Waefeso Mlango 5 Ephesians

Waefeso 5:1

Hivyo mfuateni Mungu, kama watoto wanaopendwa;

Waefeso 5:2

mkaenende katika upendo, kama Kristo naye alivyowapenda ninyi tena akajitoa kwa ajili yetu, sadaka na dhabihu kwa Mungu, kuwa harufu ya manukato.

Waefeso 5:3

Lakini uasherati usitajwe kwenu kamwe, wala uchafu wo wote wa kutamani, kama iwastahilivyo watakatifu;

Waefeso 5:4

wala aibu wala maneno ya upuzi wala ubishi; hayo hayapendezi; bali afadhali kushukuru.

Waefeso 5:5

Maana neno hili mnalijua hakika, ya kwamba hakuna mwasherati wala mchafu wala mwenye tamaa, ndiye mwabudu sanamu, aliye na urithi katika ufalme wa Kristo na Mungu.

Waefeso 5:6

Mtu asiwadanganye kwa maneno yasiyo na maana; kwa kuwa kwa sababu ya hayo hasira ya Mungu huwajia wana wa uasi.

Waefeso 5:7

Basi msishirikiane nao.

Waefeso 5:8

Kwa maana zamani ninyi mlikuwa giza, bali sasa mmekuwa nuru katika Bwana; enendeni kama watoto wa nuru,

Waefeso 5:9

kwa kuwa tunda la nuru ni katika wema wote na haki na kweli;

Waefeso 5:10

mkihakiki ni nini impendezayo Bwana.

Waefeso 5:11

Wala msishirikiane na matendo yasiyozaa ya giza, bali myakemee;

Waefeso 5:12

kwa kuwa yanayotendeka kwao kwa siri, ni aibu hata kuyanena.

Waefeso 5:13

Lakini yote yaliyokemewa hudhihirishwa na nuru maana kila kilichodhihirika ni nuru.

Waefeso 5:14

Hivyo husema, Amka, wewe usinziaye, Ufufuke katika wafu, Na Kristo atakuangaza.

Waefeso 5:15

Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima;

Waefeso 5:16

mkiukomboa wakati kwa maana zamani hizi ni za uovu.

Waefeso 5:17

Kwa sababu hiyo msiwe wajinga, bali mfahamu ni nini yaliyo mapenzi ya Bwana.

Waefeso 5:18

Tena msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; bali mjazwe Roho;

Waefeso 5:19

mkisemezana kwa zaburi na tenzi na nyimbo za rohoni, huku mkiimba na kumshangilia Bwana mioyoni mwenu;

Waefeso 5:20

na kumshukuru Mungu Baba sikuzote kwa mambo yote, katika jina lake Bwana wetu Yesu Kristo;

Waefeso 5:21

hali mnanyenyekeana katika kicho cha Kristo.

Waefeso 5:22

Enyi wake, watiini waume zenu kama kumtii Bwana wetu.

Waefeso 5:23

Kwa maana mume ni kichwa cha mkewe, kama Kristo naye ni kichwa cha Kanisa; naye ni mwokozi wa mwili.

Waefeso 5:24

Lakini kama vile Kanisa limtiivyo Kristo vivyo hivyo wake nao wawatii waume zao katika kila jambo.

Waefeso 5:25

Enyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo naye alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake;

Waefeso 5:26

ili makusudi alitakase na kulisafisha kwa maji katika neno;

Waefeso 5:27

apate kujiletea Kanisa tukufu, lisilo na ila wala kunyanzi wala lo lote kama hayo; bali liwe takatifu lisilo na mawaa.

Waefeso 5:28

Vivyo hivyo imewapasa waume nao kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe. Ampendaye mkewe hujipenda mwenyewe.

Waefeso 5:29

Maana hakuna mtu anayeuchukia mwili wake po pote; bali huulisha na kuutunza, kama Kristo naye anavyolitendea Kanisa.

Waefeso 5:30

Kwa kuwa tu viungo vya mwili wake.

Waefeso 5:31

Kwa sababu hiyo mtu atamwacha baba yake na mama yake, ataambatana na mkewe na hao wawili watakuwa mwili mmoja.

Waefeso 5:32

Siri hiyo ni kubwa; ila mimi nanena habari ya Kristo na Kanisa.

Waefeso 5:33

Lakini kila mtu ampende mke wake kama nafsi yake mwenyewe; wala mke asikose kumstahi mumewe.