Waebrania 2 Swahili & English

Listen/Download Audio
Waebrania 2 (Swahili) Hebrews 2 (English)

Kwa hiyo imetupasa kuyaangalia zaidi hayo yaliyosikiwa tusije tukayakosa. Waebrania 2:1

Therefore we ought to pay greater attention to the things that were heard, lest perhaps we drift away.

Kwa maana, ikiwa lile neno lililonenwa na malaika lilikuwa imara, na kila kosa na uasi ulipata ujira wa haki, Waebrania 2:2

For if the word spoken through angels proved steadfast, and every transgression and disobedience received a just recompense;

sisi je! Tutapataje kupona, tusipojali wokovu mkuu namna hii? Ambao kwanza ulinenwa na Bwana, kisha ukathibitika kwetu na wale waliosikia; Waebrania 2:3

how will we escape if we neglect so great a salvation-- which at the first having been spoken through the Lord, was confirmed to us by those who heard;

Mungu naye akishuhudu pamoja nao kwa ishara na ajabu na nguvu za namna nyingi, na kwa magawanyo ya Roho Mtakatifu, kama alivyopenda mwenyewe. Waebrania 2:4

God also bearing witness with them, both by signs and wonders, and by various works of power, and by gifts of the Holy Spirit, according to his own will?

Maana hakuuweka chini ya malaika ulimwengu ule ujao tunaounena, ila mtu mmoja ameshuhudia hivi mahali fulani, akisema, Waebrania 2:5

For he didn't subject the world to come, of which we speak, to angels.

Mwanadamu ni nini hata umkumbuke, Ama mwana wa binadamu, hata umwangalie? Waebrania 2:6

But one has somewhere testified, saying, "What is man, that you think of him? Or the son of man, that you care for him?

Umemfanya mdogo punde kuliko malaika, Umemvika taji ya utukufu na heshima, Umemtawaza juu ya kazi za mikono yako; Waebrania 2:7

You made him a little lower than the angels; You crowned him with glory and honor.{TR adds "and set him over the works of your hands"}

Umeweka vitu vyote chini ya nyayo zake. Kwa maana katika kuweka vitu vyote chini yake hakusaza kitu kisichowekwa chini yake. Lakini sasa bado hatujaona vitu vyote kutiwa chini yake. Waebrania 2:8

You have put all things in subjection under his feet." For in that he subjected all things to him, he left nothing that is not subject to him. But now we don't see all things subjected to him, yet.

ila twamwona yeye aliyefanywa mdogo punde kuliko malaika, yaani, Yesu, kwa sababu ya maumivu ya mauti, amevikwa taji ya utukufu na heshima, ili kwa neema ya Mungu aionje mauti kwa ajili ya kila mtu. Waebrania 2:9

But we see him who has been made a little lower than the angels, Jesus, because of the suffering of death crowned with glory and honor, that by the grace of God he should taste of death for everyone.

Kwa kuwa ilimpasa yeye, ambaye kwa ajili yake na kwa njia yake vitu vyote vimekuwapo, akileta wana wengi waufikilie utukufu, kumkamilisha kiongozi mkuu wa wokovu wao kwa njia ya mateso. Waebrania 2:10

For it became him, for whom are all things, and through whom are all things, in bringing many children to glory, to make the author of their salvation perfect through sufferings.

Maana yeye atakasaye na hao wanaotakaswa wote pia watoka kwa mmoja. Kwa ajili hii haoni haya kuwaita ndugu zake; Waebrania 2:11

For both he who sanctifies and those who are sanctified are all from one, for which cause he is not ashamed to call them brothers{The word for "brothers" here and where context allows may also be correctly translated "brothers and sisters" or "siblings."},

akisema, Nitalihubiri jina lako kwa ndugu zangu; Katikati ya kanisa nitakuimbia sifa. Waebrania 2:12

saying, "I will declare your name to my brothers. In the midst of the congregation I will sing your praise."

Na tena, Nitakuwa nimemtumaini yeye. Na tena, Tazama,mimi nipo hapa na watoto niliopewa na Mungu. Waebrania 2:13

Again, "I will put my trust in him." Again, "Behold, here am I and the children whom God has given me."

Basi, kwa kuwa watoto wameshiriki damu na mwili, yeye naye vivyo hivyo alishiriki yayo hayo, ili kwa njia ya mauti amharibu yeye aliyekuwa na nguvu za mauti, yaani, Ibilisi, Waebrania 2:14

Since then the children have shared in flesh and blood, he also himself in like manner partook of the same, that through death he might bring to nothing him who had the power of death, that is, the devil,

awaache huru wale ambao kwamba maisha yao yote kwa hofu ya mauti walikuwa katika hali ya utumwa. Waebrania 2:15

and might deliver all of them who through fear of death were all their lifetime subject to bondage.

Maana ni hakika, hatwai asili ya malaika, ila atwaa asili ya mzao wa Ibrahimu. Waebrania 2:16

For most assuredly, not to angels does he give help, but he gives help to the seed of Abraham.

Hivyo ilimpasa kufananishwa na ndugu zake katika mambo yote, apate kuwa kuhani mkuu mwenye rehema, mwaminifu katika mambo ya Mungu, ili afanye suluhu kwa dhambi za watu wake. Waebrania 2:17

Therefore he was obligated in all things to be made like his brothers, that he might become a merciful and faithful high priest in things pertaining to God, to make atonement for the sins of the people.

Na kwa kuwa mwenyewe aliteswa alipojaribiwa, aweza kuwasaidia wao wanaojaribiwa. Waebrania 2:18

For in that he himself has suffered being tempted, he is able to help those who are tempted.