Esta 6 Swahili & English

Listen/Download Audio
Esta 6 (Swahili) Esther 6 (English)

Usiku ule mfalme hakupata usingizi; akaamuru aletewe kitabu cha maandiko ya taarifa, nayo yakasomwa mbele ya mfalme. Esta 6:1

On that night the king couldn't sleep; and he commanded to bring the book of records of the chronicles, and they were read before the king.

Ikaonekana kuwa imeandikwa ya kwamba Mordekai aliwachongea Bigthana na Tereshi, wasimamizi wawili wa mfalme, katika hao waliolinda mlango, waliotaka kumtia mikono mfalme Ahasuero. Esta 6:2

It was found written that Mordecai had told of Bigthana and Teresh, two of the king's chamberlains, of those who kept the threshold, who had sought to lay hands on the king Ahasuerus.

Mfalme akasema, Je! Ni heshima gani au jaha gani Mordekai aliyofanyiziwa kwa ajili ya hayo? Watumwa wa mfalme waliomhudumu wakamwambia, Hakuna alilofanyiziwa. Esta 6:3

The king said, What honor and dignity has been bestowed on Mordecai for this? Then the king's servants who ministered to him said, "Nothing has been done for him."

Mfalme akasema, Yupo nani behewani? Ikawa Hamani alikuwa ameingia katika ua wa nje wa nyumba ya mfalme, aseme na mfalme, ili kumtundika Mordekai juu ya mti ule aliomwekea tayari. Esta 6:4

The king said, "Who is in the court?" Now Haman was come into the outward court of the king's house, to speak to the king to hang Mordecai on the gallows that he had prepared for him.

Basi watumwa wa mfalme wakamwambia, Tazama, Hamani yupo, amesimama behewani. Mfalme akasema, Na aingie. Esta 6:5

The king's servants said to him, Behold, Haman stands in the court. The king said, Let him come in.

Basi Hamani akaingia. Mfalme akamwambia, Afanyiziwe nini yule ambaye mfalme apenda kumheshimu? Hamani akasema moyoni mwake, Ni nani ambaye mfalme apenda kumheshimu kuliko mimi? Esta 6:6

So Haman came in. The king said to him, What shall be done to the man whom the king delights to honor? Now Haman said in his heart, To whom would the king delight to do honor more than to myself?

Basi Hamani akamwambia mfalme, Yule ambaye mfalme apenda kumheshimu, Esta 6:7

Haman said to the king, For the man whom the king delights to honor,

na aletewe mavazi ya kifalme ambayo mfalme amezoea kuyavaa, na farasi ambaye mfalme humpanda mwenyewe, ambaye ametiwa taji ya kifalme kichwani; Esta 6:8

let royal clothing be brought which the king uses to wear, and the horse that the king rides on, and on the head of which a crown royal is set:

na yale mavazi na yule farasi akabidhiwe mkononi mmojawapo wa maakida wa mfalme aliye mstahiki; ili makusudi amvike yule ambaye mfalme apenda kumheshimu, na kumrakibisha juu ya farasi kuipitia njia kuu ya mjini, na kupiga mbiu mbele yake, kusema, Hivyo ndivyo atakavyofanyiziwa mtu yule ambaye mfalme apenda kumheshimu. Esta 6:9

and let the clothing and the horse be delivered to the hand of one of the king's most noble princes, that they may array the man therewith whom the king delights to honor, and cause him to ride on horseback through the street of the city, and proclaim before him, Thus shall it be done to the man whom the king delights to honor.

Basi mfalme akamwambia Hamani, Hima! Twaa mavazi na farasi kama ulivyosema, ukamfanyizie vivyo hivyo Mordekai, Myahudi, aketiye mlangoni pa mfalme; lisipungue neno lo lote katika yote uliyoyasema. Esta 6:10

Then the king said to Haman, Make haste, and take the clothing and the horse, as you have said, and do even so to Mordecai the Jew, who sits at the king's gate: let nothing fail of all that you have spoken.

Ndipo Hamani alipoyatwaa mavazi na farasi, akamvika Mordekai yale mavazi, akamrakibisha juu ya farasi kuipitia njia kuu ya mjini, akapiga mbiu mbele yake, Hivyo ndivyo atakavyofanyiziwa mtu yule ambaye mfalme apenda kumheshimu. Esta 6:11

Then took Haman the clothing and the horse, and arrayed Mordecai, and caused him to ride through the street of the city, and proclaimed before him, Thus shall it be done to the man whom the king delights to honor.

Kisha Mordekai akarudi kwenye mlango wa mfalme. Bali Hamani akaenda mbio nyumbani kwake, mwenye msiba, na kichwa chake kimefunikwa. Esta 6:12

Mordecai came again to the king's gate. But Haman hurried to his house, mourning and having his head covered.

Basi Hamani akawasimulia Zereshi mkewe na rafiki zake wote kila neno lililompata. Kisha watu wake wenye hekima na Zereshi mkewe wakamwambia, Ikiwa huyu Mordekai, ambaye umeanza kuanguka mbele yake, ni wa uzao wa Wayahudi, wewe hutamweza, bali kuanguka utaanguka mbele yake. Esta 6:13

Haman recounted to Zeresh his wife and all his friends everything that had happened to him. Then his wise men and Zeresh his wife said to him, If Mordecai, before whom you have begun to fall, be of the seed of the Jews, you shall not prevail against him, but shall surely fall before him.

Hata walipokuwa katika kusema naye, wasimamizi-wa-nyumba wa mfalme walifika, wakahimiza kumleta Hamani katika karamu ile aliyoiandaa Esta. Esta 6:14

While they were yet talking with him, came the king's chamberlains, and hurried to bring Haman to the banquet that Esther had prepared.