Amosi 9 Swahili & English

Listen/Download Audio
Amosi 9 (Swahili) Amos 9 (English)

Nalimwona Bwana akisimama karibu na madhabahu; akasema, vipigo vichwa vya nguzo, hata vizingiti vitikisike; vivunje vipande vipande juu ya kichwa cha kila mmoja wao; nami nitamwua mtu wa mwisho wao kwa upanga; hapana hata mmoja wao atakayekimbia, wala hataokoka hata mmoja wao. Amosi 9:1

I saw the Lord standing beside the altar, and he said, "Strike the tops of the pillars, that the thresholds may shake; and break them in pieces on the head of all of them; and I will kill the last of them with the sword: there shall not one of them flee away, and there shall not one of them escape.

Wajapochimba waingie katika kuzimu, mkono wangu utawatoa huko; nao wajapopanda hata mbinguni, nitawatelemsha toka huko. Amosi 9:2

Though they dig into Sheol, there my hand will take them; and though they climb up to heaven, there I will bring them down.

Nao wajapojificha katika kilele cha Karmeli, nitawatafuta na kuwatoa toka huko; na wajapositirika katika vilindi vya bahari nisiwaone, nitamwagiza joka huko, naye atawauma. Amosi 9:3

Though they hide themselves in the top of Carmel, I will search and take them out there; and though they be hid from my sight in the bottom of the sea, there I will command the serpent, and it will bite them.

Nao wajapokwenda hali ya kufungwa mbele ya adui zao, nitauagiza upanga huko, nao utawaua; nami nitawaelekezea macho yangu niwatende mabaya, wala si mema. Amosi 9:4

Though they go into captivity before their enemies, there I will command the sword, and it will kill them. I will set my eyes on them for evil, and not for good.

Kwa maana Bwana, MUNGU wa majeshi, ndiye aigusaye nchi, nayo ikayeyuka, na wote wakaao ndani yake wataomboleza; nayo itainuka yote pia kama Mto, nayo itakupwa tena kama Mto wa Misri. Amosi 9:5

For the Lord, Yahweh of Hosts, is he who touches the land and it melts, and all who dwell in it will mourn; and it will rise up wholly like the River, and will sink again, like the River of Egypt.

Yeye ndiye avijengaye vyumba vyake mbinguni, na kuweka misingi ya kuba yake juu ya nchi; yeye ndiye ayaitaye maji ya bahari, na kuyamwaga juu ya uso wa nchi; Bwana ndilo jina lake. Amosi 9:6

It is he who builds his chambers in the heavens, and has founded his vault on the earth; he who calls for the waters of the sea, and pours them out on the surface of the earth; Yahweh is his name.

Je! Ninyi si kama wana wa Wakushi kwangu mimi, enyi wana wa Israeli, asema Bwana? Je! Mimi sikuwapandisha Israeli toka nchi ya Misri, na Wafilisti toka Kaftori, na Washami toka Kiri? Amosi 9:7

Are you not like the children of the Ethiopians to me, children of Israel?" says Yahweh. "Haven't I brought up Israel out of the land of Egypt, and the Philistines from Caphtor, and the Syrians from Kir?

Angalieni, macho ya Bwana MUNGU yanauangalia ufalme wenye dhambi, nami nitauangamiza utoke juu ya uso wa dunia; lakini sitaiangamiza kabisa nyumba ya Yakobo, asema Bwana. Amosi 9:8

Behold, the eyes of the Lord Yahweh are on the sinful kingdom, and I will destroy it from off the surface of the earth; except that I will not utterly destroy the house of Jacob," says Yahweh.

Kwa maana, angalieni, nitatoa amri, nami nitaipepeta nyumba ya Israeli katika mataifa yote, kama vile ngano ipepetwavyo katika ungo lakini hata chembe moja iliyo ndogo haitaanguka chini. Amosi 9:9

"For, behold, I will command, and I will sift the house of Israel among all the nations, as grain is sifted in a sieve, yet not the least kernel will fall on the earth.

Wenye dhambi wote katika watu wangu watakufa kwa upanga, hao wasemao, Mabaya hayatatupata nyuma wala mbele. Amosi 9:10

All the sinners of my people will die by the sword, who say, 'Evil won't overtake nor meet us.'

Siku hiyo nitaiinua tena maskani ya Daudi iliyoanguka, na kuziba mahali palipobomoka; nami nitayainua magofu yake, na kuyajenga kama siku za kale; Amosi 9:11

In that day I will raise up the tent of David who is fallen, and close up its breaches, and I will raise up its ruins, and I will build it as in the days of old;

wapate kuyamiliki mabaki ya Edomu, na mataifa yote yaitwayo kwa jina langu, asema Bwana, afanyaye hayo. Amosi 9:12

that they may possess the remnant of Edom, and all the nations who are called by my name," says Yahweh who does this.

Angalieni, siku zinakuja, asema Bwana, ambazo huyo alimaye atamfikilia avunaye, na yeye akanyagaye zabibu atamfikilia apandaye mbegu; nayo milima itadondoza divai tamu, na vilima vyote vitayeyuka. Amosi 9:13

"Behold, the days come," says Yahweh, "That the plowman shall overtake the reaper, And the one treading grapes him who sows seed; And sweet wine will drip from the mountains, And flow from the hills.

Nami nitawarejeza tena watu wangu Israeli waliohamishwa, nao wataijenga miji iliyoachwa maganjo, na kukaa ndani yake; nao watapanda mizabibu katika mashamba, na kunywa divai yake; nao watafanyiza bustani, na kula matunda yake. Amosi 9:14

I will bring back the captivity of my people Israel, And they will rebuild the ruined cities, and inhabit them; and they will plant vineyards, and drink wine from them. They shall also make gardens, And eat the fruit of them.

Nami nitawapanda katika nchi yao, wala hawatang'olewa tena watoke katika nchi yao niliyowapa, asema Bwana, Mungu wako. Amosi 9:15

I will plant them on their land, And they will no more be plucked up out of their land which I have given them," says Yahweh your God.