Esta 8 Swahili & English

Listen/Download Audio
Esta 8 (Swahili) Esther 8 (English)

Siku ile mfalme Ahasuero alimpa malkia Esta nyumba yake Hamani, yule adui ya Wayahudi. Mordekai naye akahudhuria mbele ya mfalme; kwa maana Esta alikuwa amedhihirisha alivyomhusu. Esta 8:1

On that day did the king Ahasuerus give the house of Haman the Jews' enemy to Esther the queen. Mordecai came before the king; for Esther had told what he was to her.

Basi mfalme akaivua pete yake, aliyompokonya Hamani, akampa Mordekai. Naye Esta akamweka Mordekai kuwa juu ya mlango wake Hamani. Esta 8:2

The king took off his ring, which he had taken from Haman, and gave it to Mordecai. Esther set Mordecai over the house of Haman.

Tena Esta akasema na mfalme mara ya pili, akaanguka miguuni pake, akamsihi kwa machozi ayaondoe madhara ya Hamani, Mwagagi, na shauri alilowafanyia Wayahudi. Esta 8:3

Esther spoke yet again before the king, and fell down at his feet, and begged him with tears to put away the mischief of Haman the Agagite, and his device that he had devised against the Jews.

Ndipo mfalme alipomnyoshea Esta fimbo yake ya dhahabu. Basi Esta akaondoka, akasimama mbele ya mfalme. Esta 8:4

Then the king held out to Esther the golden scepter. So Esther arose, and stood before the king.

Akasema, Mfalme akiona vema, nami nikiwa nimepata kibali machoni pake, na neno likionekana jema mbele ya mfalme, nami nikimpendeza machoni pake, iandikwe kuzitangua barua za Hamani bin Hamedatha, Mwagagi, alizotunga na kuziandika ili kuwaangamiza Wayahudi walioko katika majimbo yote ya mfalme. Esta 8:5

She said, If it please the king, and if I have found favor in his sight, and the thing seem right before the king, and I be pleasing in his eyes, let it be written to reverse the letters devised by Haman, the son of Hammedatha the Agagite, which he wrote to destroy the Jews who are in all the king's provinces:

Kwa maana niwezeje kuyaona mabaya yatakayowajia watu wangu? Au niwezeje kuyatazama maangamizo ya jamaa zangu? Esta 8:6

for how can I endure to see the evil that shall come to my people? or how can I endure to see the destruction of my relatives?

Mfalme Ahasuero akawaambia malkia Esta na Mordekai, Myahudi, kusema, Tazama, nimekwisha kumpa Esta nyumba yake Hamani, naye mwenyewe wamekwisha kumtundika juu ya mti, kwa sababu aliwatia mikono Wayahudi. Esta 8:7

Then the king Ahasuerus said to Esther the queen and to Mordecai the Jew, See, I have given Esther the house of Haman, and him they have hanged on the gallows, because he laid his hand on the Jews.

Basi waandikieni Wayahudi pia vyo vyote mpendavyo, kwa jina la mfalme, mkatie muhuri kwa pete ya mfalme; kwa kuwa andiko lililoandikwa kwa jina la mfalme na kutiwa muhuri kwa pete ya mfalme hakuna awezaye kulitangua. Esta 8:8

Write you also to the Jews, as it pleases you, in the king's name, and seal it with the king's ring; for the writing which is written in the king's name, and sealed with the king's ring, may no man reverse.

Basi, waandishi wa mfalme wakaitwa pale pale, siku ya ishirini na tatu ya mwezi wa tatu, ndio mwezi wa Siwani; na kama vile Mordekai alivyoamuru, Wayahudi wakaandikiwa, pamoja na maakida na maliwali, na wakuu wa majimbo toka Bara Hindi mpaka Kushi, majimbo mia na ishirini na saba, kila jimbo kwa mwandiko wake, na kila taifa kwa lugha yake; na Wayahudi kwa mwandiko wao na kwa lugha yao. Esta 8:9

Then were the king's scribes called at that time, in the third month Sivan, on the three and twentieth [day] of it; and it was written according to all that Mordecai commanded to the Jews, and to the satraps, and the governors and princes of the provinces which are from India to Ethiopia, one hundred twenty-seven provinces, to every province according to the writing of it, and to every people after their language, and to the Jews according to their writing, and according to their language.

Akaandika kwa jina la mfalme Ahasuero, na kutia muhuri kwa pete ya mfalme, akazipeleka barua kwa matarishi, wamepanda farasi, wamepanda wanyama wepesi sana waliotumika kwa huduma ya mfalme, ndio waliozalishwa katika zizi la mfalme. Esta 8:10

He wrote the name of king Ahasuerus, and sealed it with the king's ring, and sent letters by post on horseback, riding on swift steeds that were used in the king's service, bred of the stud:

Katika barua hizo mfalme aliwaruhusu Wayahudi wakusanyike katika kila mji na kuzisimamia maisha zao, kuangamiza, na kuua, na kulifisha jeshi lote la watu na la jimbo watakaowaondokea, wao na wadogo wao na wanawake; na kuyachukua mali yao kuwa nyara; Esta 8:11

in which the king granted the Jews who were in every city to gather themselves together, and to stand for their life, to destroy, to kill, and to cause to perish, all the power of the people and province that would assault them, [their] little ones and women, and to take the spoil of them for a prey,

siku moja, katika majimbo yote ya mfalme Ahasuero, yaani, siku ya kumi na tatu ya mwezi wa kumi na mbili, ndio mwezi wa Adari. Esta 8:12

on one day in all the provinces of king Ahasuerus, [namely], on the thirteenth [day] of the twelfth month, which is the month Adar.

Nakili ya andiko, ya kupigwa mbiu katika kila jimbo, ilitangazwa kwa mataifa yote, na kwa Wayahudi, wawe tayari siku ile ile kujilipiza kisasi juu ya adui zao. Esta 8:13

A copy of the writing, that the decree should be given out in every province, was published to all the peoples, and that the Jews should be ready against that day to avenge themselves on their enemies.

Matarishi wakaondoka, wamepanda wanyama wepesi sana waliotumika kwa huduma ya mfalme, huku wakihimizwa na kusukumizwa kwa amri ya mfalme; kukapigwa mbiu huko Shushani ngomeni. Esta 8:14

So the posts who rode on swift steeds that were used in the king's service went out, being hurried and pressed on by the king's commandment; and the decree was given out in Shushan the palace.

Naye Mordekai akatoka usoni pa mfalme, amevaa mavazi ya kifalme, ya rangi ya samawi na nyeupe, mwenye taji kubwa ya dhahabu, na joho ya kitani safi na rangi ya zambarau. Mji wa Shushani wakapaza sauti, wakashangilia. Esta 8:15

Mordecai went forth from the presence of the king in royal clothing of blue and white, and with a great crown of gold, and with a robe of fine linen and purple: and the city of Shushan shouted and was glad.

Ikawa nuru na furaha na shangwe na heshima kwa Wayahudi. Esta 8:16

The Jews had light and gladness, and joy and honor.

Na katika kila jimbo, na kila mji, po pote palipowasili amri ya mfalme na mbiu yake, Wayahudi wakapata furaha na shangwe, karamu na sikukuu. Hata wengi wa watu wa nchi wakajifanya Wayahudi, kwa kuwa hofu ya Wayahudi imewaangukia. Esta 8:17

In every province, and in every city, wherever the king's commandment and his decree came, the Jews had gladness and joy, a feast and a good day. Many from among the peoples of the land became Jews; for the fear of the Jews was fallen on them.