Warumi 3 Swahili & English

Listen/Download Audio
Warumi 3 (Swahili) Romans 3 (English)

Basi Myahudi ana ziada gani? Na kutahiriwa kwafaa nini? Warumi 3:1

Then what advantage does the Jew have? Or what is the profit of circumcision?

Kwafaa sana kwa kila njia. Kwanza kwa kuwa wamekabidhiwa mausia ya Mungu. Warumi 3:2

Much in every way! Because first of all, they were entrusted with the oracles of God.

Ni nini, basi, ikiwa baadhi yao hawakuamini? Je! Kutokuamini kwao kutaubatili uaminifu wa Mungu? Warumi 3:3

For what if some were without faith? Will their lack of faith nullify the faithfulness of God?

Hasha! Mungu aonekane kuwa amini na kila mtu mwongo; kama ilivyoandikwa, Ili ujulike kuwa una haki katika maneno yako, Ukashinde uingiapo katika hukumu. Warumi 3:4

May it never be! Yes, let God be found true, but every man a liar. As it is written, "That you might be justified in your words, And might prevail when you come into judgment."

Lakini, ikiwa udhalimu wetu waithibitisha haki ya Mungu, tuseme nini? Je! Mungu ni dhalimu aletaye ghadhabu? (Nasema kwa jinsi ya kibinadamu.) Warumi 3:5

But if our unrighteousness commends the righteousness of God, what will we say? Is God unrighteous who inflicts wrath? I speak like men do.

Hasha! Kwa maana hapo Mungu atawezaje kuuhukumu ulimwengu? Warumi 3:6

May it never be! For then how will God judge the world?

Lakini, ikiwa kweli ya Mungu imezidi kudhihirisha utukufu wake kwa sababu ya uongo wangu, mbona mimi ningali nahukumiwa kuwa ni mwenye dhambi? Warumi 3:7

For if the truth of God through my lie abounded to his glory, why am I also still judged as a sinner?

Kwa nini tusiseme (kama tulivyosingiziwa, na kama wengine wanavyokaza kusema ya kwamba twasema hivyo), Na tufanye mabaya, ili yaje mema? Ambao kuhukumiwa kwao kuna haki. Warumi 3:8

Why not (as we are slanderously reported, and as some affirm that we say), "Let us do evil, that good may come?" Those who say so are justly condemned.

Ni nini basi? Tu bora kuliko wengine? La! Hata kidogo. Kwa maana tumekwisha kuwashitaki Wayahudi na Wayunani ya kwamba pia wamekuwa chini ya dhambi; Warumi 3:9

What then? Are we better than they? No, in no way. For we previously charged both Jews and Greeks, that they are all under sin.

kama ilivyoandikwa, ya kwamba, Hakuna mwenye haki hata mmoja. Warumi 3:10

As it is written, "There is no one righteous. No, not one.

Hakuna afahamuye; Hakuna amtafutaye Mungu. Warumi 3:11

There is no one who understands. There is no one who seeks after God.

Wote wamepotoka, wameoza wote pia; Hakuna mtenda mema, la! Hata mmoja. Warumi 3:12

They have all turned aside. They have together become unprofitable. There is no one who does good, No, not, so much as one."

Koo lao ni kaburi wazi, Kwa ndimi zao wametumia hila. Sumu ya fira i chini ya midomo yao. Warumi 3:13

"Their throat is an open tomb. With their tongues they have used deceit." "The poison of vipers is under their lips;"

Vinywa vyao vimejaa laana na uchungu. Warumi 3:14

"Whose mouth is full of cursing and bitterness."

Miguu yao ina mbio kumwaga damu. Warumi 3:15

"Their feet are swift to shed blood.

Uharibifu na mashaka yamo njiani mwao. Warumi 3:16

Destruction and misery are in their ways.

Wala njia ya amani hawakuijua. Warumi 3:17

The way of peace, they haven't known."

Kumcha Mungu hakupo machoni pao. Warumi 3:18

"There is no fear of God before their eyes."

Basi twajua ya kuwa mambo yote inenayo torati huyanena kwa hao walio chini ya torati, ili kila kinywa kifumbwe, na ulimwengu wote uwe chini ya hukumu ya Mungu; Warumi 3:19

Now we know that whatever things the law says, it speaks to those who are under the law, that every mouth may be closed, and all the world may be brought under the judgment of God.

kwa sababu hakuna mwenye mwili atakayehesabiwa haki mbele zake kwa matendo ya sheria; kwa maana kutambua dhambi huja kwa njia ya sheria. Warumi 3:20

Because by the works of the law, no flesh will be justified in his sight. For through the law comes the knowledge of sin.

Lakini sasa, haki ya Mungu imedhihirika pasipo sheria; inashuhudiwa na torati na manabii; Warumi 3:21

But now apart from the law, a righteousness of God has been revealed, being testified by the law and the prophets;

ni haki ya Mungu iliyo kwa njia ya imani katika Yesu Kristo kwa wote waaminio. Maana hakuna tofauti; Warumi 3:22

even the righteousness of God through faith in Jesus Christ to all and on all those who believe. For there is no distinction,

kwa sababu wote wamefanya dhambi, na kupungukiwa na utukufu wa Mungu; Warumi 3:23

for all have sinned, and fall short of the glory of God;

wanahesabiwa haki bure kwa neema yake, kwa njia ya ukombozi ulio katika Kristo Yesu; Warumi 3:24

being justified freely by his grace through the redemption that is in Christ Jesus;

ambaye Mungu amekwisha kumweka awe upatanisho kwa njia ya imani katika damu yake,ili aonyeshe haki yake ,kwa sababu ya kuziachilia katika ustahimili wa MUNGU dhambi zote zilzotangulia kufanywa. Warumi 3:25

whom God set forth to be an atoning sacrifice{or, a propitiation}, through faith in his blood, for a demonstration of his righteousness through the passing over of prior sins, in God's forbearance;

apate kuonyesha haki yake wakati huu, ili awe mwenye haki na mwenye kumhesabu haki yeye amwaminiye Yesu. Warumi 3:26

to demonstrate his righteousness at this present time; that he might himself be just, and the justifier of him who has faith in Jesus.

Ku wapi, basi, kujisifu? Kumefungiwa nje. Kwa sheria ya namna gani? Kwa sheria ya matendo? La! Bali kwa sheria ya imani. Warumi 3:27

Where then is the boasting? It is excluded. By what manner of law? Of works? No, but by a law of faith.

Basi, twaona ya kuwa mwanadamu huhesabiwa haki kwa imani pasipo matendo ya sheria. Warumi 3:28

We maintain therefore that a man is justified by faith apart from the works of the law.

Au je! Mungu ni Mungu wa Wayahudi tu? Siye Mungu wa Mataifa pia? Naam, ni Mungu wa Mataifa pia; Warumi 3:29

Or is God the God of Jews only? Isn't he the God of Gentiles also? Yes, of Gentiles also,

kama kwa kweli Mungu ni mmoja, atakayewahesabia haki wale waliotahiriwa katika imani, nao wale wasiotahiriwa atawahesabia haki kwa njia ya imani iyo hiyo. Warumi 3:30

since indeed there is one God who will justify the circumcised by faith, and the uncircumcised through faith.

Basi, je! Twaibatilisha sheria kwa imani hiyo? Hasha! Kinyume cha hayo twaithibitisha sheria. Warumi 3:31

Do we then nullify the law through faith? May it never be! No, we establish the law.