Sifa Lyrics

Mwenye Nguvu by Burton King cover art

Burton King - Mwenye Nguvu Lyrics

Artist:
Burton King

Lyrics

Nasongea miguuni pako ,mimi mnyonge,mdhaifu


Unanguvu za kuinua moyo wangu


Nimejaribu kwa nguvu zangu,kwa Elimu yangu, ujanja wangu


Nimeshindwa nimekuja kwako Mungu mwenye nguvu


Maana wewe nguvu yangu, uwezo wangu,ushindi wangu


Unishike uyavute machozi yangu.


Maana ni wewe


Ni wewe mwenye nguvu,za kuinua moyo wangu


Moyo wangu baba


ili mimi nizungumze nawe. 


(Tena)


Tena ni wewe mwenye uwezo wa kuinua maisha yangu


ili mimi niishi nawe.


Ni wewe mwenye nguvu za kuinua moyo wangu


ili mimi nizungumze nawe


Tena ni wewe mwenye uwezo wa kuinia maisha yangu 


ili mimi niishi nawe.


Nimejaribu wanadamu baba


Wanadamu wanashida zao pia nao,wanakuhitaji wewe


Nimejaribu dunia yote


Dunia nayo baba inashida zake,inakuhitaji wewe


Ni wewe tu msaada wangu yesu


Ndio maana naja kwako


Unajulikana simba wa Yuda mtetezi wangu


Bendera ya ushindi wangu nakuamini ...


Ni wewe mwenye nguvu zakuinua moyo wangu


ili mimi nizungumze na wewe


Tena ni wewe mwenye uwezo wakuinua maisha yangu


ili mimi niishi nawe


Ni wewe mwenye nguvu za kuinua moyo wangu


ili mimi nizungumze nawe


Tena ni wewe mwenye uwezo wa kuinua maisha yangu


ili mimi niishi nawe


ili mimi niishi nawe 


ili mimi niishi nawe


Video