Warumi 16 Swahili & English

Listen/Download Audio
Warumi 16 (Swahili) Romans 16 (English)

Namkabidhi kwenu Fibi, ndugu yetu, aliye mhudumu wa kanisa lililoko Kenkrea; Warumi 16:1

I commend to you Phoebe, our sister, who is a servant{literally, deacon} of the assembly that is at Cenchreae,

kwamba mmpokee katika Bwana, kama iwapasavyo watakatifu; mkamsaidie katika neno lo lote atakalohitaji kwenu; kwa sababu yeye naye amekuwa msaidizi wa watu wengi, akanisaidia mimi pia. Warumi 16:2

that you receive her in the Lord, in a way worthy of the saints, and that you assist her in whatever matter she may need from you, for she herself also has been a helper of many, and of my own self.

Nisalimieni Priska na Akila, watenda kazi pamoja nami katika Kristo Yesu; Warumi 16:3

Greet Prisca and Aquila, my fellow workers in Christ Jesus,

waliokuwa tayari hata kukatwa kichwa kwa ajili ya maisha yangu; ambao ninawashukuru, wala si mimi tu, ila na makanisa ya Mataifa yote pia; nisalimieni na kanisa lililomo katika nyumba yao. Warumi 16:4

who for my life, laid down their own necks; to whom not only I give thanks, but also all the assemblies of the Gentiles.

Nisalimieni Epaineto, mpenzi wangu, aliye malimbuko ya Asia kwa Kristo. Warumi 16:5

Greet the assembly that is in their house. Greet Epaenetus, my beloved, who is the first fruits of Achaia to Christ.

Nisalimieni Mariamu, aliyejitaabisha sana kwa ajili yenu. Warumi 16:6

Greet Mary, who labored much for us.

Nisalimieni Androniko na Yunia, jamaa zangu, waliofungwa pamoja nami, ambao ni maarufu miongoni mwa mitume; nao walikuwa katika Kristo kabla yangu. Warumi 16:7

Greet Andronicus and Junias, my relatives and my fellow prisoners, who are notable among the apostles, who also were in Christ before me.

Nisalimieni Ampliato, mpenzi wangu katika Bwana. Warumi 16:8

Greet Amplias, my beloved in the Lord.

Nisalimieni Urbano, mtenda kazi pamoja nami katika Kristo, na Stakisi, mpenzi wangu. Warumi 16:9

Greet Urbanus, our fellow worker in Christ, and Stachys, my beloved.

Nisalimieni Apele, mwenye kukubaliwa katika Kristo. Nisalimieni watu wa nyumbani mwa Aristobulo. Warumi 16:10

Greet Apelles, the approved in Christ. Greet those who are of the household of Aristobulus.

Nisalimieni Herodioni, jamaa yangu. Nisalimieni watu wa nyumbani mwa Narkiso, walio katika Bwana. Warumi 16:11

Greet Herodion, my kinsman. Greet them of the household of Narcissus, who are in the Lord.

Nisalimieni Trifaina na Trifosa, wenye bidii katika Bwana. Nisalimieni Persisi, mpenzi aliyejitahidi sana katika Bwana. Warumi 16:12

Greet Tryphaena and Tryphosa, who labor in the Lord. Greet Persis, the beloved, who labored much in the Lord.

Nisalimieni Rufo, mteule katika Bwana, na mamaye, aliye mama yangu pia. Warumi 16:13

Greet Rufus, the chosen in the Lord, and his mother and mine.

Nisalimieni Asinkrito, Flegoni, Herme, Patroba, Herma, na ndugu walio pamoja nao. Warumi 16:14

Greet Asyncritus, Phlegon, Hermes, Patrobas, Hermas, and the brothers{The word for "brothers" here and where context allows may also be correctly translated "brothers and sisters" or "siblings."} who are with them.

Nisalimieni Filologo na Yulia, Nerea na dada yake, na Olimpa, na watakatifu wote walio pamoja nao. Warumi 16:15

Greet Philologus and Julia, Nereus and his sister, and Olympas, and all the saints who are with them.

Salimianeni kwa busu takatifu. Makanisa yote ya Kristo yawasalimu. Warumi 16:16

Greet one another with a holy kiss. The assemblies of Christ greet you.

Ndugu zangu, nawasihi, waangalieni wale wafanyao fitina na mambo ya kukwaza kinyume cha mafundisho mliyojifunza; mkajiepushe nao. Warumi 16:17

Now I beg you, brothers, look out for those who are causing the divisions and occasions of stumbling, contrary to the doctrine which you learned, and turn away from them.

Kwa sababu walio hivyo hawamtumikii Bwana wetu Kristo, bali matumbo yao wenyewe; na kwa maneno laini na ya kujipendekeza waidanganya mioyo ya watu wanyofu. Warumi 16:18

For those who are such don't serve our Lord, Jesus Christ, but their own belly; and by their smooth and flattering speech, they deceive the hearts of the innocent.

Maana utii wenu umewafikilia watu wote; basi nafurahi kwa ajili yenu, lakini nataka ninyi kuwa wenye hekima katika mambo mema, na wajinga katika mambo mabaya. Warumi 16:19

For your obedience has become known to all. I rejoice therefore over you. But I desire to have you wise in that which is good, but innocent in that which is evil.

Naye Mungu wa amani atamseta Shetani chini ya miguu yenu upesi. Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo na iwe pamoja nanyi. [Amina.] Warumi 16:20

And the God of peace will quickly crush Satan under your feet. The grace of our Lord Jesus Christ be with you.

Timotheo, mtenda kazi pamoja nami, awasalimu, na Lukio, na Yasoni, na Sosipatro, jamaa zangu. Warumi 16:21

Timothy, my fellow worker, greets you, as do Lucius, Jason, and Sosipater, my relatives.

Mimi Tertio, niliyeandika waraka huu, nawasalimu katika Bwana. Warumi 16:22

I, Tertius, who write the letter, greet you in the Lord.

Gayo, mwenyeji wangu na wa Kanisa lote pia awasalimu. Erasto, wakili wa mji, awasalimu, na Kwarto, ndugu yetu. Warumi 16:23

Gaius, my host and host of the whole assembly, greets you. Erastus, the treasurer of the city, greets you, as does Quartus, the brother.

Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo na iwe pamoja nanyi nyote. Amina.] Warumi 16:24

The grace of our Lord Jesus Christ be with you all! Amen.

Sasa na atukuzwe yeye awezaye kuwafanya imara, sawasawa na injili yangu na kwa kuhubiriwa kwake Yesu Kristo, sawasawa na ufunuo wa ile siri iliyositirika tangu zamani za milele, Warumi 16:25

{See Romans 14:23}

ikadhihirishwa wakati huu kwa maandiko ya manabii, ikajulikana na mataifa yote kama alivyoamuru Mungu wa milele, ili waitii Imani. Warumi 16:26

{See Romans 14:23}

Ndiye Mungu mwenye hekima peke yake. Utukufu una yeye kwa Yesu Kristo, milele na milele. Amina. Warumi 16:27

{See Romans 14:23} {TR places Romans 14:24-26 at the end of Romans instead of at the end of chapter 14, and numbers these verses 16:25-27.}