Warumi 12 Swahili & English

Listen/Download Audio
Warumi 12 (Swahili) Romans 12 (English)

Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana. Warumi 12:1

Therefore I urge you, brothers, by the mercies of God, to present your bodies a living sacrifice, holy, acceptable to God, which is your spiritual service.

Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu. Warumi 12:2

Don't be conformed to this world, but be transformed by the renewing of your mind, so that you may prove what is the good, well-pleasing, and perfect will of God.

Kwa maana kwa neema niliyopewa namwambia kila mtu aliyeko kwenu asinie makuu kupita ilivyompasa kunia; bali awe na nia ya kiasi, kama Mungu alivyomgawia kila mtu kiasi cha imani. Warumi 12:3

For I say, through the grace that was given me, to every man who is among you, not to think of himself more highly than he ought to think; but to think reasonably, as God has apportioned to each person a measure of faith.

Kwa kuwa kama vile katika mwili mmoja tuna viungo vingi, wala viungo vyote havitendi kazi moja; Warumi 12:4

For even as we have many members in one body, and all the members don't have the same function,

Vivyo hivyo na sisi tulio wengi tu mwili mmoja katika Kristo, na viungo, kila mmoja kwa mwenzake. Warumi 12:5

so we, who are many, are one body in Christ, and individually members one of another.

Basi kwa kuwa tuna karama zilizo mbalimbali, kwa kadiri ya neema mliyopewa; ikiwa unabii, tutoe unabii kwa kadiri ya imani; Warumi 12:6

Having gifts differing according to the grace that was given to us, if prophecy, let us prophesy according to the proportion of our faith;

ikiwa huduma, tuwemo katika huduma yetu; mwenye kufundisha, katika kufundisha kwake; Warumi 12:7

or service, let us give ourselves to service; or he who teaches, to his teaching;

mwenye kuonya, katika kuonya kwake; mwenye kukirimu, kwa moyo mweupe; mwenye kusimamia kwa bidii mwenye kurehemu, kwa furaha. Warumi 12:8

or he who exhorts, to his exhorting: he who gives, let him do it with liberality; he who rules, with diligence; he who shows mercy, with cheerfulness.

Pendo na lisiwe na unafiki lichukieni lililo ovu, mkiambatana na lililo jema. Warumi 12:9

Let love be without hypocrisy. Abhor that which is evil. Cling to that which is good.

Kwa pendo la udugu, mpendane ninyi kwa ninyi; kwa heshima mkiwatanguliza wenzenu; Warumi 12:10

In love of the brothers be tenderly affectionate one to another; in honor preferring one another;

kwa bidii, si walegevu; mkiwa na juhudi katika roho zenu; mkimtumikia Bwana; Warumi 12:11

not lagging in diligence; fervent in spirit; serving the Lord;

kwa tumaini, mkifurahi; katika dhiki, mkisubiri; katika kusali, mkidumu; Warumi 12:12

rejoicing in hope; enduring in troubles; continuing steadfastly in prayer;

kwa mahitaji ya watakatifu, mkifuata ukarimu; katika kukaribisha wageni mkijitahidi. Warumi 12:13

contributing to the needs of the saints; given to hospitality.

Wabarikini wanaowaudhi; barikini, wala msilaani. Warumi 12:14

Bless those who persecute you; bless, and don't curse.

Furahini pamoja nao wafurahio; lieni pamoja nao waliao. Warumi 12:15

Rejoice with those who rejoice. Weep with those who weep.

Mpatane nia zenu ninyi kwa ninyi. Msinie yaliyo makuu, lakini mkubali kushughulishwa na mambo manyonge. Msiwe watu wa kujivunia akili. Warumi 12:16

Be of the same mind one toward another. Don't set your mind on high things, but associate with the humble. Don't be wise in your own conceits.

Msimlipe mtu ovu kwa ovu. Angalieni yaliyo mema machoni pa watu wote. Warumi 12:17

Repay no one evil for evil. Respect what is honorable in the sight of all men.

Kama yamkini, kwa upande wenu, mkae katika amani na watu wote. Warumi 12:18

If it is possible, as much as it is up to you, be at peace with all men.

Wapenzi, msijilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu; maana imeandikwa, Kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa, anena Bwana. Warumi 12:19

Don't seek revenge yourselves, beloved, but give place to God's wrath. For it is written, "Vengeance belongs to me; I will repay, says the Lord."

Lakini, Adui yako akiwa na njaa, mlishe; akiwa na kiu, mnyweshe; maana ufanyapo hivyo, utampalia makaa ya moto kichwani pake. Warumi 12:20

Therefore "If your enemy is hungry, feed him. If he is thirsty, give him a drink. For in doing so, you will heap coals of fire on his head."

Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema. Warumi 12:21

Don't be overcome by evil, but overcome evil with good.