Boaz Danken

Ameshinda Yesu Lyrics

Kulikuwa na vita mbinguni 
Malaika wa Mungu 
Walipigana na yule joka 
Adui wa imani 

Wakamshinda kwa neno la ushuhuda 
Wakamshinda kwa damu ya mwanakondoo 

Ameshinda Yesu kifo na kaburi 
Ameshinda Yesu mfalme wa amani 

Halleluya Halleluya 
Halleluya Halleluya 

Tumeingia kwenye agano 
Agano la milele 
Tumewekewa muhuri kwa damu 
Damu ya mwanakondoo 

Upande wetu sisi ni washindi 
Tumeshinda pamoja naye 
Kwa kumuamini Yesu kaingia moyoni 
Tutatawala pamoja naye 

Ameshinda Yesu kifo na kaburi 
Ameshinda Yesu mfalme wa amani 

Halleluya Halleluya 
Halleluya Halleluya 

Alizidi enzi mamlaka 
Kagongemelewa msalabani 
*Akaziuia mkoko alipokuwa Goligotha 
Adhabu Ya Mungu kwa wanadamu 
Ilikuwa begani mwake 
Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona 
Ushindi tunao 

Ameshinda Yesu kifo na kaburi 
Ameshinda Yesu mfalme wa amani 

Halleluya Halleluya 
Halleluya Halleluya 

Habari njema zienee 
Mataifa yasikie 
Mfalme wetu Yesu kristo 
Ameshinda kifo na kaburi 
Wivu wa Mungu umezidi 
Alikumbuka agano lake 
Uzao wa mwanamke 
Utakuponda kichwa wewe joka 
Yesu uzao wa mwanamke 
Amemponda kichwa joka shetani 
Tumeuona utukufu kama wa mwana pekee wa Mungu 
Yaliyonenwa na manabii torati na waamuzi 
Yametimia mikononi mwake 
Yesu mwana wa Mungu 

Ameshinda Yesu kifo na kaburi 
Ameshinda Yesu mfalme wa amani 


Ameshinda Yesu Video

Source: Ameshinda Yesu Lyrics - Boaz Danken