Esta 7 Swahili & English

Listen/Download Audio
Esta 7 (Swahili) Esther 7 (English)

Basi mfalme na Hamani walikuja kula karamu pamoja na malkia Esta. Esta 7:1

So the king and Haman came to banquet with Esther the queen.

Mfalme akamwambia Esta tena siku ya pili pale pale penye karamu ya divai, Malkia Esta, dua yako ni nini? Nawe utapewa; na haja yako ni nini? Hata nusu ya ufalme utafanyiziwa. Esta 7:2

The king said again to Esther on the second day at the banquet of wine, What is your petition, queen Esther? and it shall be granted you: and what is your request? even to the half of the kingdom it shall be performed.

Ndipo malkia Esta alipojibu, akasema, Mfalme, ikiwa nimepata kibali machoni pako, na mfalme akiona vema, nipewe maisha yangu kuwa dua yangu, na watu wangu kuwa haja yangu. Esta 7:3

Then Esther the queen answered, If I have found favor in your sight, O king, and if it please the king, let my life be given me at my petition, and my people at my request:

Maana tumeuzwa, mimi na watu wangu, ili tuharibiwe, na kuuawa, na kuangamia. Kama tungaliuzwa kuwa watumwa na wajakazi, ningalinyamaza; ila hata hivyo msiba wetu haulinganishwi na hasara ya mfalme. Esta 7:4

for we are sold, I and my people, to be destroyed, to be slain, and to perish. But if we had been sold for bondservants and bondmaids, I had held my peace, although the adversary could not have compensated for the king's damage.

Ndipo mfalme Ahasuero aliponena, akamwambia malkia Esta, Ni nani huyu, tena yuko wapi, ambaye moyoni mwake alithubutu kufanya hivi? Esta 7:5

Then spoke the king Ahasuerus and said to Esther the queen, Who is he, and where is he, that dared presume in his heart to do so?

Esta akasema, Ni mtesi, tena ni adui, ndiye huyu Hamani, mtu mbaya kabisa. Mara Hamani akaingiwa na hofu mbele ya mfalme na malkia. Esta 7:6

Esther said, An adversary and an enemy, even this wicked Haman. Then Haman was afraid before the king and the queen.

Mfalme akaondoka katika ghadhabu yake kutoka kwenye karamu ya divai, akaingia bustani ya ngome. Hamani naye akasimama ili ajitakie maisha yake kwa malkia Esta; kwa kuwa aliona ya kwamba amekusudiwa madhara na mfalme. Esta 7:7

The king arose in his wrath from the banquet of wine [and went] into the palace garden: and Haman stood up to make request for his life to Esther the queen; for he saw that there was evil determined against him by the king.

Kisha mfalme akarudi kutoka katika bustani ya ngome hata mahali pa karamu ya divai. Ikawa Hamani amejitupa chini penye kitanda alipokuwapo Esta. Mfalme akasema, Namna gani! Je! Atamfanyia malkia jeuri hata machoni pangu nyumbani mwangu? Na neno lilipotoka kinywani mwa mfalme, wakamfunika uso Hamani. Esta 7:8

Then the king returned out of the palace garden into the place of the banquet of wine; and Haman was fallen on the couch whereon Esther was. Then said the king, Will he even force the queen before me in the house? As the word went out of the king's mouth, they covered Haman's face.

Ndipo aliposema Harbona, msimamizi-wa-nyumba mmojawapo wa wale waliohudhuria mbele ya mfalme, Tazama, basi, mti wa mikono hamsini urefu wake, Hamani aliomwekea tayari Mordekai, ambaye alinena vema kwa ajili ya mfalme, upo umesimamishwa nyumbani kwa Hamani. Mfalme akasema, Mtundikeni juu yake. Esta 7:9

Then said Harbonah, one of the chamberlains who were before the king, Behold also, the gallows fifty cubits high, which Haman has made for Mordecai, who spoke good for the king, stands in the house of Haman. The king said, Hang him thereon.

Basi wakamtundika Hamani juu ya mti aliomwekea tayari Mordekai. Ghadhabu ya mfalme ikatulia.

Esta 7:10

So they hanged Haman on the gallows that he had prepared for Mordecai. Then was the king's wrath pacified.