Sarah Magesa - Kumbe Upo Hivi Lyrics

Kumbe Upo Hivi Lyrics

Kumbe upo hivi Baba
Kumbe upo hivi Yesu
Kumbe upo hivi Baba
Kumbe upo hivi Yesu

Matendo yako mungu
Yananifanya nishangae
Huruma zako Baba
Zinanifanya nishangae
Matendo yako mungu
Yananifanya nishangae
Huruma zako Baba
Zinanifanya nishangae

Yale unayotenda Baba
Hakuna awezaye kutendaaa
Umenitoa chini mavumbini
Ukanipandisha juu kwa neema yakoo
Ukaniweka juu mpaka kileleli
Ukaniketisha na wakubwa bwana

Kumbe upo hivi Baba (upo hivi Baba)
Kumbe upo hivi Yesu (upo hivi Yesu)
Kumbe upo hivi Baba
Kumbe upo hivi Yesu (unatisha Yesu)
Kumbe upo hivi Baba (wewe ni wa ajabu)
Kumbe upo hivi Yesu (mataifa yanakushangaa)
Kumbe upo hivi Baba (upo hivii Babaa)
Kumbe upo hivi Yesu

Yesu na wanafunzi wake
Walipokuwa wakisafirii
Walipokuwa katikatii ya bahari
Bahari imechafuka, sena eeeh eeh
Walilia walilia sana oohwa
Walilia wakiumia mioyo
Walipolalamika juu yako mungu
Ukasimama, ukasimamisha dhoruba
Wakabaki wanashangaa, shangaa na kuulizana aah
Huyu ni mtu wa namna ganii
Mbona bahari imrtii, dhoruba imetulia
Huyu ni mtu wa namna gani ?
Ndivyo ilivyo na mimi, Baba
Nashangaa, umenihurumia, mungu
Niliyeonekana sifai katikati ya watu umeniheshimisha
Niliyedharauliwa katikati ya wengi umetela heshima
Kumbe upo hivi Babaa
Katikati ya huzuni unaleta furaha
Kumbe upo hivi Yesu
Katikati ya kulia unaleta kicheko
Kumbe upo hivi Yesu mwanaume wa wanaume
Katikati ya magonjwa unaleta uzima

Kumbe upo hivi Baba (magonjwa yanaondoka)
Kumbe upo hivi Yesu, umasikini unaondokaa
Kumbe upo hivi Baba
Kumbe upo hivi Yesu (Baaabaaa aaah)
Kumbe upo hivi Baba
Kumbe upo hivi Yesu
Kumbe upo hivi Baba
Kumbe upo hivi Yesu

Nakuomba mungu wangu
Nakuomba Baba yangu
Wakumbuke watu hawa wanaopitia magumu
Wakumbuke watu hawa wenye vilio mioyoni mwao
Wakumbuke watu hawa waliokata tamaa
Wakumbuke watu hawa wasio na majibu Yesu
Kama ulivyomkumbuka
Meshaki abednego na
Shadrack kwenye moto ule
Walitupwa watatu mungu aah
Walitupwa watatu wakawa hawana majibu
Kumbe wewe mungu ulikuwa wane kwao
Uliwaokoa na moto ule Yesu
Kumbe mungu wewe upo hivi
Kumbe Baba wewe upo hivi
Kumbe mungu wewe upo hivi

Kumbe upo hivi Baba (simba wa yuda)
Kumbe upo hivi Yesu (bwana wa bwana)
Kumbe upo hivi Baba (nguvu yaaangu)
Kumbe upo hivi Yesu
Kumbe upo hivi Baba
Kumbe upo hivi Yesu
Kumbe upo hivi Baba
Kumbe upo hivi Yesu


Kumbe Upo Hivi Video

Sarah Magesa Songs

Related Songs