Waebrania 13 Swahili & English

Listen/Download Audio
Waebrania 13 (Swahili) Hebrews 13 (English)

Upendano wa ndugu na udumu. Waebrania 13:1

Let brotherly love continue.

Msisahau kuwafadhili wageni; maana kwa njia hii wengine wamewakaribisha malaika pasipo kujua. Waebrania 13:2

Don't forget to show hospitality to strangers, for in doing so, some have entertained angels without knowing it.

Wakumbukeni hao waliofungwa kana kwamba mmefungwa pamoja nao; na hao wanaodhulumiwa, kwa vile ninyi nanyi mlivyo katika mwili. Waebrania 13:3

Remember those who are in bonds, as bound with them; and those who are ill-treated, since you are also in the body.

Ndoa na iheshimiwe na watu wote, na malazi yawe safi; kwa maana waasherati na wazinzi Mungu atawahukumia adhabu. Waebrania 13:4

Let marriage be held in honor among all, and let the bed be undefiled: but God will judge the sexually immoral and adulterers.

Msiwe na tabia ya kupenda fedha; mwe radhi na vitu mlivyo navyo; kwa kuwa yeye mwenyewe amesema, Sitakupungukia kabisa, wala sitakuacha kabisa. Waebrania 13:5

Be free from the love of money, content with such things as you have, for he has said, "I will in no way leave you, neither will I in any way forsake you."

Hata twathubutu kusema, Bwana ndiye anisaidiaye, sitaogopa; Mwanadamu atanitenda nini? Waebrania 13:6

So that with good courage we say, "The Lord is my helper. I will not fear. What can man do to me?"

Wakumbukeni wale waliokuwa wakiwaongoza, waliowaambia neno la Mungu; tena, kwa kuuchunguza sana mwisho wa mwenendo wao, iigeni imani yao. Waebrania 13:7

Remember your leaders, men who spoke to you the word of God, and considering the results of their conduct, imitate their faith.

Yesu Kristo ni yeye yule, jana na leo na hata milele. Waebrania 13:8

Jesus Christ is the same yesterday, today, and forever.

Msichukuliwe na mafundisho ya namna nyingine nyingine, na ya kigeni; maana ni vizuri moyo ufanywe imara kwa neema, wala si kwa vyakula, ambavyo wao waliokwenda navyo hawakupata faida. Waebrania 13:9

Don't be carried away by various and strange teachings, for it is good that the heart be established by grace, not by food, through which those who were so occupied were not benefited.

Tuna madhabahu ambayo wale waihudumiao ile hema hawana ruhusa kula vitu vyake. Waebrania 13:10

We have an altar from which those who serve the holy tabernacle have no right to eat.

Maana wanyama wale ambao damu yao huletwa ndani ya patakatifu na kuhani mkuu kwa ajili ya dhambi, viwiliwili vyao huteketezwa nje ya kambi. Waebrania 13:11

For the bodies of those animals, whose blood is brought into the holy place by the high priest as an offering for sin, are burned outside of the camp.

Kwa ajili hii Yesu naye, ili awatakase watu kwa damu yake mwenyewe, aliteswa nje ya lango. Waebrania 13:12

Therefore Jesus also, that he might sanctify the people through his own blood, suffered outside of the gate.

Basi na tutoke tumwendee nje ya kambi, tukichukua shutumu lake. Waebrania 13:13

Let us therefore go forth to him outside of the camp, bearing his reproach.

Maana hapa hatuna mji udumuo, bali twautafuta ule ujao. Waebrania 13:14

For we don't have here an enduring city, but we seek that which is to come.

Basi, kwa njia yake yeye, na tumpe Mungu dhabihu ya sifa daima, yaani, tunda la midomo iliungamayo jina lake. Waebrania 13:15

Through him, then, let us offer up a sacrifice of praise to God continually, that is, the fruit of lips which make confession to his name.

Lakini msisahau kutenda mema na kushirikiana; maana sadaka kama hizi ndizo zimpendezazo Mungu. Waebrania 13:16

But don't forget to be doing good and sharing, for with such sacrifices God is well pleased.

Watiini wenye kuwaongoza, na kuwanyenyekea; maana wao wanakesha kwa ajili ya roho zenu, kama watu watakaotoa hesabu, ili kwamba wafanye hivyo kwa furaha wala si kwa kuugua; maana isingewafaa ninyi. Waebrania 13:17

Obey your leaders and submit to them, for they watch on behalf of your souls, as those who will give account, that they may do this with joy, and not with groaning, for that would be unprofitable for you.

Tuombeeni; maana tunaamini kwamba tuna dhamiri njema, tukitaka kuwa na mwenendo mwema katika mambo yote. Waebrania 13:18

Pray for us, for we are persuaded that we have a good conscience, desiring to live honorably in all things.

Nami nawasihi zaidi sana kufanya hayo ili nirudishwe kwenu upesi. Waebrania 13:19

I strongly urge you to do this, that I may be restored to you sooner.

Basi, Mungu wa amani aliyemleta tena kutoka kwa wafu Mchungaji Mkuu wa kondoo, kwa damu ya agano la milele, yeye Bwana wetu Yesu, Waebrania 13:20

Now may the God of peace, who brought again from the dead the great shepherd of the sheep with the blood of an eternal covenant, our Lord Jesus,

awafanye ninyi kuwa wakamilifu katika kila tendo jema, mpate kuyafanya mapenzi yake, naye akifanya ndani yetu lipendezalo mbele zake, kwa Yesu Kristo; utukufu una yeye milele na milele. Amina. Waebrania 13:21

make you complete in every good work to do his will, working in you that which is well pleasing in his sight, through Jesus Christ, to whom be the glory forever and ever. Amen.

Lakini nawasihi, ndugu, mchukuliane na neno hili lenye maonyo maana nimewaandikia kwa maneno machache. Waebrania 13:22

But I exhort you, brothers, endure the word of exhortation, for I have written to you in few words.

Jueni ya kuwa ndugu yetu Timotheo amekwisha kufunguliwa; ambaye, akija upesi, nitaonana nanyi pamoja naye. Waebrania 13:23

Know that our brother Timothy has been freed, with whom, if he comes shortly, I will see you.

Wasalimuni wote wenye kuwaongoza, na watakatifu wote; hao walio wa Italia wanawasalimu. Waebrania 13:24

Greet all of your leaders and all the saints. The Italians greet you.

Neema na iwe nanyi nyote. Waebrania 13:25

Grace be with you all. Amen.