Erasto Shengezi

Amenitoa Mbali - Acha Nikuimbie Amen Haleluya Amen Lyrics

Niseme nini bwana kwa ajili ya upendo wako,
Baba uliacha utukufu mbinguni
Baba kwa ajili ya dhambi zangu
ukaishi kama mwanadamu
kwa ajilli yangu Baba,
Wowo oh Ayaya.

Kama sio wewe Baba wangu ningelikuwa wapi mimi?
Kama sio upendo wako mkuu Yesu wangu ningekuwa nimekufa,
Nilikuwa mbali na wokovu wako, Massiah Yesu
Na hukumu yako ilikuwa juu yangu, lakini ukakubali kushuka
Ili unifilie, mimi niitwe mwana wa Mungu,
Sasa leo mimi naimba, saa leo mimi ni Huru
kwa Damu yako Masiah iliyomwagika msalabani!

Acha nikuimbie, amen
Acha nikuabudu, amen
Acha nikuinue, Amen
Amen Haleluya amen
Nani kama wewe? Amen
Angekubali kunifia Bwana, amen
Oh Amen,Oh Hallelujah Amen

Kuzunguka nimezunguka hata mbio nimekimbia,
kutafuta rafiki Baba sikupata kama wewe,
Nashukuru kwa upendo wako nimeona wema wako,
Wokovu nimeuona, sasa naimba Halleluyah...
Naita milele lele Amen.
Mwimbie Yesu wangu Hakuna kama wewe wanipenda Jinsi

Acha nikuimbie, amen
Kimbilio la maisha yangu, amen
Unastahili sifa baba Yangu
Amen Haleluya amen
Kama sio wewe ningelikuwa wapi, amen
Unastahili sifa Baba, amen
Yelele hehe
Amen Haleluya Amen
Ooh Yesu upewe sifa, Amen
Uinuliwe Masaiah wangu,amen
Ulikubali aibu Baba Yangu,
Amen Haleluya amen
Nilikuwa nimekufa, amen
Nilikuwa nimeenda mbali, amen
Upewe sifa Baba, amen
Haleluya amen


Amenitoa Mbali - Acha Nikuimbie Amen Haleluya Amen Video

Source: Amenitoa Mbali - Acha Nikuimbie Amen Haleluya Amen Lyrics - Erasto Shengezi