benyamini; Esta 2:5

There was a certain Jew in Shushan the palace, whose name was Mordecai, the son of Jair, the son of Shimei, the son of Kish, a Benjamite,

ambaye kwamba amechukuliwa mateka kutoka Yerusalemu miongoni mwa wafungwa waliochukuliwa pamoja na Yekonia, mfalme wa Yuda; ambaye Nebukadreza, mfalme wa Babeli,alimchukua. Esta 2:6

who had been carried away from Jerusalem with the captives who had been carried away with Jeconiah king of Judah, whom Nebuchadnezzar the king of Babylon had carried away.

Naye alikuwa amemlea Hadasa, yaani, Esta, binti wa mjomba wake, kwa kuwa hana baba wala mama. Naye msichana huyu alikuwa wa umbo mzuri na uso mwema; nao walipokufa baba yake na mama yake, yule Mordekai alimtwaa kuwa binti yake yeye. Esta 2:7

He brought up Hadassah, who is, Esther, his uncle's daughter: for she had neither father nor mother, and the maiden was fair and beautiful; and when her father and mother were dead, Mordecai took her for his own daughter.

Basi ikawa, wakati iliposikiwa amri ya mfalme na mbiu yake, wasichana wengi wakakusanyika huko Shushani ngomeni mikononi mwa Hegai; Esta naye aliingizwa katika nyumba ya mfalme, mikononi mwa Hegai mwenye kuwalinda wanawake. Esta 2:8

So it happened, when the king's commandment and his decree was heard, and when many maidens were gathered together to Shushan the palace, to the custody of Hegai, that Esther was taken into the king's house, to the custody of Hegai, keeper of the women.

Yule mwanamwali akampendeza, akapokea fadhili kwake; naye akampa upesi vifaa vya utakaso, pamoja na posho zake, na vijakazi saba walio haki yake, wa nyumbani mwa mfalme. Pia akamhamisha yeye na vijakazi wake akawaweka mahali pazuri katika nyumba ya wanawake. Esta 2:9

The maiden pleased him, and she obtained kindness of him; and he speedily gave her things for her purification, with her portions, and the seven maidens who were meet to be given her out of the king's house: and he removed her and her maidens to the best place of the house of the women.

Walakini Esta hakudhihirisha kabila yake wala jamaa yake, kwa maana ndivyo alivyomwagiza Mordekai asiwadhihirishe. Esta 2:10

Esther had not made known her people nor her relatives; for Mordecai had charged her that she should not make it known.

Na yule Mordekai akawa akitembea kila siku mbele ya ua wa nyumba ya wanawake, ili ajue hali yake Esta, na hayo yatakayompata. Esta 2:11

Mordecai walked every day before the court of the women's house, to know how Esther did, and what would become of her.

Basi ilipowadia zamu yake mwanamwali mmojawapo aingie kwa mfalme Ahasuero, hali akiisha kufanyiwa sawasawa na sheria ya wanawake miezi kumi na miwili; yaani, ndivyo zilivyotimia siku zao za utakaso, miezi sita kwa mafuta ya manemane, na miezi sita kwa manukato na vifaa vya utakaso wa wanawake; Esta 2:12

Now when the turn of every maiden was come to go in to king Ahasuerus, after it had been done to her as prescribed for the women twelve months (for so were the days of their purification accomplished, [to wit], six months with oil of myrrh, and six months with sweet odors and with the things for the purifying of the women),

mwanamwali huingia hivyo kwa mfalme; kila akitakacho hupewa kwenda nacho kutoka katika nyumba ya wanawake ili kuingia katika nyumba ya mfalme. Esta 2:13

then in this wise came the maiden to the king: whatever she desired was given her to go with her out of the house of the women to the king's house.

