Enda Nasi - Tunaomba Uwepo Wako Uende Nasi

Mp3

Tunaomba uwepo wako uende nasi
Ewe Bwana wa majeshi utusikie
Kama huendi nasi, hatutaki kutoka hapa
Hatuwezi pekee yetu, enda nasi
Tu watu wa shingo ngumu tusamehe
Hatufai mbele zako, turehemu
Tusafishe ee Baba, tuonyeshe uso wako
Twahitaji neema yako, enda nasi

Tutavua mapambo yetu
Na vitu vyote vya thamani kwetu
Mioyo yetu twaleta mbele zako
Tutakase na utembee nasi

Tunaomba utuonyeshe njia zako
Kwa maana umetuita kwa jina
Twalilia Ee Bwana, utukufu na uso wako
Bila wewe tutashindwa, enda nasi

Tutavua mapambo yetu
Na vitu vyote vya thamani kwetu
Mioyo yetu twaleta mbele zako
Tutakase na utembee nasi


Top Songs United States
Share:

Write a review/comment/correct the lyrics of Enda Nasi - Tunaomba Uwepo Wako Uende Nasi:

22 Comments/Reviews

 • Fidelis Musyoka

  Inanibamba sana 4 months ago

 • Thomas Mwalwala Mwaisabu

  your song's thy realy bless me God bless you 4 months ago

 • Suzzane Kamola Mulindu

  Am spirit filled. Have been repeatedly doing this song, and I can feel the spirit moving in my Son's Exam Room. 8 months ago

 • Martha

  I'm singing right now. The song touch my heart 8 months ago

 • Andrew Senior

  very powerful it's like am am having dinner with Jesus Christ 9 months ago

 • JUDY JUMA

  powerful song 10 months ago

 • Sandrea

  wonderful song
  10 months ago

 • Violet

  Barikiwa mtumishi 11 months ago

 • Valerian Baltazary

  wimbo huu ni nzuri sana. 11 months ago

 • Samuel Nsabimana

  Nyimbo nzuli saana.kama kiumbe cha Mungu,ili ndio ombi kubwa tunaloweza kutumia. 1 year ago

 • Load More Comments