Sifa Lyrics

Amenifanyia Amani by Paul Clement cover art

Paul Clement - Amenifanyia Amani Lyrics

Artist:
Paul Clement
Album:
Usiyeshindwa
Official Release:
06 Feb 2019

Lyrics

Amenifanyia amani
Amenifanyia amani
Kaondoa huzuni yangu
Kanifanyia amani.


Nijapopita, kwenye bonde la mauti
Sitaogopa, maana wewe uko nami
Gongo lako na fimbo yako, eh Bwana vyanifariji
Wanifanyia amani umesema, ya kwamba hutaniacha
Sababu mimi, ni mboni ya jicho lako
Bwana wanitazama, asubuhi, mchana, jioni
Eeh Bwana, kweli Mungu wa baraka


Amenifanyia amani
Amenifanyia amani
Kaondoa huzuni yangu
Kanifanyia amani.


Amebadilisha uchungu wangu, umekua ni furaha yangu
Oh huyu Yesu amenipa furaha
Kanifanyia amani
Amebadilisha machozi yangu yamekuwa ni furaha yangu oooh!
Huyu Yesu amenipa furaha kanifanyia amani


Amenifanyia amani
Amenifanyia amani
Kaondoa huzuni yangu
Kanifanyia amani.


Furaha unipayo siyo kama ya dunia hii
Amani unipayo siyo kama ya ulimwengu huu
Wewe waniganga moyo nipatapo uchungu
Wanifanyia amani


Amenifanyia furaha
Amenifanyia furaha
Kaondoa huzuni yangu
Kanifanyia furaha.


Video