Wimbo Ulio Bora 2 Swahili & English

Listen/Download Audio
Wimbo Ulio Bora 2 (Swahili) Song Of Songs 2 (English)

Mimi ni ua la uwandani, Ni nyinyoro ya mabondeni. Wimbo Ulio Bora 2:1

I am a rose of Sharon, A lily of the valleys.

Kama nyinyoro kati ya miiba, Kadhalika mpenzi wangu kati ya binti. Wimbo Ulio Bora 2:2

As a lily among thorns, So is my love among the daughters. Beloved

Kama mpera kati ya miti ya msituni, Kadhalika mpendwa wangu kati ya vijana. Naliketi kivulini mwake kwa furaha, Na matunda yake naliyaonja kuwa matamu. Wimbo Ulio Bora 2:3

As the apple tree among the trees of the wood, So is my beloved among the sons. I sat down under his shadow with great delight, His fruit was sweet to my taste.

Akanileta mpaka nyumba ya karamu, Na bendera yake juu yangu ni mapenzi. Wimbo Ulio Bora 2:4

He brought me to the banquet hall. His banner over me is love.

Nishibisheni zabibu, niburudisheni kwa mapera, Kwa maana nimezimia kwa mapenzi. Wimbo Ulio Bora 2:5

Strengthen me with raisins, Refresh me with apples; For I am faint with love.

Mkono wake wa kushoto uko chini ya kichwa changu, Nao wa kuume unanikumbatia! Wimbo Ulio Bora 2:6

His left hand is under my head. His right hand embraces me.

Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu, Kwa paa na kwa ayala wa porini, Msiyachochee mapenzi, wala kuyaamsha, Hata yatakapoona vema yenyewe. Wimbo Ulio Bora 2:7

I adjure you, daughters of Jerusalem, By the roes, or by the hinds of the field, That you not stir up, nor awaken love, Until it so desires.

Sikiliza! Ni mpendwa wangu! Tazama, anakuja, Akiruka milimani, akichachawa vilimani. Wimbo Ulio Bora 2:8

The voice of my beloved! Behold, he comes, Leaping on the mountains, Skipping on the hills.

Mpendwa wangu ni kama paa, au ayala. Tazama, asimama nyuma ya ukuta wetu, Achungulia dirishani, atazama kimiani. Wimbo Ulio Bora 2:9

My beloved is like a roe or a young hart. Behold, he stands behind our wall! He looks in at the windows. He glances through the lattice.

Mpendwa wangu alinena, akaniambia, Ondoka, mpenzi wangu, mzuri wangu, uje zako, Wimbo Ulio Bora 2:10

My beloved spoke, and said to me, Rise up, my love, my beautiful one, and come away.

Maana tazama, kaskazi imepita, Masika imekwisha, imekwenda zake; Wimbo Ulio Bora 2:11

For, behold, the winter is past. The rain is over and gone.

Maua yatokea katika nchi, Wakati wa kupelea umefika, Na sauti ya mwigo husikiwa kwetu. Wimbo Ulio Bora 2:12

The flowers appear on the earth; The time of the singing has come, And the voice of the turtle-dove is heard in our land.

Mtini wapevusha tini zake, Na mizabibu inachanua, Inatoa harufu yake nzuri; Ondoka, mpenzi wangu, mzuri wangu, uje zako. Wimbo Ulio Bora 2:13

The fig tree ripens her green figs. The vines are in blossom; They give forth their fragrance. Arise, my love, my beautiful one, And come away. Lover

Hua wangu, mafichoni mwa jabali, Katika sitara za magenge, Nitazame uso wako, nisikie sauti yako, Maana sauti yako ni tamu na uso wako mzuri. Wimbo Ulio Bora 2:14

My dove in the clefts of the rock, In the hiding places of the mountainside, Let me see your face. Let me hear your voice; For your voice is sweet, and your face is lovely.

Tukamatie mbweha, Wale mbweha wadogo, Waiharibuo mizabibu, Maana mizabibu yetu yachanua. Wimbo Ulio Bora 2:15

Catch for us the foxes, The little foxes that spoil the vineyards; For our vineyards are in blossom. Beloved

Mpendwa wangu ni wangu, na mimi ni wake; Hulisha kundi lake penye nyinyoro. Wimbo Ulio Bora 2:16

My beloved is mine, and I am his. He browses among the lilies.

Hata jua lipunge, na vivuli vikimbie, Unigeukie, mpendwa wangu, Nawe uwe kama paa, au ayala, Juu ya milima ya Betheri. Wimbo Ulio Bora 2:17

Until the day is cool, and the shadows flee away, Turn, my beloved, And be like a roe or a young hart on the mountains of Bether.