Huenda jioni, na asubuhi hurudi nyumba ya pili ya wanawake, mikononi mwa Shaashgazi, msimamizi wake mfalme, mwenye kuwalinda masuria. Wala haingii tena kwa mfalme, isipokuwa amempendeza mfalme, naye akaitwa kwa jina. Esta 2:14

In the evening she went, and on the next day she returned into the second house of the women, to the custody of Shaashgaz, the king's chamberlain, who kept the concubines: she came in to the king no more, except the king delighted in her, and she were called by name.

Hata ilipowadia zamu yake Esta, binti Abihaili, mjomba wake Mordekai, ambaye alimtwaa kuwa binti yake, ili aingie kwa mfalme, yeye hakutaka kitu, ila vile vilivyoagizwa na Hegai, msimamizi wake mfalme, mwenye kuwalinda wanawake. Naye huyu Esta alikuwa amepata kibali machoni pa wote waliomwona. Esta 2:15

Now when the turn of Esther, the daughter of Abihail the uncle of Mordecai, who had taken her for his daughter, was come to go in to the king, she required nothing but what Hegai the king's chamberlain, the keeper of the women, appointed. Esther obtained favor in the sight of all those who looked at her.

Basi Esta alipelekwa kwa mfalme Ahasuero, katika nyumba ya kifalme, mwezi wa kumi, ndio mwezi wa Tebethi, mwaka wa saba wa kumiliki kwake. Esta 2:16

So Esther was taken to king Ahasuerus into his house royal in the tenth month, which is the month Tebeth, in the seventh year of his reign.

Mfalme akampenda Esta kuliko wanawake wote, naye akapata neema na kibali machoni pake kuliko mabikira wote; basi akamtia taji ya kifalme kichwani pake, akamfanya awe malkia badala ya Vashti. Esta 2:17

The king loved Esther above all the women, and she obtained favor and kindness in his sight more than all the virgins; so that he set the royal crown on her head, and made her queen instead of Vashti.

Ndipo mfalme alipowafanyia karamu kubwa maakida wake wote na watumishi wake, yaani, karamu yake Esta; akafanya msamaha katika majimbo yote, akatoa zawadi sawasawa na ukarimu wa mfalme. Esta 2:18

Then the king made a great feast to all his princes and his servants, even Esther's feast; and he made a release to the provinces, and gave gifts, according to the bounty of the king.

Basi mabikira walipokusanyika mara ya pili, Mordekai alikuwa akiketi mlangoni pa mfalme. Esta 2:19

When the virgins were gathered together the second time, then Mordecai was sitting in the king's gate.

Esta alikuwa hajadhihirisha jamaa yake wala kabila yake, kama vile Mordekai alivyomwagiza; kwa maana Esta alikuwa akiyashika maagizo ya Mordekai, vile vile kama wakati alipolelewa naye. Esta 2:20

Esther had not yet made known her relatives nor her people; as Mordecai had charged her: for Esther did the commandment of Mordecai, like as when she was brought up with him.

Ikawa siku zile, Mordekai alipokuwa akiketi mlangoni pa mfalme, wawili katika wasimamizi wake mfalme, Bigthana na Tereshi, wangoje mlango, walighadhibika, wakataka kumpelekea mikono mfalme Ahasuero. Esta 2:21

In those days, while Mordecai was sitting in the king's gate, two of the king's chamberlains, Bigthan and Teresh, of those who kept the threshold, were angry, and sought to lay hands on the king Ahasuerus.

Basi Mordekai akapata kulijua jambo hilo, naye akamjulisha Esta, malkia; naye Esta akamwambia mfalme habari hiyo kwa jina la Mordekai. Esta 2:22

The thing became known to Mordecai, who shown it to Esther the queen; and Esther told the king [of it] in Mordecai's name.

Na jambo hilo lilipochunguzwa, na hakika ikapatikana, hao wote wawili wakatundikwa juu ya mti. Hayo pia yakaandikwa katika kitabu cha taarifa mbele ya mfalme. Esta 2:23

When inquisition was made of the matter, and it was found to be so, they were both hanged on a tree: and it was written in the book of the chronicles before the king.