Mercy Wairegi - Kama Si Wewe Lyrics

Lyrics

Pendo gani hili, bwana ukanipenda kabla nikujue, wewe umenipenda mimi nani sasa, bila wewe maishani kabla nikujue, wewe ulinipenda na wakati nakukosea, Bwana wee wanisamehe waniita mwana wako, hata wakati ni dhaifu sistahili mbele zako, naja kwa unyenyekevu kwani mimi bila wewe, mimi si kitu, si kitu

ningekuwa wapi, kama si wewe ningeitwa nani, kama si wewe ningefanya nini, kama si wewe kwani bila wewe, mimi si kitu

nikikumbuka jinsi ulivyo,sina la kusema nilipotea, kwenye dhambi ukaniokoa mimi ni nani, mbele zako kama sio wewe,ningekuwa wapi kama si wewe,ulinipenda ukanionyesha njia.ulinipenda ukaniokoa sina mwingine

ningekuwa wapi, kama si wewe ningeitwa nani, kama si wewe ningefanya nini, kama si wewe kwani bila wewe, mimi si kitu

najitoa kwako bwana, uinuke ndani yangu mimi kwako mtumishi, nitumie upendavyo najitoa kwako bwana,nitumie upendavyo mimi kwako mtumishi, nakuomba nitumie nijaze, nijaze, nijaze na roho yako nifinyange, nitumie, najitoa mbele zako

ningekuwa wapi, kama si wewe ningeitwa nani, kama si wewe ningefanya nini, kama si wewe kwani bila wewe, mimi si kitu

@ Billy Frank & Mercy Wairege

Kama Si wewe (Were it not for You)

Video

Kama Sio Wewe By Mercy Wairegi Njenga (Official video)

Thumbnail for Kama Si Wewe video
Loading...
In Queue
View Lyrics