Warumi 7 Swahili & English

Listen/Download Audio
Warumi 7 (Swahili) Romans 7 (English)

Ndugu zangu, hamjui (maana nasema na hao waijuao sheria) ya kuwa torati humtawala mtu wakati anapokuwa yu hai? Warumi 7:1

Or don't you know, brothers{The word for "brothers" here and where context allows may also be correctly translated "brothers and sisters" or "siblings."} (for I speak to men who know the law), that the law has dominion over a man for as long as he lives?

Kwa maana mwanamke aliye na mume amefungwa na sheria kwa yule mume wakati anapokuwa yu hai; bali akifa yule mume, amefunguliwa ile sheria ya mume. Warumi 7:2

For the woman that has a husband is bound by law to the husband while he lives, but if the husband dies, she is discharged from the law of the husband.

Basi wakati awapo hai mumewe, kama akiwa na mume mwingine huitwa mzinzi. Ila mumewe akifa, amekuwa huru, hafungwi na sheria hiyo, hata yeye si mzinzi, ajapoolewa na mume mwingine. Warumi 7:3

So then if, while the husband lives, she is joined to another man, she would be called an adulteress. But if the husband dies, she is free from the law, so that she is no adulteress, though she is joined to another man.

Kadhalika, ndugu zangu, ninyi pia mmeifia torati, kwa njia ya mwili wa Kristo, mpate kuwa mali ya mwingine, yeye aliyefufuka katika wafu, kusudi tumzalie Mungu matunda. Warumi 7:4

Therefore, my brothers, you also were made dead to the law through the body of Christ, that you would be joined to another, to him who was raised from the dead, that we might bring forth fruit to God.

Kwa maana tulipokuwa katika hali ya mwili, tamaa za dhambi, zilizokuwako kwa sababu ya torati, zilitenda kazi katika viungo vyetu hata mkaizalia mauti mazao. Warumi 7:5

For when we were in the flesh, the sinful passions which were through the law, worked in our members to bring forth fruit to death.

Bali sasa tumefunguliwa katika torati, tumeifia hali ile iliyotupinga, ili sisi tupate kutumika katika hali mpya ya roho, si katika hali ya zamani, ya andiko. Warumi 7:6

But now we have been discharged from the law, having died to that in which we were held; so that we serve in newness of the spirit, and not in oldness of the letter.

Tusemeje, basi? Torati ni dhambi? Hasha! Walakini singalitambua dhambi ila kwa sheria; kwa kuwa singalijua kutamani, kama torati isingalisema, Usitamani. Warumi 7:7

What shall we say then? Is the law sin? May it never be! However, I wouldn't have known sin, except through the law. For I wouldn't have known coveting, unless the law had said, "You shall not covet."

Lakini dhambi ilipata nafasi kwa ile amri, ikafanya ndani yangu kila namna ya kutamani. Kwa maana dhambi bila sheria imekufa. Warumi 7:8

But sin, finding occasion through the commandment, produced in me all kinds of coveting. For apart from the law, sin is dead.

Nami nalikuwa hai hapo kwanza bila sheria; ila ilipokuja ile amri, dhambi ilihuika, nami nikafa. Warumi 7:9

I was alive apart from the law once, but when the commandment came, sin revived, and I died.

Nikaona ile amri iletayo uzima ya kuwa kwangu mimi ilileta mauti. Warumi 7:10

The commandment, which was for life, this I found to be for death;

Kwa maana dhambi, kwa kupata nafasi kwa ile amri, ilinidanganya, na kwa hiyo ikaniua. Warumi 7:11

for sin, finding occasion through the commandment, deceived me, and through it killed me.

Basi torati ni takatifu, na ile amri ni takatifu, na ya haki, na njema. Warumi 7:12

Therefore the law indeed is holy, and the commandment holy, and righteous, and good.

Basi je! Ile iliyo njema ilikuwa mauti kwangu mimi? Hasha! Bali dhambi, ili ionekane kuwa ni dhambi hasa, ilifanya mauti ndani yangu kwa njia ya ile njema, kusudi kwa ile amri dhambi izidi kuwa mbaya mno. Warumi 7:13

Did then that which is good become death to me? May it never be! But sin, that it might be shown to be sin, by working death to me through that which is good; that through the commandment sin might become exceeding sinful.

Kwa maana twajua ya kuwa torati asili yake ni ya rohoni; bali mimi ni mtu wa mwilini, nimeuzwa chini ya dhambi. Warumi 7:14

For we know that the law is spiritual, but I am fleshly, sold under sin.

Maana sijui nifanyalo, kwa sababu lile nilipendalo, silitendi; bali lile nilichukialo ndilo ninalolitenda. Warumi 7:15

For I don't know what I am doing. For I don't practice what I desire to do; but what I hate, that I do.

Lakini kama nikilitenda lile nisilolipenda, naikiri ile sheria ya kuwa ni njema. Warumi 7:16

But if what I don't desire, that I do, I consent to the law that it is good.

Basi sasa si mimi nafsi yangu ninayetenda hilo, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu Warumi 7:17

So now it is no more I that do it, but sin which dwells in me.

Kwa maana najua ya kuwa ndani yangu, yaani, ndani ya mwili wangu, halikai neno jema; kwa kuwa kutaka nataka, bali kutenda lililo jema sipati. Warumi 7:18

For I know that in me, that is, in my flesh, dwells no good thing. For desire is present with me, but I don't find it doing that which is good.

Kwa maana lile jema nilipendalo, silitendi; bali lile baya nisilolipenda ndilo nilitendalo. Warumi 7:19

For the good which I desire, I don't do; but the evil which I don't desire, that I practice.

Basi kama lile nisilolipenda ndilo nilitendalo, si mimi nafsi yangu nilitendaye, bali ni ile dhambi ikaayo ndani yangu. Warumi 7:20

But if what I don't desire, that I do, it is no more I that do it, but sin which dwells in me.

Basi nimeona sheria hii, ya kuwa kwangu mimi nitakaye kutenda lililo jema, lipo lililo baya. Warumi 7:21

I find then the law, that, to me, while I desire to do good, evil is present.

Kwa maana naifurahia sheria ya Mungu kwa utu wa ndani, Warumi 7:22

For I delight in God's law after the inward man,

lakini katika viungo vyangu naona sheria iliyo mbali, inapiga vita na ile sheria ya akili zangu, na kunifanya mateka ya ile sheria ya dhambi iliyo katika viungo vyangu. Warumi 7:23

but I see a different law in my members, warring against the law of my mind, and bringing me into captivity under the law of sin which is in my members.

Ole wangu, maskini mimi! Ni nani atakayeniokoa na mwili huu wa mauti? Warumi 7:24

What a wretched man I am! Who will deliver me out of the body of this death?

Namshukuru Mungu, kwa Yesu Kristo Bwana wetu. Basi, kama ni hivyo, mimi mwenyewe kwa akili zangu naitumikia sheria ya Mungu, bali kwa mwili wangu sheria ya dhambi. Warumi 7:25

I thank God through Jesus Christ, our Lord! So then with the mind, I myself serve God's law, but with the flesh, the sin's law.