Sifa Lyrics

Kama Sio Wewe 1 by Emily Kanchori cover art

Emily Kanchori - Kama Sio Wewe 1 Lyrics

Artist:
Emily Kanchori

Lyrics

Ulinijua toka tumboni mwa mama yangu
mkono wako mkuu ukawa juu yangu
ukanipenda hata pasipokukutambua
ukanitoa mautini ukanifanya wako


Chorus
kama sio wewe Yesu ningekuwa wapi?
nashukuru Baba kwa upendo wako mkuu
kama sio wewe Yesu ningekuwa wapi?
nashukuru Baba kwa upendo wako mkuu


safari pamoja nawe sio mteremko
milima mabonde umenikomboa Yesu
uliahidi kutoniacha pekee yangu
nashuhudia uaminifu wako kwangu


Chorus
kama sio wewe Yesu ningekuwa wapi?
nashukuru Baba kwa upendo wako mkuu
kama sio wewe Yesu ningekuwa wapi?
nashukuru Baba kwa upendo wako mkuu


safarini Baba nimekuita ukaitika
safarini Baba machozi mengi umeyafuta
nimejua Mungu ajibuye maombi
nimepata rafiki asiyebadilika


Chorus
kama sio wewe Yesu ningekuwa wapi?
nashukuru Baba kwa upendo wako mkuu
kama sio wewe Yesu ningekuwa wapi?
nashukuru Baba kwa upendo wako mkuu


Video