Waefeso 2 Swahili & English

Listen/Download Audio
Waefeso 2 (Swahili) Ephesians 2 (English)

Nanyi mlikuwa wafu kwa sababu ya makosa na dhambi zenu; Waefeso 2:1

You were made alive when you were dead in transgressions and sins,

ambazo mliziendea zamani kwa kuifuata kawaida ya ulimwengu huu, na kwa kumfuata mfalme wa uwezo wa anga, roho yule atendaye kazi sasa katika wana wa kuasi; Waefeso 2:2

in which you once walked according to the course of this world, according to the prince of the powers of the air, the spirit who now works in the children of disobedience;

ambao zamani, sisi sote nasi tulienenda kati yao, katika tamaa za miili yetu, tulipoyatimiza mapenzi ya mwili na ya nia, tukawa kwa tabia yetu watoto wa hasira kama na hao wengine. Waefeso 2:3

among whom we also all once lived in the lust of our flesh, doing the desires of the flesh and of the mind, and were by nature children of wrath, even as the rest.

Lakini Mungu, kwa kuwa ni mwingi wa rehema, kwa mapenzi yake makuu aliyotupenda; Waefeso 2:4

But God, being rich in mercy, for his great love with which he loved us,

hata wakati ule tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa yetu; alituhuisha pamoja na Kristo; yaani, tumeokolewa kwa neema. Waefeso 2:5

even when we were dead through our trespasses, made us alive together with Christ (by grace you have been saved),

Akatufufua pamoja naye, akatuketisha pamoja naye katika ulimwengu wa roho, katika Kristo Yesu; Waefeso 2:6

and raised us up with him, and made us to sit with him in the heavenly places in Christ Jesus,

ili katika zamani zinazokuja audhihirishe wingi wa neema yake upitao kiasi kwa wema wake kwetu sisi katika Kristo Yesu. Waefeso 2:7

that in the ages to come he might show the exceeding riches of his grace in kindness toward us in Christ Jesus;

Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu; Waefeso 2:8

for by grace you have been saved through faith, and that not of yourselves; it is the gift of God,

wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu. Waefeso 2:9

not of works, that no one would boast.

Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo. Waefeso 2:10

For we are his workmanship, created in Christ Jesus for good works, which God prepared before that we would walk in them.

Kwa ajili ya hayo kumbukeni ya kwamba zamani ninyi, mlio watu wa Mataifa kwa jinsi ya mwili, mnaoitwa Wasiotahiriwa na wale wanaoitwa Waliotahiriwa, yaani, tohara ya mwilini iliyofanyika kwa mikono; Waefeso 2:11

Therefore remember that once you, the Gentiles in the flesh, who are called "uncircumcision" by that which is called "circumcision," (in the flesh, made by hands);

kwamba zamani zile mlikuwa hamna Kristo, mmefarakana na jamii ya Israeli, wageni wasio wa maagano ya ahadi ile. Mlikuwa hamna tumaini, hamna Mungu duniani. Waefeso 2:12

that you were at that time separate from Christ, alienated from the commonwealth of Israel, and strangers from the covenants of the promise, having no hope and without God in the world.

Lakini sasa, katika Kristo Yesu, ninyi mliokuwa mbali hapo kwanza mmekuwa karibu kwa damu yake Kristo. Waefeso 2:13

But now in Christ Jesus you who once were far off are made near in the blood of Christ.

Kwa maana yeye ndiye amani yetu, aliyetufanya sisi sote tuliokuwa wawili kuwa mmoja; akakibomoa kiambaza cha kati kilichotutenga. Waefeso 2:14

For he is our peace, who made both one, and broke down the middle wall of partition,

Naye akiisha kuuondoa ule uadui kwa mwili wake; ndiyo sheria ya amri zilizo katika maagizo; ili afanye hao wawili kuwa mtu mpya mmoja ndani ya nafsi yake; akafanya amani. Waefeso 2:15

having abolished in the flesh the hostility, the law of commandments contained in ordinances, that he might create in himself one new man of the two, making peace;

Akawapatanisha wote wawili na Mungu katika mwili mmoja, kwa njia ya msalaba, akiisha kuufisha ule uadui kwa huo msalaba. Waefeso 2:16

and might reconcile them both in one body to God through the cross, having killed the hostility thereby.

Akaja akahubiri amani kwenu ninyi mliokuwa mbali, na amani kwao wale waliokuwa karibu. Waefeso 2:17

He came and preached peace to you who were far off and to those who were near.

Kwa maana kwa yeye sisi sote tumepata njia ya kumkaribia Baba katika Roho mmoja. Waefeso 2:18

For through him we both have our access in one Spirit to the Father.

Basi tangu sasa ninyi si wageni wala wapitaji, bali ninyi ni wenyeji pamoja na watakatifu, watu wa nyumbani mwake Mungu. Waefeso 2:19

So then you are no longer strangers and foreigners, but you are fellow citizens with the saints, and of the household of God,

Mmejengwa juu ya msingi wa mitume na manabii, naye Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni. Waefeso 2:20

being built on the foundation of the apostles and prophets, Christ Jesus himself being the chief cornerstone;

Katika yeye jengo lote linaungamanishwa vema na kukua hata liwe hekalu takatifu katika Bwana. Waefeso 2:21

in whom the whole building, fitted together, grows into a holy temple in the Lord;

Katika yeye ninyi nanyi mnajengwa pamoja kuwa maskani ya Mungu katika Roho. Waefeso 2:22

in whom you also are built together for a habitation of God in the Spirit.