Warumi 10 Swahili & English

Listen/Download Audio
Warumi 10 (Swahili) Romans 10 (English)

Ndugu zangu, nitakayo sana moyoni mwangu, na dua yangu nimwombayo Mungu, ni kwa ajili yao, ili waokolewe. Warumi 10:1

Brothers, my heart's desire and my prayer to God is for Israel, that they may be saved.

Kwa maana nawashuhudia kwamba wana juhudi kwa ajili ya Mungu, lakini si katika maarifa. Warumi 10:2

For I testify about them that they have a zeal for God, but not according to knowledge.

Kwa maana, wakiwa hawaijui haki ya Mungu, na wakitaka kuithibitisha haki yao wenyewe, hawakujitia chini ya haki ya Mungu. Warumi 10:3

For being ignorant of God's righteousness, and seeking to establish their own righteousness, they didn't subject themselves to the righteousness of God.

Kwa maana Kristo ni mwisho wa sheria, ili kila aaminiye ahesabiwe haki. Warumi 10:4

For Christ is the fulfillment{or, completion, or end} of the law for righteousness to everyone who believes.

Kwa maana Musa aliandika juu ya haki itokayo kwa sheria, ya kuwa, Mtu afanyaye hiyo ataishi kwa hiyo. Warumi 10:5

For Moses writes about the righteousness of the law, "The one who does them will live by them."

Bali ile haki ipatikanayo kwa imani yanena hivi, Usiseme moyoni mwako, Ni nani atakayepanda kwenda mbinguni? (Yaani, ni kumleta Kristo chini), Warumi 10:6

But the righteousness which is of faith says this, "Don't say in your heart, 'Who will ascend into heaven?' (that is, to bring Christ down);

au, Ni nani atakayeshuka kwenda kuzimuni? (Yaani, ni kumleta Kristo juu, kutoka kwa wafu.) Warumi 10:7

or, 'Who will descend into the abyss?' (that is, to bring Christ up from the dead.)"

Lakini yanenaje? Lile neno li karibu nawe, katika kinywa chako, na katika moyo wako; yaani, ni lile neno la imani tulihubirilo. Warumi 10:8

But what does it say? "The word is near you, in your mouth, and in your heart;" that is, the word of faith, which we preach:

Kwa sababu, ukimkiri Yesu kwa kinywa chako ya kuwa ni Bwana, na kuamini moyoni mwako ya kuwa Mungu alimfufua katika wafu, utaokoka. Warumi 10:9

that if you will confess with your mouth the Lord Jesus, and believe in your heart that God raised him from the dead, you will be saved.

Kwa maana kwa moyo mtu huamini hata kupata haki, na kwa kinywa hukiri hata kupata wokovu. Warumi 10:10

For with the heart, one believes unto righteousness; and with the mouth confession is made unto salvation.

Kwa maana andiko lanena, Kila amwaminiye hatatahayarika. Warumi 10:11

For the Scripture says, "Whoever believes in him will not be disappointed."

Kwa maana hakuna tofauti ya Myahudi na Myunani; maana yeye yule ni Bwana wa wote, mwenye utajiri kwa wote wamwitao; Warumi 10:12

For there is no distinction between Jew and Greek; for the same Lord is Lord of all, and is rich to all who call on him.

kwa kuwa, Kila atakayeliitia Jina la Bwana ataokoka. Warumi 10:13

For, "Whoever will call on the name of the Lord will be saved."

Basi wamwiteje yeye wasiyemwamini? Tena wamwaminije yeye wasiyemsikia? Tena wamsikieje pasipo mhubiri? Warumi 10:14

How then will they call on him in whom they have not believed? How will they believe in him whom they have not heard? How will they hear without a preacher?

Tena wahubirije, wasipopelekwa? Kama ilivyoandikwa, Ni mizuri kama nini miguu yao wahubirio habari ya mema! Warumi 10:15

And how will they preach unless they are sent? As it is written: "How beautiful are the feet of those who preach the Gospel of peace, Who bring glad tidings of good things!"

Lakini si wote walioitii ile habari njema. Kwa maana Isaya asema, Bwana, ni nani aliyeziamini habari zetu? Warumi 10:16

But they didn't all listen to the glad news. For Isaiah says, "Lord, who has believed our report?"

Basi imani, chanzo chake ni kusikia; na kusikia huja kwa neno la Kristo. Warumi 10:17

So faith comes by hearing, and hearing by the word of God.

Lakini nasema, Je! Wao hawakusikia? Naam, wamesikia, Sauti yao imeenea duniani mwote, Na maneno yao hata miisho ya ulimwengu. Warumi 10:18

But I say, didn't they hear? Yes, most assuredly, "Their sound went out into all the earth, Their words to the ends of the world."

Lakini nasema, Je! Waisraeli hawakufahamu? Kwanza Musa anena, Nitawatia wivu kwa watu ambao si taifa, Kwa taifa lisilo na fahamu nitawaghadhibisha. Warumi 10:19

But I ask, didn't Israel know? First Moses says, "I will provoke you to jealousy with that which is no nation, With a nation void of understanding I will make you angry."

Na Isaya anao ujasiri mwingi, asema, Nalipatikana nao wasionitafuta, Nalidhihirika kwao wasioniulizia. Warumi 10:20

Isaiah is very bold, and says, "I was found by those who didn't seek me. I was revealed to those who didn't ask for me."

Lakini kwa Israeli asema, Mchana kutwa naliwanyoshea mikono watu wasiotii na wakaidi. Warumi 10:21

But as to Israel he says, "All day long I stretched out my hands to a disobedient and contrary people."