Waebrania 6 Swahili & English

Listen/Download Audio
Waebrania 6 (Swahili) Hebrews 6 (English)

Kwa sababu hiyo, tukiacha kuyanena mafundisho ya kwanza ya Kristo, tukaze mwendo ili tuufikilie utimilifu; tusiweke msingi tena wa kuzitubia kazi zisizo na uhai, na wa kuwa na imani kwa Mungu, Waebrania 6:1

Therefore leaving the doctrine of the first principles of Christ, let us press on to perfection--not laying again a foundation of repentance from dead works, of faith toward God,

na wa mafundisho ya mabatizo, na kuwekea mikono, na kufufuliwa wafu, na hukumu ya milele. Waebrania 6:2

of the teaching of baptisms, of laying on of hands, of resurrection of the dead, and of eternal judgment.

Na hayo tutafanya Mungu akitujalia. Waebrania 6:3

This will we do, if God permits.

Kwa maana hao waliokwisha kupewa nuru, na kukionja kipawa cha mbinguni, na kufanywa washirika wa Roho Mtakatifu, Waebrania 6:4

For concerning those who were once enlightened and tasted of the heavenly gift, and were made partakers of the Holy Spirit,

na kulionja neno zuri la Mungu, na nguvu za zamani zijazo, Waebrania 6:5

and tasted the good word of God, and the powers of the age to come,

wakaanguka baada ya hayo, haiwezekani kuwafanya upya tena hata wakatubu; kwa kuwa wamsulibisha Mwana wa Mungu mara ya pili kwa nafsi zao, na kumfedhehi kwa dhahiri. Waebrania 6:6

and then fell away, it is impossible to renew them again to repentance; seeing they crucify the Son of God for themselves again, and put him to open shame.

Maana nchi inayoinywa mvua inayoinyeshea mara kwa mara, na kuzaa mboga zenye manufaa kwa hao ambao kwa ajili yao yalimwa, hushiriki baraka zitokazo kwa Mungu; Waebrania 6:7

For the land which has drunk the rain that comes often on it, and brings forth a crop suitable for them for whose sake it is also tilled, receives blessing from God;

bali ikitoa miiba na magugu hukataliwa na kuwa karibu na laana; ambayo mwisho wake ni kuteketezwa. Waebrania 6:8

but if it bears thorns and thistles, it is rejected and near being cursed, whose end is to be burned.

Lakini, wapenzi, ijapokuwa twanena hayo, katika habari zenu tumesadiki mambo yaliyo mazuri zaidi, na yaliyo na wokovu. Waebrania 6:9

But, beloved, we are persuaded of better things for you, and things that accompany salvation, even though we speak like this.

Maana Mungu si dhalimu hata aisahau kazi yenu, na pendo lile mlilolidhihirisha kwa jina lake, kwa kuwa mmewahudumia watakatifu, na hata hivi sasa mngali mkiwahudumia. Waebrania 6:10

For God is not unrighteous, so as to forget your work and the labor of love which you showed toward his name, in that you served the saints, and still do serve them.

Nasi twataka sana kila mmoja wenu aidhihirishe bidii ile ile, kwa utimilifu wa matumaini hata mwisho; Waebrania 6:11

We desire that each one of you may show the same diligence to the fullness of hope even to the end,

ili msiwe wavivu, bali mkawe wafuasi wa hao wazirithio ahadi kwa imani na uvumilivu. Waebrania 6:12

that you won't be sluggish, but imitators of those who through faith and patience inherited the promises.

Kwa maana Mungu, alipompa Ibrahimu ahadi, kwa sababu alikuwa hana mkubwa kuliko yeye mwenyewe wa kumwapa, aliapa kwa nafsi yake, Waebrania 6:13

For when God made a promise to Abraham, since he could swear by none greater, he swore by himself,

akisema, Hakika yangu kubariki nitakubariki, na kuongeza nitakuongeza. Waebrania 6:14

saying, "Most surely I will bless you, and I will surely multiply you."

Na hivyo kwa kuvumilia akaipata ile ahadi. Waebrania 6:15

Thus, having patiently endured, he obtained the promise.

Maana wanadamu huapa kwa yeye aliye mkuu kuliko wao; na kwao ukomo wa mashindano yote ya maneno ni kiapo, kwa kuyathibitisha. Waebrania 6:16

For men indeed swear by a greater one, and in every dispute of theirs the oath is final for confirmation.

Katika neno hilo Mungu, akitaka kuwaonyesha zaidi sana warithio ile ahadi, jinsi mashauri yake yasivyoweza kubadilika, alitia kiapo katikati; Waebrania 6:17

In this way God, being determined to show more abundantly to the heirs of the promise the immutability of his counsel, interposed with an oath;

ili kwa vitu viwili visivyoweza kubadilika, ambavyo katika hivyo Mungu hawezi kusema uongo, tupate faraja iliyo imara, sisi tuliokimbilia kuyashika matumaini yale yawekwayo mbele yetu; Waebrania 6:18

that by two immutable things, in which it is impossible for God to lie, we may have a strong encouragement, who have fled for refuge to take hold of the hope set before us.

tuliyo nayo kama nanga ya roho, yenye salama, yenye nguvu, yaingiayo hata mle mlimo ndani ya pazia, Waebrania 6:19

This hope we have as an anchor of the soul, a hope both sure and steadfast and entering into that which is within the veil;

alimoingia Yesu kwa ajili yetu, mtangulizi wetu, amekuwa kuhani mkuu hata milele kwa mfano wa Melkizedeki. Waebrania 6:20

where as a forerunner Jesus entered for us, having become a high priest forever after the order of Melchizedek.