Esta Mlango 10 Esther

Esta 10:1

Basi mfalme Ahasuero alitoza kodi katika nchi na katika visiwa vya bahari.

Esta 10:2

Na matendo yake yote yenye nguvu na ya ushujaa, na habari zote za ukuu wake Mordekai ambao alipewa na mfalme, hazikuandikwa katika kitabu-cha-taarifa cha wafalme wa Umedi na Uajemi?

Esta 10:3

Kwa maana Mordekai Myahudi akawa wa pili wake mfalme Ahasuero, na mkuu wa Wayahudi, amependeza mbele ya jamii ya ndugu zake; ambaye aliwatafuta watu wake wema, na kuiangalia hali njema ya wazao wao wote.