Esta 5 Swahili & English

Listen/Download Audio
Esta 5 (Swahili) Esther 5 (English)

Ikawa siku ya tatu Esta alijivika mavazi yake ya kifalme, akasimama katika ua wa ndani wa nyumba ya mfalme, kuielekea nyumba ya mfalme; naye mfalme akaketi juu ya kiti chake cha enzi katika nyumba ya mfalme, kuuelekea mlango wa nyumba. Esta 5:1

Now it happened on the third day, that Esther put on her royal clothing, and stood in the inner court of the king's house, over against the king's house: and the king sat on his royal throne in the royal house, over against the entrance of the house.

Ikawa, mfalme alipomwona malkia Esta amesimama uani, yeye akapata kibali machoni pake; naye mfalme akamnyoshea Esta fimbo ya dhahabu aliyokuwa nayo mkononi. Basi Esta akakaribia, akaigusa ncha ya fimbo. Esta 5:2

It was so, when the king saw Esther the queen standing in the court, that she obtained favor in his sight; and the king held out to Esther the golden scepter that was in his hand. So Esther drew near, and touched the top of the scepter.

Mfalme akamwambia, Malkia Esta, wataka nini? Nayo ni haja gani uliyo nayo? Utapewa hata nusu ya ufalme. Esta 5:3

Then said the king to her, What will you, queen Esther? and what is your request? it shall be given you even to the half of the kingdom.

Esta akasema, Mfalme akiona vema, na aje leo, mfalme na Hamani, kwenye karamu niliyomwandalia. Esta 5:4

Esther said, If it seem good to the king, let the king and Haman come this day to the banquet that I have prepared for him.

Basi mfalme akasema, Mhimize Hamani, ili ifanyike kama Esta alivyosema. Hivyo mfalme na Hamani wakafika katika karamu ile aliyoiandaa Esta. Esta 5:5

Then the king said, Cause Haman to make haste, that it may be done as Esther has said. So the king and Haman came to the banquet that Esther had prepared.

Basi mfalme akamwambia Esta pale penye karamu ya divai, Dua yako ni nini? Nawe utapewa; na haja yako ni nini? Hata nusu ya ufalme utafanyiziwa. Esta 5:6

The king said to Esther at the banquet of wine, What is your petition? and it shall be granted you: and what is your request? even to the half of the kingdom it shall be performed.

Esta akajibu, na kusema, Dua yangu ni hii, na haja yangu ni hii, Esta 5:7

Then answered Esther, and said, My petition and my request is:

Ikiwa nimepata kibali machoni pa mfalme, na mfalme akiona vema kunipa niombalo, na kunifanyizia haja yangu, na aje tena mfalme na Hamani kwenye karamu nitakayowaandalia, nami kesho nitafanya kama vile mfalme alivyosema. Esta 5:8

if I have found favor in the sight of the king, and if it please the king to grant my petition, and to perform my request, let the king and Haman come to the banquet that I shall prepare for them, and I will do tomorrow as the king has said.

Basi Hamani alitoka siku ile kwa furaha na ukunjufu wa moyo; lakini Hamani alipomwona Mordekai mlangoni pa mfalme, ya kwamba hasimami wala kutetemeka mbele yake, alijaa ghadhabu juu ya Mordekai. Esta 5:9

Then went Haman forth that day joyful and glad of heart: but when Haman saw Mordecai in the king's gate, that he didn't stand up nor move for him, he was filled with wrath against Mordecai.

Walakini Hamani akajizuia, akaenda zake nyumbani kwake; akatuma kuwaita rafiki zake na Zereshi mkewe. Esta 5:10

Nevertheless Haman refrained himself, and went home; and he sent and fetched his friends and Zeresh his wife.

Naye Hamani akawasimulia habari za fahari ya mali zake, na wingi wa watoto wake, nayo mambo yote pia ambayo mfalme amemfanikisha katika hayo, na jinsi alivyompandisha juu ya maakida na watumishi wa mfalme. Esta 5:11

Haman recounted to them the glory of his riches, and the multitude of his children, and all the things in which the king had promoted him, and how he had advanced him above the princes and servants of the king.

Zaidi ya hayo Hamani akasema, Naye malkia Esta hakumkaribisha mtu ye yote pamoja na mfalme katika karamu aliyoiandaa, ila mimi peke yangu; hata na kesho pia nimealikwa naye pamoja na mfalme. Esta 5:12

Haman said moreover, Yes, Esther the queen did let no man come in with the king to the banquet that she had prepared but myself; and tomorrow also am I invited by her together with the king.

Bali haya yote yanifaa nini, pindi nimwonapo yule Mordekai, Myahudi, ameketi mlangoni pa mfalme? Esta 5:13

Yet all this avails me nothing, so long as I see Mordecai the Jew sitting at the king's gate.

Basi Zereshi mkewe akamwambia, na rafiki zake wote, Na ufanyizwe mti wa mikono hamsini urefu wake, na kesho asubuhi useme na mfalme ili Mordekai atundikwe juu yake; ndipo utakapoingia kwa kicheko pamoja na mfalme karamuni. Basi neno likampendeza Hamani, akaufanyiza ule mti. Esta 5:14

Then said Zeresh his wife and all his friends to him, Let a gallows be made fifty cubits high, and in the morning speak you to the king that Mordecai may be hanged thereon: then go you in merrily with the king to the banquet. The thing pleased Haman; and he caused the gallows to be made.