Wimbo Mpya Lyrics

The Saints Ministers swahili

Chorus:
Nina Imani nitaimba wimbo mpya, wimbo wa washindi, nifikapo kando ya Bahari ya kioo furaha ghaya, Yesu Kristo Mkombozi wetu, atatuimbisha wimbo mpya, atanipa sauti nzuri kushinda hii.

Wimbo Mpya Video

Buy/Download Audio

Wimbo Mpya Lyrics

Nina Imani nitaimba wimbo mpya, wimbo wa washindi, nifikapo kando ya Bahari ya kioo furaha ghaya, Yesu Kristo Mkombozi wetu, atatuimbisha wimbo mpya, atanipa sauti nzuri kushinda hii.

1. Wimbo haujaimbwa tangu kuumbwa kwa dunia, wimbo mtamu mzuri, wimbo mpya, Malaika hawautambui wastaajabu kwa umbali, Hawauenzi, hawafahamu wimbo huo. 

2. Tarumbeta, vunubi, na zeze zasikika kote, Ni anga la Muziki uchezwao kwa ustadi Mkuu, wimbo wa sifa kwa Kuhani Mkuu. 

3. Wale wazee ishirini na wanne.. 
  Wainama na kuinuka, wakimsujudu Bwana, Mkuu wa majeshi, (Hapo ndipo penye subira,) ya watakatifu, walioshika amri zake, na IMANI yake Yesu, Tazama nikaona, Mwanakondoo amesimama juu ya mlima zayuni, na Watu mia na arobaini na nne elfu, vipaji vya nyuso zao jina la Baba na Mwana, Nikasikia sauti toka mbinguni, kama ya maji mengi, kama ya radi Kuu, kama ya wapiga vunubi wakipiga vunubi vyao, (Sifa kwa Kuhani mkuu)