Wimbo Ulio Bora 5 Swahili & English

Listen/Download Audio
Wimbo Ulio Bora 5 (Swahili) Song Of Songs 5 (English)

Naingia bustanini mwangu, umbu langu, bibi arusi, Nachuma manemane yangu na rihani, Nala sega la asali na asali yangu, Nanywa divai yangu na maziwa. Kaleni, rafiki zangu, kanyweni, Naam, nyweni sana, wapendwa wangu. Wimbo Ulio Bora 5:1

I have come into my garden, my sister, my bride. I have gathered my myrrh with my spice; I have eaten my honeycomb with my honey; I have drunk my wine with my milk. Friends Eat, friends! Drink, yes, drink abundantly, beloved. Beloved

Nalikuwa nimelala, lakini moyo wangu u macho, Sikiliza! Mpendwa wangu anabisha! Nifungulie, umbu langu, mpenzi wangu, Hua wangu, mkamilifu wangu, Kwa maana kichwa changu kimelowa umande, Nywele zangu zina manyunyu ya usiku. Wimbo Ulio Bora 5:2

I was asleep, but my heart was awake. It is the voice of my beloved who knocks: Open to me, my sister, my love, my dove, my undefiled; For my head is filled with dew, My hair with the dampness of the night.

Nimeivua kanzu yangu; niivaeje? Nimeitawadha miguu; niichafueje? Wimbo Ulio Bora 5:3

I have taken off my robe. Indeed, must I put it on? I have washed my feet. Indeed, must I soil them?

Mpendwa wangu aliutia mkono wake tunduni, Na moyo wangu ukachomeka kwa ajili yake. Wimbo Ulio Bora 5:4

My beloved thrust his hand in through the latch opening. My heart pounded for him.

Nikaondoka nimfungulie mpendwa wangu; Mikono yangu ilidondoza manemane, Na vidole vyangu matone ya manemane, Penye vipini vya komeo. Wimbo Ulio Bora 5:5

I rose up to open for my beloved. My hands dripped with myrrh, My fingers with liquid myrrh, On the handles of the lock.

Nalimfungulia mpendwa wangu, Lakini mpendwa wangu amegeuka amepita; (Nimezimia nafsi yangu aliponena), Nikamtafuta, nisimpate, Nikamwita, asiniitikie. Wimbo Ulio Bora 5:6

I opened to my beloved; But my beloved left; gone away. My heart went out when he spoke. I looked for him, but I didn't find him. I called him, but he didn't answer.

Walinzi wazungukao mjini waliniona, Wakanipiga na kunitia jeraha, Walinzi walindao kuta zake Wakaninyang'anya shela yangu. Wimbo Ulio Bora 5:7

The watchmen who go about the city found me. They beat me. They bruised me. The keepers of the walls took my cloak away from me.

Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu, Ninyi mkimwona mpendwa wangu, Ni nini mtakayomwambia? Ya kwamba nazimia kwa mapenzi. Wimbo Ulio Bora 5:8

I adjure you, daughters of Jerusalem, If you find my beloved, That you tell him that I am faint with love. Friends

Mpendwa wa namna gani ni mpendwa wako, Wewe uliye mzuri katika wanawake, Mpendwa wa namna gani ni mpendwa wako, Hata wewe utusihi hivyo? Wimbo Ulio Bora 5:9

How is your beloved better than another beloved, You fairest among women? How is your beloved better than another beloved, That you do so adjure us? Beloved

Mpendwa wangu ni mweupe, tena mwekundu, Mashuhuri miongoni mwa elfu kumi; Wimbo Ulio Bora 5:10

My beloved is white and ruddy. The best among ten thousand.

Kichwa chake ni kama dhahabu safi sana, Nywele zake ni za ukoka, nyeusi kama kunguru; Wimbo Ulio Bora 5:11

His head is like the purest gold. His hair is bushy, black as a raven.

Macho yake ni kama hua penye vijito, Wakioga kwa maziwa, wakiikalia mito iliyojaa; Wimbo Ulio Bora 5:12

His eyes are like doves beside the water brooks, Washed with milk, mounted like jewels.

Mashavu yake ni kama matuta ya rihani, Ambayo hufanyizwa manukato; Midomo yake ni kama nyinyoro, Inadondoza matone ya manemane; Wimbo Ulio Bora 5:13

His cheeks are like a bed of spices with towers of perfumes. His lips are like lilies, dropping liquid myrrh.

Mikono yake ni kama mianzi ya dhahabu, lliyopambwa kwa zabarajadi; Kiwiliwili chake kama kazi ya pembe, Iliyonakishiwa kwa yakuti samawi; Wimbo Ulio Bora 5:14

His hands are like rings of gold set with beryl. His body is like ivory work overlaid with sapphires.

Miguu yake ni kama nguzo za marimari, Zilizowekwa juu ya misingi ya dhahabu; Sura yake ni kama Lebanoni, Ni bora mfano wa mierezi; Wimbo Ulio Bora 5:15

His legs are like pillars of marble set on sockets of fine gold. His appearance is like Lebanon, excellent as the cedars.

Kinywa chake kimejaa maneno matamu, Ndiye mzuri sana pia pia. Ni huyu mpendwa wangu, ni huyu rafiki yangu, Enyi binti za Yerusalemu. Wimbo Ulio Bora 5:16

His mouth is sweetness; Yes, he is altogether lovely. This is my beloved, and this is my friend, Daughters of Jerusalem. Friends